bayyinaat

Published time: 08 ,October ,2017      10:40:25
1) Kumpenda Imamu Ali (a.s). 2) Kuwatendea hisani wazazi wawili. 3) Kuunga undugu. 4) Kuwapa mavazi waumini wasiojiweza. 5) Kuwapa maziwa waumini wasiojiweza..........
News ID: 114

MAMBO YANAYOPELEKEA URAHISI KATIKA KIFO

1) Kumpenda Imamu Ali (a.s).

2) Kuwatendea hisani wazazi wawili.

3) Kuunga undugu.

4) Kuwapa mavazi waumini wasiojiweza.

5) Kuwapa maziwa waumini wasiojiweza.

6) Kufunga (Saumu).

7) Kusoma Surat Yaasin (يس) mara kwa mara.

MAMBO YATAKAYOIPA UZITO MIZANI SIKU YA KIAMA

1) Ukimya.

2) Tabia njema.

3) Kuepuka kile kisichofaa.

4) Kutamka (لا اله الّا الله والحمد لله).

5) Kutamka kauli hii baada ya kusimama kwenye kikao;

(سبحان ربّک ربّ العزّة عمّا يصفون وسلام علی المرسلين والحمد لله ربّ العالمين).

6) Kumsabihi Allah kwa wingi.

7) Kuwa msafi wa Roho (Ndani) Zaidi kuliko wa Dhahiri.

MAMBO YATAKAYOPELEKEA KUINGIA PEPONI

1) Kumcha Mwenyezi Mungu katika siri na dhahiri.

2) Kuwatendea Hisani Wazazi wawili.

3) Kufunga Sunna japo siku moja.

4) Kufupisha matarajio.

5) Kutosahau Kifo.

6) Kuunga Undugu.

7) Tabia njema.

8) Kuwatendea watu Usawa.

9) Kuhurumia Mayatima.

10) Kusaidia wanyonge na wasiojiweza.

11) Kumnyenyekea Allah.

12) Kutatua matatizo ya Waislamu.

13) Kuwa mwenye tabia njema kwa watu.

14) Kuipa shida ya Muumini kipaumbele.

15) Kusaidia Yatima hadi atakapoacha kuhitajia watu.

16) Kukaa kwa Mwanazuoni japo saa moja.

17) Kutembelea makaburi ya Mawalii wa Mwenyezi Mungu.

18) Kusalia maiti ya Muumini.

19) Kustahi kukiuka amri ya Mwenyezi Mungu katika siri.

20) Kuridhika na kile alichokuneemesha Mwenyezi Mungu.

SIFA ZA SADAKA

1) Huzidisha Mali.

2) Huleta shifaa.

3) Huzuia Balaa na matatizo.

4) Mtoaji wake huvuka Sirat mithili ya Umeme.

5) Mtoa Sadaka ataingia peponi bila kuhesabiwa.

MAMBO YATAKAYOPELEKEA WEPESI KATIKA HISABU SIKU YA KIAMA

6) Kujihesabu kabla hujahesabiwa.

7) Kujiepusha na Matamanio ya nafsi.

8) Kuwatendea wema wazazi wawili.

9) Kuunga Undugu.

10) Tabia Njema.

11) Kula kidogo.

12) Kutoa sadaka kwa siri wakati wa usiku.

13) Kuleta faraja ndani ya nafsi ya Muumini

MAMBO YATAKAYOPEKEA KUTOINGIA PEPONI

1) Kutotoa mikopo kwa Waumini wenye shida.

2) Kuwapa adha majirani.

3) Kuwepo kizuizi baina yako na Muumini.

4) Kutoheshimu Wazazi wawili.

5) Duyuthi (Dhuyuthi: Ni yule ambaye mkewe anatenda zinaa na ilihali atambua hilo lakini asiwe na wivu).

6) Kunywa pombe.

7) Kufanya Uchawi.

8) Kuvunga Undugu.

9) Kula mali ya Haramu.

10) Kutowalipa Wafanya kazi Ujira wao ipasavyo.

11) Kutoa masimango baada ya kutoa sadaka.

12) Ubahili.

13) Kupeleleza/ kufanya ujasusi.

14) Kuongea maovu na matusi.

MAMBO YATAKAYOPELEKEA ADHABU ZA KABURINI

1) Kupoteza na kupuuzia Neema za Mwenyezi Mungu.

2) Kupuuzia Sala.

3) Kupeleleza/ kufanya ujasusi.

4) Kutodhibiti kutapakaa mikojo.

5) Kujitenga mbali na Familia pamoja na Ndugu.

6) Kumteta Muumini.

7) Kusema Uongo.

8) Tabia mbaya kwa Familia na Ndugu.

Sheikh : Juma. R. Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: