Baada ya kufahamu kwamba dini ya Kiislamu siku zote imekuwa ni
yenye kuweka mifumo sahihi kwa wana familia ili kuweza kufikia malengo makubwa,
sasa ni wakati wa kuweza kufahamu kwamba kuna watu ambao kwa kutumia akili zao
za kawaida wamejaribu kuja na mifumo yao ya kifamilia wakiwa na imani kwamba ni
mifumo sahihi hali ya kuwa mambo ni kinyume kabisa, bali tunakuta ni mifumo
ambayo inaharibu na kubomoa kabisa familia za wanadamu.
Ifuatayo ni baadhi ya
mifumo hiyo pamoja na athari zake katika familia n akwa jamii kwa ujumla.
1.
Mfumo wa Marcus
Huu ni mfumo ambao tunaweza kuuita janga katika familia
na jamii nzima za wanadamu, kwa maana msingi mkubwa wa mfumo huu ni kuhakikisha
kwamba mtoto tangia akiwa mdogo basi analelewa katika maisha ya kwamba
anatakiwa ajitambue kwamba yeye ni mkazi tu na wala hana mahusiano na familia
yeyote ile.
Hivyo mtoto baada ya
kuzaliwa hawi ni mwanafamilia wa familia fulani, bali huwa ni mkazi tu wa jamii
ile.
Maulama wa elimu za jamii
wanaukosoa mfumo huu kwa kusema ".....Ikiwa mambo yatafikia katika hali hii,
basi jamii nzima itaanguka, na pia hakutakuwa na familia thabiti, kwa maana
moja ya nguzo muhimu katika familia inakuwa imeanguka....”.
Rejea kitabu Al Usratul wal Mujtamaa uk 14
Ndio, hakuna familia wala
jamii ambayo itaweza kusimama bila ya nguzo, kwa maana mtoto kama mtoto ni
nguzo muhimu katika kujenga familia na jamii kwa ujumla kama tulivyotanguliza,
sasa endapo mtoto atakuwa ni fikra ya kwamba yeye si wa familia fulani bila
shaka atakuwa na fikra ya kwamba yeye si wa jamii fulani pia, hivyo mwisho wa
siku hakutakuwa na familia wala jamii iliyo thabiti.
2.
Mfumo wa Masson "Masonism”
Huu pia ni mfumo ambao unalenga moja kwa moja katika
kumtenganisha mwanadamu na familia yake. Haya si maneno yangu mimi , bali
tunayakuta endapo tutarejea katika hotuba ya mwenyewe Mason ambayo aliitoa
mnamo mwaka 1921 alipokuwa akiwapa watu njia za kuweza kutenganisha baina ya
familia na nguzo zake.
Anasema ".......Ili muwe
na uwezo wa kutenganisha baina ya familia ni lazia kwanza muweze kuondoa
maadili na misingi yake kwa familia hizo kwa kutumia mambo ambayo yamekatazwa
kwao, na hii ni kutokana na kwamba nafsi za wanadamu siku zote huwa zinapenda
kuelemea yale ambayo zimekatazwa kwayo, kama
vile kukata mahusiano n akukaribia kila lililo chafu. Kama ambavyo pia nafsi
hizo hupendelea zaidi mambo ya kila mmoja kuwa kivyake kuliko mambo ya
kushikamana katika familia au jamii moja, au kukaa na kupiga porojo katika
vijiwe kuliko kusimamia mambo yanayohusu familia zao. Sasa watu kama hawa
unaweza kuwahadaa kwa kuwaahidi nafasi na nyadhifa kubwa na hata vipato vikubwa
kutoka kwetu.........”
Rejea
Utangulizi wa kitabu cha Istratijiyatul Usra uk 11
Nadhani umejionea mwenyewe
jinsi gani watu walivyo na nia thabiti katika kuharibu familia n ajamii kwa
ujumla, tena hata kwa kutumia gharama kubwa kabisa katika hilo. Cha msingi ni
kwamba inatakiwa tuelewe ya kuwa kila mfumo ambao unakuwa unapingana na mfumo
sahihi wa familia na jamii, au kila mfumo ambao utakuwa hauelewi kwa usahihi
misingi na malengo ya familia basi inatakiwa tuutupilie mbali, kwa maana bila
shaka utakuwa ni mfumo wenye kutuangushia katika majanga na machafuko ya
kifamilia na kijamii kwa ujumla.