Ni jukumu la kila mpenda
maendeleo ya familia n ajamii yake kwa ujumla kuweza kutoa juhudi zake katika
kuhakikisha kwamba familia yake na jamii yake kwa ujumla inatilia umuhimu swala
zima la hisia za wahusika wake. Kwanini nasema hivi?, na kwa sababu hisia za
mwanadamu hasa katika swala la kupenda kuwa na mahusiano ni kali sana kuliko
tunavyofikiria, n anaweza kusema kwamba ni swala ambalo linawasukuma wengi sana
kufanya mambo yaliyo mengi. Mfano leo hii utakuta kuna asilimia kubwa ya watu
ambao wanafanya juu chini waweze kupata kipato, nafasi kubwa, nyadhifa n a hata
majina, lakini lengo kubwa ni ili tu waweze kufikia katika kutimiza hisia zao
kwa wale ambao wanaamini ndio sahihi kwao. Pia hata ukija kwa ambao tayari wapo
katika familia zao bado utakuta kwamba jambo ambalo linapelekea kuendelea
kubakia kwa upendo, amani, masikilizano ndani ya familia hizo ni swala zaima la
hisia, n a laiti kama kusingalikuwa na hisia hizo basi kusingalikuwa na upendo
ambao ulikuwepo wakati hisia hizo zilikuwepo baina yao. Najua unaweza ukawa
bado hujakubaliana nami katika hili, ila nitakupa mfano wa mwisho wa kuweza
kukufanya ukubaliane nami, angalia leo hii watu ambao tunawaita ni "waliofiwa
na hisia zao”, yaani wale watu ambao hawana hisia kabisa za kuwa karibu na
wengine, jinsi gani ambavyo wanateseka na kutaabika katika maisha yao, wenyewe
ukiwauliza kunako jambo hili watakujibu kwamba wapo salama na wanafurahia
maisha yao, lakini si kweli, ni kwamba wanakuwa na matatizo makubwa sana
kijamii. Na kama isingalikuwa ni tatizo basi kusingalikuwa na mahospitali
makubwa ulimwenguni ambayo yanahusika na kutibu tatizo hili. Ni kwamba wamekaa
na kuchunguza watu wa namna hii na kukuta kwamba kuna baadhi ya matatizo
hayatoki isipokuwa kwa watu hawa tu.
Hivyo basi ni jukumu la
kila mwana familia kuweza kuhakikisha kwamba nguzo za familia yake zinajijenga
katika mahusiano sahihi na ambayo ni yenye kuruhusiwa na misingi sahihi ya
familia na dini kwa ujumla, kwa maana huwezi kuisemea nafsi ya wanafamilia wako
kwa kusema kwamba mtoto wangu au mwenza
wangu hana fikra wala mawazo ya kufuata
hisia zake, kumbuka kwamba hisia za wanadamu katika swala la mahusiano ni kali
mno. Na endapo mwanafamilia hatokuwa makini katika jambo hili basi atajikuta
mwisho wa siku anajuta kwa kukuta kwamba moja ya nguzo za familia yake imefuata
ukali wa hisia zake na kuangukia katika mahusiano ambayo si sahihi kwake.
Mahusiano ambayo si sahihi
Kama tulivyotanguliza ni
kwamba kila mwanafamilia anatakiwa kuwa makini katika kuhakikisha kwamba nguzo
za familia yake zinashikamana na mahusiano ambayo ni sahihi. Hapa tulikuwa
tunajaribu kulenga kwamba kuna mahusiano ambayo si sahihi katika jamii, na
mwisho wa mahusiano haya ambayo si sahihi ni kuharibu na kuvunja misingi ya
familia n a jamii kwa ujumla kutokana na athari zake mbaya.
Tutajaribu kuelezea baadhi
ya mahusiano hayo ambayo si sahihi pamoja na athari zake zinazoambatana nayo.
kuwa nasi katika wakati ujao......