bayyinaat

Published time: 08 ,October ,2017      10:26:03
Mtukufu Mtume baada ya kutimiza Hijja ya mwisho na kutekeleza ibada za Hijja, na kufuta athari za kijahili na kuweka jiwe jeusi mahala pake na kukaa Makka kwa siku moja, Malaika Jibril alimjia Mtume na Aya hizi za....
News ID: 109

Ghadir khum ni mahala pa mkataba na makubaliano ya umma wa Kiislamu pamoja na Uimamu na Wilaya ya Imam Ali (a.s). kwa dalili hiyo tukio la Ghadir limekuwa ni lenye kutazamiwa sana kwa Mashia na wanazuoni wa kidini, kwa sababu Shia anaamini hapo ndipo ambapo ukhalifa na Uimamu baada ya Mtume (s.a.w.w) umeainisha na kutangazwa na Mtume Muhammad (s.a.w.w), tofauti na Ahlusunna ambao katika kumuainisha Imam wana hitilafu, kwa sababu ya mapungufu ya Makhalifa watatu (Abubakr, Omar na Othman) kukalia ukhalifa bila haki. Ama swali muhimu ni kwamba, ni yupi aliyekuwa sambamba na chimbuko la Qur’ani na yupi aliyekuwa kinyume na chimbuko hilo:

AYA ZILIZOBAINISHA TUKIO LA GHADIR.

Kutokana na umuhimu wa tukio lililojiri katika viwanja vya Ghadir na kugeuka kuwa tukio lenye umuhimu katika mambo ya ulimwengu wa Kiislamu, kwani awali ilikuwa lazima kuzingatia ufikishaji wa amri ya Mwenyezi Mungu na ushuhuda wa Mtume (s.a.w.w), kwa sababu msingi wa itikadi na historia umeelemea katika amri za Mwenyezi Mungu, kwa kuthibitisha nusura hii. Kwa kuangalia mifano ya Aya na riwaya tunaamini kwamba Shia wanaitikadia kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alifikisha kwa ubainifu mzuri juu ya maswala ya Uimamu na uongozi wa jamii ya Kiislam. Na sisi hapa tubainishe Aya za Qur’ani kwa sura ya sababu ya kushuka kwake na ushuhuda na muhimu zaidi ni pokezi za Shia kuhusu itikadi hii.

AYA ZA SURAT AL-A’NKABUT.

Mtukufu Mtume baada ya kutimiza Hijja ya mwisho na kutekeleza ibada za Hijja, na kufuta athari za kijahili na kuweka jiwe jeusi mahala pake na kukaa Makka kwa siku moja, Malaika Jibril alimjia Mtume na Aya hizi za Surat al-a’nkabut:

«بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ. أَحَسِبَ النَّاسُ أَنْ يتْرَكُوا أَنْ يقُولُوا آمَنَّا وَهُمْ لَا يفْتَنُونَ. وَلَقَدْ فَتَنَّا الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ فَلَيعْلَمَنَّ اللَّهُ الَّذِينَ صَدَقُوا وَلَيعْلَمَنَّ الْكَاذِبِينَ. أَمْ حَسِبَ الَّذِينَ يعْمَلُونَ السَّيئَاتِ أَنْ يسْبِقُونَا سَاءَ مَا يحْكُمُونَ».

"KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. Je! Wanadhani watu wataachwa kwa kuwa wanasema: Tumeamini. Nao wasijaribiwe?. Hakika tuliwajaribu walio kuwa kabla yao, na kwa yakini Mwenyezi Mungu atawatambulisha walio wa kweli na atawatambulisha walio waongo. Au wanadhani wanao tenda maovu kwamba watatushinda? Hukumu mbaya hiyo wanayo hukumu”.[1]

Kisha ikaja amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu kuwa; lazima amtambulishe Ali bin Abitalib (a.s) kuwa ndiye khalifa wake na kuwajuza watu kuingia katika fitina kwa sababu ya jambo hilo.

AYA ZA MWISHO WA SURAT AL-HIJR.

Kabla ya tukio la Ghadir, amri ya siri kutoka kwa Mwenyezi Mungu ya kuainisha ukhalifa wa Ali (a.s) kwa Mtume (s.a.w.w). bi Aisha na Bi Hafsa walifichua habari hii kwa Baba zao (Hali ambayo kushuka amri hii ilikuwa ni siri kwa Mtume na kuwa kabla ya amri ya kuibainisha asimueleze yeyote), nao kwa msaada wa wanafiki wakapanga njama za kumuua Mtume (s.a.w.w). wakati huo Malaika Jibril alimjia Mtume na kumueleza hila za wanafiki:

«فَوَرَبِّكَ لَنَسْأَلَنَّهُمْ أَجْمَعِينَ. عَمَّا كَانُوا يعْمَلُونَ. فَاصْدَعْ بِمَا تُؤْمَرُ وَأَعْرِضْ عَنِ الْمُشْرِكِينَ. إِنَّا كَفَينَاكَ الْمُسْتَهْزِئِينَ».

"Basi Naapa kwa Mola wako Mlezi! Tutawahoji wote. Kwa waliyo kuwa wakiyatenda. Basi wewe yatangaze uliyo amrishwa, na jitenge na washirikina. Hakika Sisi tunatosha kukukinga na wanao kejeli”.[2]

AYA YA IBLAAGH (UFIKISHAJI).

Imam Baqir (a.s) katika kubainisha Aya hii amesema: Mwenyezi Mungu amemuamuru Mtume wake (s.a.w.w) kuwahabarisha watu wilaya ya Ali (a.s) na upande mwingine akashusha Aya ya kumtii walii amr, watu wakatahamaki kuwa je! Amri ni ya Mwenyezi Mungu? Au ni ubainifu wa Aya ya kumtii walii amr, na Walii mkusudiwa si mwingine ila ni kumtangaza Ali bin Abitalib (a.s). wakati huu alikuwa mwenye hofu kufikisha ujumbe huo kutokana na hila za wanafiki waliokusudia kufanya hilo na ili yeye akamilishe kazi zilizosalia, Mwenyezi Mungu akashusha Aya hii:

«يا أَيهَا الرَّسُولُ بَلِّغْ مَا أُنْزِلَ إِلَيكَ مِنْ رَبِّكَ وَإِنْ لَمْ تَفْعَلْ فَمَا بَلَّغْتَ رِسَالَتَهُ وَاللَّهُ يعْصِمُكَ مِنَ النَّاسِ إِنَّ اللَّهَ لَا يهْدِي الْقَوْمَ الْكَافِرِينَ».

"ewe Mtume! Fikisha uliyo teremshiwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Mwenyezi Mungu atakulinda na watu. Hakika Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri”.[3]

AYA YA 1-2 NA 51-52 ZA SURAT AL-QALAM.

Imam Sadiq (a.s) alipokuwa katika viwanja vya Ghadir khum, alimwambia Hussein bin Jamal kuwa: Wakati Mtume (s.a.w.w) mahala hapa alipokuwa ameshika mkono wa Ali (a.s) na kusema: "Yule ambaye mimi ni kiongozi wake, basi Ali pia ni kiongozi wake”. Watu wanne (Mashuhuri kwa unafiki) waliokuwa wamesimama kando ya hema, walimuangalia Mtume (Wakati akinyoosha mkono wa Ali (a.s), mmoja wao akasema: Muangalieni macho anavyoyatoa, kama jahili. Mwenyezi Mungu akamshushia Aya hizi:

«وَإِنْ يكَادُ الَّذِينَ كَفَرُوا لَيزْلِقُونَكَ بِأَبْصَارِهِمْ لَمَّا سَمِعُوا الذِّكْرَ وَيقُولُونَ إِنَّهُ لَمَجْنُونٌ. وَمَا هُوَ إِلَّا ذِكْرٌ لِلْعَالَمِينَ».

"Na walio kufuru hukaribia kukutelezesha kwa macho yao, wanapo sikia mawaidha, na wanasema: Hakika yeye ni mwendawazimu. Na hayakuwa haya, ila ni ukumbusho kwa walimwengu wote”.[4]

Mtume (s.a.w.w) akasoma na Aya hizi:

«بِسْمِ اللَّهِ الرَّحْمَنِ الرَّحِيمِ ن وَالْقَلَمِ وَمَا يسْطُرُونَ. مَا أَنْتَ بِنِعْمَةِ رَبِّكَ بِمَجْنُونٍ».

"WA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU. Nuun. Naapa kwa kalamu na yale wayaandikayo. Kwa neema ya Mola wako Mlezi wewe si mwendawazimu”.[5]

AYA YA KUKAMILIKA DINI

Baada ya Mtume (s.a.w.w) katika hadhira ya watu kutangaza wilaya ya Ali (a.s), Aya hii ikashuka:

«الْيوْمَ يئِسَ الَّذِينَ كَفَرُوا مِنْ دِينِكُمْ فَلَا تَخْشَوْهُمْ وَاخْشَوْنِ الْيوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا فَمَنِ اضْطُرَّ فِي مَخْمَصَةٍ غَيرَ مُتَجَانِفٍ لِإِثْمٍ فَإِنَّ اللَّهَ غَفُورٌ رَحِيمٌ».

"Leo walio kufuru wamekata tamaa na Dini yenu; basi msiwaogope, bali niogopeni Mimi. Leo nimekukamilishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. Na mwenye kushurutishwa na njaa, bila ya kupendelea dhambi, basi hakika Mwenyezi Mungu ni mwingi wa msamaha na Mwenye kurehemu”.[6]

Sheikh : Juma. R. Kazingati.



[1] Suratul A’nkabut/ 1-3.

[2] Suratul Hijr/ 92-95.

[3] Suratul Maida/ 67.

[4] Suratul Qalam/ 51.

[5] Suratul Qalam/ 1-2.

[6] Suratul Maida/ 3.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: