bayyinaat

Published time: 20 ,October ,2017      09:02:20
Kwanza nishukuru kuona kwamba wenyewe wanakubali kwamba kitendo hiki ni kuchepuka na kutoka katika njia kuu, kisha ndipo niweke wazi kwanini wenyewe wanasema ni kuchepuka. Bila shaka wanajua kwamba kitendo hiki ni kufanyia hiyana familia yako......
News ID: 120


Kama tulivyotanguliza ni kwamba kila mwanafamilia anatakiwa kuwa makini katika kuhakikisha kwamba nguzo za familia yake zinashikamana na mahusiano ambayo ni sahihi. Hapa tulikuwa tunajaribu kulenga kwamba kuna mahusiano ambayo si sahihi katika jamii, na mwisho wa mahusiano haya ambayo si sahihi ni kuharibu na kuvunja misingi ya familia n a jamii kwa ujumla kutokana na athari zake mbaya.

Tutajaribu kuelezea baadhi ya mahusiano hayo ambayo si sahihi pamoja na athari zake zinazoambatana nayo.

1.   Zinaa

Moja kati ya mambo ambayo huhesabika ni katika mahusiano ambayo si sahihi ni swala zima la uzinzi au zinaa, kwa lugha ya sasa wanaita (michepuko) kwa maana ya mahusiano yasiyo rasmi.

Kwanza nishukuru kuona kwamba wenyewe wanakubali kwamba kitendo hiki ni kuchepuka na kutoka katika njia kuu, kisha ndipo niweke wazi kwanini wenyewe wanasema ni kuchepuka. Bila shaka wanajua kwamba kitendo hiki ni kufanyia hiyana familia yako, jambo ambalo si jema  kiakili hata kidini pia, pia kuna athari nyingine ambazo zinakuja kama vile kukosa heshima ya watoto wake, kupungua mapenzi yake kwa familia yake n a mengineyo. Lakini cha kushangaza ni kwamba jambo hili la zinaa ndilo jambo ambalo limeenea sana katika vizazi vya zama hizi kama ambavyo Muhammad bin Farid Wujdiy anasema "....Jambo la kusikitisha mno ni kwamba swala la zinaa ndilo ambalo limechukua sura mno n akuenea katika karne hii pamoja na mambo mengine ambayo hayaendani na mfumo sahihi wa maisha ya wanadamu....”

Ndio, leo hii vijana ambao tayari wamefikia umri wa kuoa hawataki kabisa kusikia jambo hilo, wakiwa na hoja ya kwamba wakijiingiza katika ndoa basi maisha yatawaendesha sana na watatakiwa wafanye kazi mno, au wakati mwingine hutoa hoja ya kwamba kama wakitaka kuoa hali ya kuwa hawana maisha mazuri na kipato kizuri cha pesa basi watashindwa kuoa katika familia au nyumba za wenye uwezo wao kimaisha. Hivyo hutumia muda mwingi sana katika kutafuta vipato, majina, au maisha mazuri ili tu waweze kuoa hao ambao wanawafikiria. Lakini wanasahau kwamba wakati ambao yeye anajishughulisha na kutafuta hayo maisha mazuri, si kwamba zile hisia kali zinampa nafasi pia, bali zinaendelea kumshawishi na kumsukuma kuelekea upande uutakao, hivyo kujikuta huku akisubiri mke wa ndoto zake hapa kati anakuwa amefanya mambo mengi sana ambayo si sahihi kwake (kama ilivyo kwa vijana wengi sana wa sasa).

Cha muhimu ni kwamba kila familia na jamii kwa ujumla kuweza kuweka mifumo sahihi ya kuweza kuepukana na janga hili kubwa ambalo hakuna jamii ambayo itashikamana nalo  ila ni kwamba Mwenyezi Mungu ataiadhibu jamii ile kwa aina mbalimbali za adhabu. Hii ni ukiachilia bali adhabu ambazo Uislamu umeziweka kwa kila mwenye kufanya kitendo hicho na kwa masharti yake ambayo yameelezewa kwa kirefu katika surat Al Nur aya ya 2 pale Mwenyezi Mungu aliposema:

الزَّانِيَةُ وَالزَّانِي فَاجْلِدُوا كُلَّ وَاحِدٍ مِنْهُمَا مِائَةَ جَلْدَةٍ ۖ وَلَا تَأْخُذْكُمْ بِهِمَا رَأْفَةٌ فِي دِينِ اللَّهِ إِنْ كُنْتُمْ تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ۖ وَلْيَشْهَدْ عَذَابَهُمَا طَائِفَةٌ مِنَ الْمُؤْمِنِينَ

"....Mzinifu mwanamke na mzinifu mwanamume, mtandikeni kila mmoja katika wao bakora mia. Wala isikushikeni huruma kwa ajili yao katika hukumu ya Mwenyezi Mungu, ikiwa nyinyi mnamuamini Mwenyezi Mungu na Siku ya Mwisho. Na lishuhudie adhabu yao kundi la Waumini...”

Pamoja n akwamba kuna ambao wanajiona wao ni wajuaji wakubwa wa haki na wenye huruma kubwa sana kwa wanadamu, ambao wanakuja na kusema kwamba hukumu hii ni yenye kuonea na haiendani kabisa na huruma kwa wanadamu. Ati!!, hivi kuna mwenye huruma kwa viumbe zaidi ya aliyeviumba?, lazima itambulike kwamba hukumu hii ni yenye kulenga kutengeneza familia na jamii iliyo bora zaidi, je kuna huruma zaidi ya hii?, hivyo basi ikiwa kuna jambo lolote ambalo linataka kuja kuharibu yale yaliyo bora kwa wanadamu ni lazia likemewe na lichukuliwe hatua kali.

2.   Kuingiliana kinyume na maumbile

Moja kati ya mifumo ambayo inakuja kupiga vita n a kutokomeza kabisa mfumo sahihi wa maisha ya kifamilia na kijamii kwa ujumla ni mfumo wa wanadamu kuchagua maisha ya kuingilia na kinyume na maumbile wao kwa wao au kwa ibara nyingine ni mapenzi ya jinsia moja.

Kwa maana baada ya jambo hili basi hakutakuwa tena na malengo ya kufikiria kujenga familia au jamii kwa ujumla. N a hapa naongelea kwa ujumla kabisa, iwe anayefanya jambo hili ni mtu ambaye tayari ana familia yake, au awe hana familia. Kwa maana kama atakuwa na familia yake kisha akashiriki jambo hili huko nje bila shaka zile athari za kutokuwa na mapenzi na familia yake na nyinginezo bado zitaambatana naye, na kama atakuwa hana familia basi ndio kabisa, maana hata hiyo fikra ya kuwa na familia na jamii hatokuwa nayo.

Lakini kwa zama hizi swala la mapenzi ya jinsia moja ni swala ambalo limeshika kasi sana, tunaambiwa katika baadhi ya nchi za Ulaya, kuna wanasheria ambao husimama kidete katika kutetea jambo hili, hali ambayo imepelekea kuona baadhi ya watu wakiacha familia zao na kutafuta vijana ambao wanaoana nao n a kuendeleza mahusiano ya jinsia moja. Sasa hiki kitendo cha mtu kutelekeza familia yake ni moja tu ya athari ambao zinatokana na jambo hili baya. Bado kuna adhabu za Mwenyezi Mungu juu ya mshiriki wa kitendo hiki kama vile:

a.    Kuuwawa kwa upanga

b.   Kuchomwa moto

c.    Kuangushiwa ukuta

d.   Kutupwa kutoka juu ya jengo refu

Na ambaye anafanyiwa kitendo hiki kama atakuwa ni mwenye kubalehe na ana akili timamu basi ni lazima auwawe, n akama atakuwa hajabalehe basi kuna hukumu zake maalumu ambazo unaweza kurejea vitabu vya hukumu.

Muhimu ni kwamba jambo hili ni katika ambo ambayo yanaharibu kabisa misingi na malengo ya familia na jamii kwa ujumla, na linatakiwa likemewe kwa nguvu zote.

itaendelea......

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: