bayyinaat

Published time: 08 ,October ,2017      10:19:08
Ibn Omar aliulizwa kunako Ali na Othman. Akasema: Ama kuhusu Ali musiniulize kuhusu yeye; Angalieni daraja yake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), kwani (Mtume) alifunga milango yetu Msikitini, na akaacha mlango (wa Ali)........
News ID: 108

1.               FAKHARI YA KUWA PAMOJA NA QUR’ANI

Hadithi ya Mtume (s.a.w.w) aliposema: "Ali yuko pamoja na Qur’ani”, ni moja katika wasifu  wa Imam Ali (a.s) ambao hakuna sahaba hata mmoja wa Mtume (s.a.w.w) hakuinukuu, ambayo wapokezi wengi ni katika shakhsiya kubwa za Nabii huyo.

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):

«عَلیٌّ مَعَ القُرآنِ و القرآنُ مَعَ عَلیّ، لَن یَفتَرقا حَتّی یَردا عَلَیّ الحَوض«.

"Ali yuko pamoja na Qur’ani na Qur’ani iko pamoja na Ali, katu havitoachana hadi vitakaponifikia kwenye Hodhi”.[1]

Yaani Ali amegandana na Qur’ani, na maneno yake na matendo yake ni mfumo wa Aya za Qur’ani.

2.               FAKHARI YA KUFUNGULIWA MLANGO WA NYUMBA YA ALI (A.S)

Hadithi ya kufungwa milango ni katika hadithi mutawatir kwa Shia na Sunni, na hakuna shaka ndani yake. Hadithi imenukuliwa kwa tamko tofautitofauti. Na hapa tunaleta mfano kutoka katika vyanzo vya Kisuni:

«إنَّ رَسولَ اللّهِ(ص) أمَرَ بِسَدِّ الأَبوابِ إلّا بابَ عَلِی».

"Kwa hakika Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) aliamuru kufungwa milango yote ila mlango wa Ali”.[2]

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):

 «سُدّوا أبوابَ المَسجِدِ غَیرَ بابِ عَلِی. فَیدخُلُ المَسجِدَ جُنُبا وهُوَ طَریقُهُ لَیسَ لَهُ طریقٌ غَیرُهُ».

"Fungeni milango yote ya msikiti isipokuwa mlango wa Ali. Anaingilia msikitini akiwa mwenye janaba na hiyo ndio njia yake hana njia nyingine”.[3]

Abdillah bin Arqam al-kinaniy:

«خَرَجنا إلَى المَدینَةِ زَمَنَ الجَمَلِ، فَلَقینا سَعدَ بنَ مالِک بِها، فَقالَ: أمَرَ رَسولُ اللّهِ(ص) بِسَدِّ الأَبوابِ الشّارِعَةِ فِی المَسجِدِ، وتَرَک بابَ عَلِی رضى الله عنه».

"Tulitoka nje ya mji wa Madina wakati wa vita vya Ngamia, tukakutana na Sa’ad bin Malik, akasema: Mtume (s.a.w.w) aliamuru kufungwa milango yote ya msikiti, akaacha mlango wa Ali (Radhiallahu anh’u”.[4]

Jaabir bin Abdillah:

«سَمِعتُ رَسولَ اللّهِ(ص) یقولُ: سُدُّوا الأَبوابَ کلَّها إلّا بابَ عَلِی وأومَأَ بِیدِهِ إلى بابِ عَلِی».

"Nimemsikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akisema: "Fungeni milango yote ila mlango wa Ali na akaashiria kwenye mlango wa Imam Ali”.[5]

سُئِلَ ابنُ عُمَرَ عَن عَلِی وعُثمانَ. فَقالَ: أمّا عَلِی فَلا تَسأَلوا عَنهُ؛ انظُروا إلى مَنزِلَتِهِ مِن رَسولِ اللّهِ، فَإِنَّهُ سَدَّ أبوابَنا فِی المَسجِدِ، وأقَرَّ بابَهُ.

Ibn Omar aliulizwa kunako Ali na Othman. Akasema: Ama kuhusu Ali musiniulize kuhusu yeye; Angalieni daraja yake kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w), kwani (Mtume) alifunga milango yetu Msikitini, na akaacha mlango (wa Ali)”.[6]

إنَّ النَّبِی(ص) قالَ: سُدّوا عَنّی کلَّ خَوخَةٍ فِی المَسجِدِ إلّا خَوخَةَ عَلِی.

Kwa hakika Mtume (s.a.w.w) amesema: Fungeni mapitio yote ya Msikitini, ila maingilio ya Ali”.[7]

Zaid bin Arqam;

«کانَ لِنَفَرٍ مِن أصحابِ رَسولِ اللّهِ(ص) أبوابٌ شارِعَةٌ فِی المَسجِدِ، قالَ: فَقالَ یوما: سُدّوا هذِهِ الأَبوابَ إلّا بابَ عَلِی».

"Kulikuwa na maingilio ya baadhi ya wafuasi wa Mtume (s.a.w.w) waliyopitia msikitini, akasema; siku moja akasema (s.a.w.w): "Fungeni milango hii ila mlango wa Ali”.

قالَ: فَتَکلَّمَ فی ذلِک النّاسُ، قالَ: فَقامَ رَسولُ اللّهِ(ص)، فَحَمِدَ اللّهَ تَعالى وأثنى عَلَیهِ، ثُمَّ قالَ: أمّا بَعدُ، فَإِنّی أمَرتُ بِسَدِّ هذِهِ الأَبوابِ إلّا بابَ عَلِی، وقالَ فیهِ قائِلُکم، وإنّی وَاللّهِ ما سَدَدتُ شَیئا ولا فَتَحتُهُ! ولکنّی امِرتُ بِشَی ءٍ فَاتَّبَعتُهُ.

Amesema (mpokezi wa riwaya): Watu wakanong’onezana kuhusu hilo, akasema; Akasimama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, akamhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, kisha akasema: ama baada ya hayo, Hakika Mimi nimeamrisha kufunga milango hii ila mlango wa Ali, akalizungumzia mmoja wenu, Na mimi ninaapa kwa Mwenyezi Mungu, sikufunga chochote wala kufungua chochote! Lakini Mimi nimeamrishwa kitu nikatekeleza”.[8]

Fadhila ya Ali katika agizo hili la Mtume (s.a.w.w) ni pale aliposema katika hadhira ya Watu baada ya kumsifu mwenyezi Mungu na kumhimidi;

Mimi nimetekeleza amri ya Mola wangu ya kufunga milango yote ila mlango wa Ali, lakini nyinyi mkanisema, kwa hakika Mimi sikufunga wala kufungua chochote, isipokuwa nimetii amri niliyopewa”.[9]

Kutoka kwa ibn Abbas amesema:

عن ابن عباس قال: لمّا سدّ رسول الله صلی الله علیه و آله و سلم الابواب الشّارعة الی المسجد الاّ باب علیٍّ علیه السلام ضجّ اصحابه من ذلک فقالوا یا رسول الله لم سددت ابوابنا و ترکت باب هذا الغلام!

"Pindi Mtukufu Mtume (s.a.w.w) alipofunga milango ya wapitaji msikitini ila mlango wa Ali (a.s), Masahaba wake walilalamikia hilo wakamuliza; Ewe Mjumbe wa Mungu: Kwanini umefunga milango yetu na umeacha mlango wa Kijana huyu!”.

Akasema (s.a.w.w):

«انّ الله تبارک و تعالی امرنی بسدّ ابوابکم و ترک باب علیٍّ ...».

"Kwa hakika Mwenyezi Mungu mtukufu ameniamuru nifunge milango yenu na kuacha mlango wa Ali…”.

 

Sheikh : Juma. R. Kazingati.



[1] Mustadrak al-haakim, juz 3, uk 134. Sawai’q ala-muhriqah, cha Ibn Hajar uk 122. Yanabi’u al- mawadda, mlango wa 20, uk 90.

[2] Sunan at-tirmidhiy, juz 5, uk 641, hadithi ya 3732. Sunan an-nasaai, uk 105, hadithi ya 43. Hilyat al-auliyaa, juz 4, uk 153. Taarekh madinat damashq, juz 42, uk 138. Al-manaaqib, cha Ibn al-ghazaaliy, uk 260, hadithi ya 308.

[3] Musnad Ibn Hambal, juz 1, uk 709, hadithi ya 3062. Fadhaail al-sahaabah, cha Ibn Hambal, juz 2, uk 684, hadithi ya 1168. Al-mustadrak A’laa as-sahihayn, juz 3, uk 144, hadithi ya 4652. Al-isaabah, juz 4, uk 467, namba 5704. Al-bidaaya wa al-nihaaya, juz 7, uk 339. Al-manaaqib, cha Khorazmiy, uk 127, hadithi ya 140.

[4] Musnad ibn Hambal, juz 1, uk 371, hadithi nambari, 1511.

[5] Taarekh al-baghdadiy, juz 7, uk 205, hadithi nambari, 3669. Hilyat al-auliyaa, juz 4, uk 153.

[6] Al’mu’jam al-awsat, juz 2, uk 38, hadithi nambari, 1166.

[7] Musnad al-bazzaar, juz 3, uk 368, hadithi nambari, 1169.

[8] Musnad Ibn Hambal, juz 7, 79, hadithi nambari, 19307. Fadhail al-sahaabah; cha Ibn Hambal, juz 2, uk 581, hadithi nambari, 985. Al-mustadrak a’laa as-sahihayn, juz 3, uk 135, hadithi nambari, 4631. Nasaai, uk 98, hadithi nambari, 38. Taarekh madinat damashaq, juz 42, uk 138, hadithi nambari, 8522-8523. As-sawaa’iq al-muhriqah, uk 124, hadithi nambari, 24. Al-Manaaqib, cha Khorazmiy, uk 327, hadithi nambari, 338.

[9] Ila al-sharaa’I, mlango wa 154, uk 201. Bihar al-anwaar, juz 39, uk 19-35. Mustadrak al-haakim, juz 3, uk 125.

LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: