bayyinaat

Published time: 08 ,October ,2017      10:36:10
DALILI ZA UKAMILIFU WA AKILI 1) Kutoudhi watu, na wao kutarajia yake mema. 2) Kutumia mali zake katika njia ya Mola wake. 3) Kujiepusha kuongea sana......
News ID: 112

DALILI ZA UKAMILIFU WA AKILI

1) Kutoudhi watu, na wao kutarajia yake mema.

2) Kutumia mali zake katika njia ya Mola wake.

3) Kujiepusha kuongea sana.

4) Kukinaika na Mali ya Dunia.

5) Kutotosheka kumaliza umri wake kutafuta elimu.

6) Kutaka radhi za Mola zaidi kuliko kuridhisha walimwengu.

7) Kuzingatia umuhimu wa kutendea Watu hisani, na kutojali umuhimu wa kutendea hisani.

8) Kutazama watu kwa wema kuliko mwenyewe.

MAMBO YANAYOZIDISHA KUMBUKUMBU

1) Kula asali kwa wingi.

2) Kupiga mswaki.

3) Kusoma sana Qur’ani.

4) Kufanya Hijamu.

5) Kukata kucha siku ya Jumatatu.

6) Kula Asali iliyochanganywa na Zaafarani ya unga.

MAMBO YANAYOPUNGUZA KUMBUKUMBU

1) Kula tunda chachu (Kali).

2) Kula chakula alichoacha Panya.

3) Kukojoa ndani maji tulivu.

4) Kusoma mawe ya juu ya makaburi.

5) Kupita katikati ya wanawake.

MAMBO YANAYOSABABISHA UGUMU WA MOYO

1) kuombaomba sana.

2) Kuwa mwenye matarajio marefu.

3) Kuacha kufanya dhikiri.

4) Ulafi.

5) Ung’ang’anizi wa Kutenda madhambi.

6) Kufanya sana tendo la ndoa na wanawake wengi.

7) Kuongeaongea sana na wanawake.

8) Kukinzana na wanaokula kidogo.

9) Kukaa sana na Matajiri walioghafilika na Mola wao.

10) Kunywa Damu.

11) Kula Nyama siku arobaini mfululizo.

12) Kucheka sana.

13) Kulala punde tu baada ya kula.

14) Kusikiliza Upuuzi/ miziki.

15) Kuwinda sana wanyama.

16) Kutembea zaidi katika Kasri za Watawala (Viongozi).

17) Kumwagia udongo kwenye kaburi la ndugu yako.

MAMBO YANAYOLAINISHA MOYO

1) Kula Adesi (Dengu).

2) Kula komamanga.

3) Kushika Kichwa cha Yatima.

MAMBO YANAYOLETA NURU YA MOYO NA KUONDOA WASIWASI WAKE

1) Kula siki.

2) Kula komamanga.

3) Kuosha kichwa kwa Maji ya Sidr (Mkunazi).

4) Kupaka Hina.

5) Kupiga mswaki.

6) Kutamka kauli hii (لا إله إلّا الله).

7) Kusoma Surat An- Naas (قل أعوذ بربّ النّاس).

8) Kusoma Tasbih kwa wingi.

9) Kukariri kusoma dhikri hii;

توکلت علی الحي الذي لا يموت والحمد لله الذي لم يتّخذ صاحبة ولا ولداً ولم يکن له شريک في الملک ولم يکن له وليّ من الذّلّ وکبّره تکبيراً.

MAMBO YANAYOONDOA HUZUNI NA GHADHABU

1) Kutia Udhu na kuoga kila wakati.

2) Kusujudu kwa muda mrefu.

3) Kukaa kama umesimama, na kusimama kama umekaa.

4) Kutamka kauli hii; (لا حول ولا قوّة إلّا بالله العليّ العظيم).

5) Kula Zaituni.

MAMBO YANAYOZIDISHA UMRI WA MAISHA YA MJA WA ALLAH

1) Kuwatendea Hisani wazazi wawili.

2) Kujiepusha kuudhi Watu.

3) Kuheshimu wazee na wakubwa.

4) Kuunga Undugu.

5) Kujiepusha kukata Miti ya Bustani, isipokuwa panapobidi.

6) Kutia Udhu.

7) Kulinda Afya.

8) Kusema vyema na Watu.

9) Kutendea wema Watu.

10) Kuamiliana vizuri na Majirani.

11) Kurefusha Rukuu na Sijida (katika Sala).

12) Kuendelea kukaa katika meza ya Chakula pindi unapolisha watu.

13) Kutendea Hisani Familia.

14) Kuwa mwenye Udhu wakati wote.

MAMBO YANAYOPUNGUZA UMRI

1) Kukiuka amri za Mwenyezi Mungu.

2) Kukithirisha kutenda dhambi ya zinaa.

3) Kudhulumu Waja wa Mwenyezi Mungu.

4) Kuvunja Undugu.

5) Kiapo cha Uongo.

6) Kutotilia Umuhimu Sala.

MAMBO YANAYOZIDISHA RIZIKI YA MJA

1) Tabia njema.

2) Tabia nzuri kwa Majirani.

3) Kuwafanyia Hisani wazazi wawili.

4) Kuunga Undugu.

5) Kutoa Sadaka.

6) Nia njema.

7) Kuosha mikono kabla ya chakula.

8) Kuosha Vyombo baada ya chakula.

9) Kufagia Nyumba.

10) Kuwasha Taa (za ndani) kabla halijazama Jua.

11) Kula Mdalasini katika meza ya chakula.

12) Kuchana Nywele.

13) Kusafisha mazingira ya Mlango wa Nyumba.

14) Kuwapa kipaumbele wasiojiweza.

15) Kuwa mchumi.

16) Kujiepusha na Matamanio.

17) Wema na Uaminifu.

18) Kukata kucha na Nywele katika siku ya Ijumaa.

19) Kuomba msamaha kwa Allah.

20) Kutamka; (حول ولا قوّة إلّا بالله).

21) Kutamka mara thelathini; (سبحان الله وبحمده سبحان الله العطيم وبحمده).

22) Kuombea Du’a Waumini.

23) Kusalimia na kusoma (قل هو الله أحد) baada ya kuingia Nyumbani.

24) Kusoma Ayatul Kursiy (آية الکرسي).

25) Kutamka kila siku kauli hiyo mara mia moja; (لا اله الّا الله الملک الحقّ المبين).

26) Kusoma Surat Yaasin (يس).

27) Kusoma Surat (والصّافّات) kila siku ya Ijumaa.

28) Kusoma Suratul Waqi’ah kila usiku (الواقعة).

29) Kusali Sala za Usiku.

30) Kumtegemea Allah.

Sheikh : Juma. R. Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: