bayyinaat

Published time: 06 ,October ,2017      12:06:25
Vilevile kuacha kuunga undugu hadi watakapo tajirika, na kuacha Sala hadi watakapotoka ndani ya wakati wake, na kuacha kutoa nasaha na kutozuia dhulma, na kutotoa zaka hadi utakapo wakuta umauti na kufunga kauli.................
News ID: 103

Wengi wetu husoma katika dua Kumayli vipengele vifuatavyo, ya kwamba:

«اللهم اغفر لي الذنوب التي تهتك العصم ، اللهم اغفر لي الذنوب التي تنزل النقم ، اللهم اغفر لي الذنوب التي تغير النعم ، اللهم اغفر لي الذنوب التي تحبس الدعاء ، اللهم اغفر لي الذنوب التي تنزل البلاء ، اللهم اغفر لي كل ذنب أذنبته وكل خطيئة أخطأتها».

"Mola wangu nisamehe madhambi yanayovunja kinga baina yangu ili kukufikia wewe, Mola wangu nisamehe madhambi yanayoshusha/ yanayoleta nakama, Mola wangu nisamehe madhambi yanayobadili neema yako kwangu, Mola wangu nisamehe madhambi yafungayo Dua kupokelewa, Mola wangu nisamehe madhambi yanayoleta balaa, Mola wangu nisamehe kila dhambi niitendayo na kila kosa nikosalo”.

Je! Mmekwishajiuliza siku moja, ni dhambi gani hizi ambazo huzuia dua kupokelewa, na kushusha nakama na kubadili neema na kumnyima mwanadamu Raha yake ya dunia na kumzuia kufikia katika ukamilifu wa kufika juu n.k?

Ndugu msomaji wangu, hizi ni baadhi ya riwaya ambazo hufasiri na kupembua haya madhambi.

Al-kaafi cha sheikh al- kuleyni, juz 2, uk 447-448.

Kutoka kwa Abuu abdillah (a.s) amesema:

«الذنوب التي تغير النعم البغي والذنوب التي تورث الندم القتل ، والتي تنزل النقم الظلم ، والتي تهتك الستر شرب الخمر ، والتي تحبس الرزق الزنا ، والتي تعجل الفناء قطيعة الرحم ، و التي ترد الدعاء وتظلم الهواء عقوق الوالدين».

"Madhambi ambayo hubadili neema ni Uonevu, na madhambi ambayo huleta majuto ni; Kuua nafsi, na madhambi ambayo hushusha nakama ni; Dhulma, na ambayo huvunja sitara/ kinga ni kunywa pombe, na ambayo hufunga riziki ni; Zinaa, na ambayo huharakisha mauti ya ghafla ni; Kuvunja undugu, na ambayo huzuia dua kupokelewa na kuzuia mfua ni; kutowaheshimu wazazi wawili”.

Aidha:

Ma’anil akhbaar cha sheikh Saduq, uk 296-271.

Nilimsikia Zainul A’bidin Ali bin al- hussein (a.s) anasema:

"Madhambi ambayo hubadili neema ni: Kuonea watu, na kutojihusisha na ada ya kutenda heri, na kufanya mema, na kukana neema, na kuacha kushukuru neema. Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: "Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao”.

1. Madhambi ambayo huleta majuto ni: Kuua nafsi ambayo Mwenyezi Mungu ameharamisha kuuliwa. Amesema (s.w.t): "Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza”.

Na amesema tena (s.w.t) katika kisa cha Qaabil alipomuua nduguye Haabil na akashindwa kumzika na ikamsukuma nafsi yake kwa kumuua nduguye na akaamua, kwamba: "Basi akawa miongoni mwa wenye kujuta”.

Vilevile kuacha kuunga undugu hadi watakapo tajirika, na kuacha Sala hadi watakapotoka ndani ya wakati wake, na kuacha kutoa nasaha na kutozuia dhulma, na kutotoa zaka hadi utakapo wakuta umauti na kufunga kauli.

2. Na madhambi ambayo hushusha nakama ni: Mjuzi kuasi kwa uonevu na kujikweza kwa watu na kuwastahazai wengine na kuwakejeli.

3. Na madhambi ambayo huvunja kinga ni: Kunywa pombe, na kucheza kamari, na kufanya mizaha na upuuzi vitakavyopelekea watu kucheka, na kutaja aibu za watu, na kukaa na wala riba na wapokea rushwa.

4. Na madhambi yanayoshusha balaa ni: kuacha kusaidia wanaohitaji, na kuacha kumsaidia aliyedhulumiwa, na kupoteza suala la kuamrisha mema na kukemea mabaya.

5. Na madhambi ambayo huzidisha maadui ni: kujifaharisha kwa dhulma, na kutangaza uovu, na kuhalalisha mabaya, na kuasi waja wema, na kuwaunga mkono watu waovu.

6. Na madhambi ambayo huharakisha kifo cha ghafla ni: Kuvunja undugu, na kula yamini ya uongo, na kusema kauli za uongo, kufanya zinaa, na kuzuia njia ya Waislamu, na kudai uimamu bighairi ya haki.

7. Na madhambi yanayokata matumaini ni: Kukata tamaa katika rehema ya Mwenyezi Mungu, na kumtumainia asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kukadhibisha adhabu ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

8. Na madhambi yanayoondoa kinga ni: Kumhitajia asiyekuwa Mwenyezi Mungu, na kufanya uharibifu wa kutoa katika njia ya batili, na kufanya ubahili kwa familia, watoto na watu wa karibu na kuwa mbaya wa tabia, na uchache wa subira, na kutumia nguvu/ ukali, na kuwa uvivu, na kuwadharau wenye dini.

9. Na madhambi ambayo huzuia dua kujibiwa ni: kuwa na nia mbaya, na mwenye mwenendo mbaya kitandani, na kufanyia unafiki ndugu, na kutosadiki majibu ya dua, na kuchelewesha Sala na mambo ya faradhi hadi kupita wakati wake, na kuacha kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kutenda wema na kutoa sadaka, na kutumia maneno mabaya na machafu.

10. Na madhambi yanayozuia mvua ni: Ujeuri/ kiburi cha viongozi katika madaraka yao, na viapo vya uongo, na kuficha ukweli, na kuzuia zaka na mikopo na misaada, na ugumu wa moyo kwa mafukara na wenye shida, na kuwadhulumu mayatima na wajane, na kumfukuza muombaji na kumfungia mlango wakati wa usiku ajapo kukuomba.

. . . . . . . . .

Imeletwa kwenu na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.


LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: