bayyinaat

Published time: 21 ,February ,2018      22:05:51
News ID: 234

Tupo katika mwendelezo wa kujadili njia ambazo zinaweza kutumia ili mwanadamu aweze kujiepusha na mahusiano yasiyo sahihi, ambapo kwa sasa tunaangalia namna yakujiepusha na swala la kujichua. Karibu sana.

1. Kushiriki mazoezi

Moja ya njia ambazo zinaweza kumkomboa mwanadamu kutoka katika utumwa wa kujiridhisha kijinsia, ni swala zima la kushiriki mazoezi.

Na hapa katika mazoezi kuna mambo mengi sana ambayo yanaingia ndani yake, kwani lengo hasa ni kwamba huyu mtu apate jambo la kumshughulisha na kumsahaulisha kunako ada yake hiyo, hivyo anaweza kushiriki katika mambo mbalimbali kama vile matendo ya fani za uchoraji au kujisomea mambo yenye faida.

2. Kubadili mfumo wa chakula

Bila shaka kuna baadhi ya vyakula ambavyo vinahemua hisia za mwanadamu na kumfanya afikirie swala la kushiriki tendo la ndoa, sasa kwa huyu ambaye yeye hana mke na anakabiliana na janga la kujiridhisha ni vyema kwake kutokula kabisa vyakula hivyo. Mfano wa vyakula hivyo ni kama vile siki, vilevi, ulaji wa nyama sana na vinginevyo ambavyo vinahamisha kushiriki tendo la ndoa, na badala yake ale vyakula kama vile mbogamboga na matunda.

3. Kufuata misingi ya Afya

Kwamba mtu mwenye kushiriki tendo la kujiridhisha basi ni muhimu sana kuweza kuzingatia baadhi ya mambo ambayo yanashauriwa na wataalamu wa afya, kama vile usafi, kutobakia kitandani muda mrefu baada ya kuamka pamoja na kujishughulisha na mambo yenye faida.

Hizi ni baadhi tu ya njia ambazo zinaweza kumfanya mwanadamu kupukana na janga la kujiridhisha, lakini kama tulivyosema kwamba hakuna njia sahihi na salama kama vile vijana kuhamasishwa kuoa haraka, kwani kama bado mtu ataendelea kujichua baada ya kuwa ameshaoa inakuwa rahisi sana kuelewa kwamba tatizo lake halikuwa kukidhi tu haja za kimwili, bali alikwa na tatizo lingine.

Hivyo basi kiujumla tunaweza kusema kwamba mambo ambayo tumetoka kuyataja hapo juu, ndio mambo ambayo yanapingana kabisa na falsafa ya utengenezaji wa familia, na ndio maana tukayapa jina la mahusiano ambayo si sahihi. Kwa maana mwenye kujihusisha na mahusiano hayo basi kama alikuwa na familia basi familia yake itabomoka, na kama alikuwa hana familia basi ndio anaharibu kabisa hata mipango ya kuwa na hiyo familia.

Asante sana kwa kuwa nami katika mada hii, usiache kuungana nami tena katika mada ijayo.

Sh Abdul Razaq Bilal


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: