bayyinaat

Published time: 06 ,October ,2017      11:59:41
Leo hii katika nchi zilizoendelea zaidi asilimia 85, wanawake wenye umri kati ya miaka 25 hadi 49 pamoja na maisha ya kando ya kifamilia, wameendeleza kipaji chao katika maisha yao ya kifamilia. Wanawake wenye kujishughulisha wengi hufanya jitihada za kulea watoto au familia zao au watu wanaowahusu kwa kufanya mlinganisho wa kazini na watoto wao......
News ID: 102

Hakika uwezo wa kuunganisha maisha ni kipaji chenye kuleta uchovu mkubwa pamoja na maisha ya kifamilia yaliyo kamilika yenye mpangilio ni uhodari mkubwa; hasa ikiwa ni kwa Mwanamke wa nyumbani, na mama mlezi pia. Leo hii katika nchi zilizoendelea zaidi asilimia 85, wanawake wenye umri kati ya miaka 25 hadi 49 pamoja na maisha ya kando ya kifamilia, wameendeleza kipaji chao katika maisha yao ya kifamilia. Wanawake wenye kujishughulisha wengi hufanya jitihada za kulea watoto au familia zao au watu wanaowahusu kwa kufanya mlinganisho wa kazini na watoto wao, kwa kuomba msaada, lakini kwa hali kama hiyo pia wako baadhi ya wanawake ni wenye uwezo mkubwa zaidi kuliko wengine wa kupangilia mikakati na ratiba kwa ajili ya maisha yao.

WATAALAM KATIKA MAANDALIZI HAYA HUTOA NASAHA ZIFUATZO:

KUWA MWENYE MIPANGO:

Wakati/ muda waweza kuwa ni rafiki yako bora na adui yako mbaya. Katika sura ambayo wewe utakuwa ni Mama wa familia pia ni mwanamke mjasiriamali ni bora wakati/ muda ukautumia vyema. Kwa sababu wanawake wengi wajasiriamali siku ya ijumaa hupika chakula kingi cha wiki nzima na kukihifadhi ndani ya friza, ili asilazimike kupika kila siku/ kila saa, na usiku arejeapo nyumbani badala ya kuandaa chakula basi hukipasha na masaa mengine yaliyobaki ni kwa ajili ya maandalizi ya mavazi/ unifomu na ratiba za masomo za watoto wake. Na kwa upande mwingine ni kwamba hujaribu wakati wa asubuhi kuamka kabla ya kila mtu na wengine pia kazi zao za lazima mfano za kibenki nk hupenda kuzifanya asubuhi na mapema.

USIJIIBIE MWENYEWE:

Kuwa kwako Mama si kwa maana hii kwamba uwe mchukua posho kidogo, kwa kuwa huna mtoto, fanya kazi/ jishughulishe. Ni vyema pia mkafahamu ya kwamba akina mama wajasiriamali huweza kuwa watulivu na wenye msukumo zaidi ya wanawake wajasiriamali ambao hawajaolewa. Isipokuwa tu siku zote uwe ni mwenye kumridhisha kiongozi wa familia na umthibitishie kwamba ni mwenye kufika mapema kazini na mwenye kuwahi nyumba, ili ikiwa kwamba itatokea umechelewa kidogo kurudi nyumbani asije kukulaumu mtu. Pia ni muhimu kulizingatia hilo kwamba wewe unayo maisha ya kifamilia na haipaswi kwa kung’ang’ania wafanya kazi wenzio, ukatumia masaa ya ziada ya familia yako kazini kwako.

TAMBUA THAMANI YA MUDA WAKO:

Kwa kuwa wewe ni mwenye familia na pia ni mwenye kumridhisha kiongozi wa familia njia bora ya utatuzi wa hilo ni kwamba; kila kazi ifanye kwa wakati wake. Sahau kazi za ofisini uwapo nyumbani na usiwe mpiga simu sana nyumbani uwapo kazini. Kwa mfumo huu utaweza kutumia masaa yako vyema na kuathirika kwa mfumo huu, na ikiwa utalazimika siku moja kazi za ofisini kuzibeba nyumbani hakikisha asubuhi unashauriana na familia yako na usikilize nadharia zao. Kwa njia nyingine ni kwamba ikiwa watoto wamezoea kuja kazini kwako pasina dalili yoyote, ni bora ukaacha tabia hiyo mara moja. Isipokuwa katika hali ya dharura ijitokezapo, mmoja wa familia yako anaweza kurejea kazini kwako au kuwasiliana na wewe. Kinyume chake ikiwa Bosi au wafanya kazi wenzako wamezoea, uwapo nje ya ofisi kuwasiliana na wewe ni bora wakati ambao uwapo nyumbani kuzima simu yako au kuwajibu kwa njia ya sms.

JIPUMZISHE KWA MUDA WA KUTOSHA:

Haipaswi kutumia nguvu zote katika maisha ya kifamilia na kazi zako. Ijapokuwa vyote viwili vinakuhitajia, ama usisahau kuwa na wewe lazima ujitengee muda wako. Kwa mfano chagua mazoezi ya viungo uyapendayo na muda wake na siku yake maalum. Matembeezi, gymnastiki na hata kwenda kufanya manunuzi pamoja na ndugu au rafiki jambo hili litakusaidia kukuepusha na uchovu. Jiweke faragha kidogo ili siku zote uweze kuwa mwenye nguvu ya kutosha katika kuendesha kazi zako na mambo ya kifamilia.

OMBA MSAADA:

Kufanya kazi ni maamuzi ambayo wewe na mume wako mliyoyachukua. Hivyo basi muombe msaada katika kazi za nyumbani na kuangalia watoto. Kuosha vyombo, kuandaa chakula, kupeleka watoto shule na kuwarudisha nyumbani na kuwaogesha watoto ni nyadhifa ambazo mnaweza kugawana ili muweze kufanikiwa katika mikakati yenu ya kimaisha na kifamilia pia. Katika sura kama hii ikiwa ni mwenye uwezo mzuri unaweza kutafuta msaidizi wa watoto au mfanya kazi kwa ajili ya kusaidia kushughulikia mambo ya nyumbani. Kwa mfumo huu utapata muda mwingi wa kazi.

USIJIONE MZEMBE:

Hakuna mwanamke awezaye kufanya kazi za nyumbani na pia kazi za ofisini kwake bila kukosa mapungufu yoyote. Hivyo usijione mzembe. Ikiwa kwa leo utakuwa umechoka na usiweze kupika chakula, hakuna tatizo ikiwa kwa muda uliochoka utaagiza chakula hotelini japo mara moja si suala ambalo limekataliwa.

USISAHAU SHAKHSIYA/ UTU WAKO:

Kuwa kwako Mama, na kuwa kwako mke au Mwanamke mjasiriamali isiwe ni sababu ya wewe kuwa mtumwa. Ni lazima daima ulinde uanamke wako mwenyewe. Wanawake wengi wamezoea kujiachia na kujifanya wenye kujitolea ili kusifika kwa wengine, lakini kazi hii haina usahihi ndani yake. Linda uhalisia wa uanamke wako. Jaribu kujiweka smati na kuvaa mavazi mazuri japo mara moja. Wewe ni mwanamke na jitahidi kubaki kuwa mwanamke kwa fahari na si kujirahisisha kwa kila mtu.

Imetarjumiwa na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: