bayyinaat

Published time: 03 ,December ,2017      18:36:53
Katika kipindi chake,suala la upasuaji wa mwili wa mwanadamu halikuwa maarufu na kimsingi suala hilo lilitambuliwa kuwa ni kinyume na maadili na mafundisho ya dini. Hata hivyo katika vitabu vyake kama kile cha Liber Almansoris, Zakaria Razi alibainisha na kuweka wazi suala la upasuaji wa mifupa, mishipa, ubongo, jicho, sikio, mapafu, moyo, utumbo na kadhalika na ...........
News ID: 143

Ubunifu mpya wa Zakaria Razi katika taaluma ya tiba

Katika kipindi chake,suala la upasuaji wa mwili wa mwanadamu halikuwa maarufu na kimsingi suala hilo lilitambuliwa kuwa ni kinyume na maadili na mafundisho ya dini. Hata hivyo katika vitabu vyake kama kile cha Liber Almansoris, Zakaria Razi alibainisha na kuweka wazi suala la upasuaji wa mifupa, mishipa, ubongo, jicho, sikio, mapafu, moyo, utumbo na kadhalika na kueleza picha ya uti wa mgongo, matundu yake, uboho na kadhalika. Razi alikuwa tabibu wa kwanza aliyetambua baadhi ya mishipa katika kichwa na shingo ya mwanadamu na kutoa maelezo na ufafanuzi kuhusu viungo hivyo.

Tabibu Razi pia alikuwa miongoni mwa watu wachache sana ambao katika zama hizo walisisitiza umuhimu na nafasi ya elimu ya lishena chakulana mchango wake katika afya ya mwanadamu. Katika uwanja huo Razi ameandika kitabu alichokipa jina la "Manufaa ya Vyakula na Madhara Yake" ambacho kimekusanya mambo yote ya tiba ya afya ya chakula. Kitabu hicho kina faslu na milango kadhaa. Ndani yake, tabibu Razi ameeleza sifa za vyakula mbalimbali, sababu za kuwa na hamu ya chakula na kinyume chake, mmengenyo wa chakula, mazoezi ya viungo, na kadhalika.

Razi alikuwa mtu wa kwanza aliyeanza mchakato wa kubadili Alkemi(Alchemy) kwa maana ya kemia ya karne za kati iliyokusudia kugeuza metali ya kawaida kuwa dhahabu, na kuifanya elimu ya kemia. Kutokana na mbinu zilizotumiwa na msomi huyo Mwislamu wa Iran, tunaweza kusema kuwa, Razi alikuwa miongoni mwa waasisi wa elimu ya kemia.

Mkemia wa KijerumaniDakta Julius Ruska ambaye amefanya uhakiki kuhusu vitabu na maandiko ya msomi huyo wa Kiislamu ameandika kuwa: Kwa mara ya kwanza kabisa,Razi alianzisha mfumo mpya katikaelimu ya kemiaambao tunaweza kuupa jina la mfumo wa elimu ya vitendo na nadharia ya kemia. Miongoni mwa matundamuhimu ya tabibu Razi ni ugunduzi waasidi sulfuriki na alikoli.

Razi alitabahari sana katika elimu nyingi za sayansi asilia (bayolojia, kemia na fizikia), na vilevile katika metafizikia, yaani falsafa ya kuchunguza chanzo cha uhai na maarifa, na ameandika vitabu vingi katika elimu hizo. Faharasa ya kwanza kabisa ya vitabu vya Zakaria Razi iliandikwa na yeye mwenyewe na inapatikana katika kitabu cha al Fihrist kilichoandikwa na mtaalamu maarufu wa vitabu katika karne ya nneHijria, Ibn Nadeem.

Faharasa hiyo inaonesha kuwa, Razi aliandika vitabu 184 katika maudhui mbalimbali kama tiba, mantiki, hisabati, falaki, falsafa na sayansi asilia.

Vitabu vyake

Miongoni mwa vitabu mashuhuri vya Razi ni Kitab al-Hawi fi al-Tibb(Liber Continens) ambacho kinahesabiwa kuwa tabu kubwa (encyclopedia)la maarifa ya tiba. Ndani ya kitabu hichopia kuna nadharia za madaktari na matabibu wa kabla ya Zakaria Razi. Kitabu hicho kilitarjumiwa kwa lugha ya kilatini mwaka 1297 Miladia. Kitabu kingine cha msomi huyo Mwislamu ni Tiba ya Mansuri (Liber Almansoris). Kitabu hiki ndicho cha pili kwa umuhimu sana kati ya vitabu vya msomi huyo baada ya kile cha al Hawi.Katika kitabu hiki, Razi ameeleza elimu msingi ya masuala ya udaktari katika makala kumi. Makala ya tisa ya kitabu hicho ina kichwa cha maneno: Tiba ya maradhi yote kuanzia utosini hadi kidole gumba. Makala hii imechapishwa Ulaya katika kitabu kinachojitegemea na hadi mwishoni mwa karne ya 15 kilikuwa sehemu ya ratiba ya masomo ya tiba barani Ulaya.

Nyakati za mwisho za uhai wake

Muhammad bin Zakaria Razi alipitisha kipindi cha mwishoni mwa umri wake katika mji wa Rei ambako alifundisha na kulea wanafunzi wengi waliotokea kuwa mabingwa katika elimu ya udaktari. Kipindi hicho macho ya Razi yaliingiwa na mtoto wa jicho na mmoja wa wanafunzi wake kutoka Tabaristan alikwenda Reikwa ajili ya kumtibu mwalimu wake. Razi alimwambia mwanafunzi kwamba, kazi hiyo itamzidishia mashaka na maumivu nakwamba anahisikifo chake kilikuwa kimekaribia; hivyo hakuna haja ya kujitia mashakani kwa ajili ya kurejesha uwezo wake wa kuona.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa na mwaka 312 Hijria Muhammad bin Zakaria Razi aliaga dunia katika mji alikozaliwa wa Reinchini Iran.
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: