bayyinaat

Published time: 05 ,December ,2017      12:24:41
Hili kwa asili ni jambo jema sana na linalofaa kutukuzwa na kila mmoja, ila kwa kuwa tunataka kufikia katika hali njema zaidi basi ni wajibu wetu kuweza kuhamisha ada hii kutoka katika hali ya kusherehekea tu na kuihamisha katika hali ya kujifunza mambo muhimu kutoka...........
News ID: 144

Kwa hakika jambo la kusherehekea mazazi ya Mtukufu Mtume Muhammad (saww) ni katika mambo ambayo Waislamu wa dunia nzima wamelizoea kuanzia tangu na tangu, n apia ni katika mambo ambayo yamekuwa yakidumishwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja mpaka kingine, mpaka kufikia hali y akwamba swala hili limekuwa ni lenye kuadhimishwa kuanzia ngazi ya mijumuiko mikubwa mpaka kufikia sasa limekuwa likiazimishwa hata kwa ngazi za familia fulani.

Lakini hii yote ni kwa minajili tu ya kuonyesha kwamba huyu mtu wanayemuadhimisha si kwamba ni mtu wa kawaida, n a hivyo katika upande huu Waislamu wanakuwa kama Umma nyinginezo ambazo zimekuwa zikiadhimisha masiku muhimu yao matukufu ikiwa ni pamoja na kutukuza zama hizo takatifu.

Hili kwa asili ni jambo jema sana na linalofaa kutukuzwa na kila mmoja, ila kwa kuwa tunataka kufikia katika hali njema zaidi basi ni wajibu wetu kuweza kuhamisha ada hii kutoka katika hali ya kusherehekea tu na kuihamisha katika hali ya kujifunza mambo muhimu kutoka katika maadhimisho haya, hii sio mada yangu kwa siku ya leo, japokuwa imepita kutokana na hali ya maneno kuvuta maneno yanayofanana nayo.

Tukirudi katika mada ni kwamba pamoja na kwamba kuna kila dalili ya kuonyesha kwamba swala la kusherehekea au kukumbuka mazazi ya Mtume (saww) ni jambo jema na lenye kusifiwa na wala halina tatizo lolote lile, bado unakuta kuna baadhi ya watu ambao wao kila kukicha wao ni wenye kutafuta sababu tu za kuweza kusimamisha jambo hili, nasema hivi kwa sababu mpaka leo hii bado hawajapata la kusema na wala hawatakuja kupata la kusema katika kusimamisha swala hili. Japokuwa wenyewe wanajinadi ya kwamba wamepata msingi wa kusimamisha swala hili.

Ila kwa mujibu wa maneno yao au kwa ibara sahihi ni kwamba kutokana na wataalamu kusoma maneno yao wamekuja kugundua kwamba, jambo ambalo limepelekea wao kuamini kwamba wana hoja thabiti ya kusimamisha swala hili ni kutokana na ufahamu wao usio sahihi katika kuelewa na kuelezea maana sahihi ya neno "Bidaa” "Uzushi katika dini”. Na kutoelewa kwao huku kumepelekea kuharamisha mambo mengi sana ambayo yana misingi katika dini yetu, kwa kuishia tu kusema kwamba mambo hayo hayana dalili mahususi inayo yahusu.

Na hapa ndugu msomaji ndipo ambapo ningependa kuanzia mazungumzo yetu haya kuhusiana na kusherehekea mazazi ya Mtume (saww), ambapo kwanza tutaangalia uhalali n ausahihi wake, kisha kuja kujadili hizo rai za hao ambao wanaamini kwamba wamefanikiwa kwazo kusimamisha swala hili kisheria.

Ila katika kubainisha swala hili kuna baadhi ya mambo kwanza ningependa yawe kama utangulizi n a ufunguo wa kuingia katika mada yetu kwa hivyo vipengele viwili. Napenda itambulike kwamba:

1.    Matukio matukufu siku zote huwa yanafanya masiku yake kuwa na utukufu pia.   

Hapa namaanisha nini?, nataka kusema kwamba siku kama siku haiwezi kuwa na utukufu fulani ikiwa hakuna jambo tukufu ambalo limetokea ndani yake, angalia mifano katika masiku kama Eid Fitr na Adh-ha, Usiku wa Lailatul Qadr, Masiku ya mwezi wa Ramadhani, Siku ya kutumilizwa Bwana Mtume (saww), na matukio mengineyo mengi mno, utakuta kwamba utukufu wa masiku haya unatokana na jambo ambalo lipo ndani ya siku ile, na wala si asili ya siku yenyewe.

Mfano imepokelewa katika riwaya za ubora wa siku ya Ijumaa kutoka katika Sahih Muslim kwamba "......Mwenyezi Mungu alimuumba Adamu siku ya Ijumaa na pia kumpeleka Peponi siku ya Ijumaa...”[1]

Au ukirejea katika baraka za mwezi wa Ramadhani ni kwamba Mwenyezi Mungu mwenyewe amesema "......Mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imeteremka Quran.....”[2].

Au kunako Usiku wa Cheo na daraja "Lailatul Qadr”, unakuta Mwenyezi Mungu anasema "...Hakika sisi tumeiteremsha katika usiku wa cheo,  n ani jambo gani litakalokujulisha ni upi huo usiku wa cheo?, usiku wa cheo ni bora kuliko miezi Elfu moja.........”.[3]

Unakuta kwamba masiku haya yote yamepata sifa hizo kutokana na uzito wa matukio ambayo yametukia katika siku hizo.

        Sasa tuje katika asili ya mada yetu n a kujiuliza swali moja tu ambalo ni, ikiwa masiku hupata utukufu kutokana na matukio yanaotukia ndani ya siku hiyo, kwanini siku ya kuzaliwa Mtume isiwe ni katika mfumo huu pia?, yaani ikawa siku hii nayo inachukua utukufu kutokana na tukio tukufu la kuzaliwa Bwana na mbora wa viumbe vyote, au kuna mwenye kukataa kwamba kuzaliwa kwa Mtume Muhammad si katika matukio matakatifu?.

Itaendelea sehemu ya pili......[1] Sahih Muslim Kitabu Swala, Mlango wa Fadhila za siku ya Ijuma

[2] Baqara 185

[3] Al Qadr aya 1-3

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: