bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      20:58:34
News ID: 258

MADHUMUNI YA KUTOA NA SADAKA KWA MUJIBU WA MANENO YA MAASUMINA (A.S).

Utoaji na sadaka ni kanuni ya kijamii katika dunia ya maumbile na hususan katika ujenzi wa mwili wa kila kiumbe aliye hai; si moyo pekee wa Mwanadamu upo kwa ajili ya kuendesha mwili, bali ziko seli mbalimbali zenye kuusaidia moyo katika kuendesha mwili wa binadamu, ubongo, ini na viungo vingine vya mwili wa mwanadamu vyote ni chanzo cha kusambaza damu ndani ya mwili na usuli ya maisha ya mafungamano ya mwili, hivyo bila mawasiliano hayo hakuna maana ya kupeleka na kupokea mawasiliano ya kuendesha mwili.

1) Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):

إِنَّ عَلَى كُلِّ مُسْلِمٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ صَدَقَةً، قِيلَ: مَنْ يُطِيقُ ذَلِكَ؟ قَالَ (ص): إِمَاطَتُكَ الْأَذَى عَنِ الطَّرِيقِ صَدَقَةٌ وَ إِرْشَادُكَ الرَّجُلَ إِلَى الطَّرِيقِ صَدَقَةٌ وَ عِيَادَتُكَ الْمَرِيضَ صَدَقَةٌ وَ أَمْرُكَ بِالْمَعْرُوفِ صَدَقَةٌ وَ نَهْيُكَ عَنِ الْمُنْكَرِ صَدَقَةٌ وَ رَدُّكَ السَّلَامَ صَدَقَةٌ.

"Hakika ni wadhifa wa kila Mwislamu kila siku atoe sadaka, akaulizwa: Ni nani awezae hilo?

Akasema (s.a.w.w): Iwapo utaondoa kitu ambacho kitakuwa ni adha kwa wengine njiani hakika hiyo ni sadaka, na kumuelekeza aliyepotea njia pia ni sadaka, na kumtembelea mgonjwa ni sadaka, na kuamrisha mema na kukemea mabaya ni sadaka, na kuitikia salamu ni sadaka”.[1]

2) Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w):

«مِنَ الصَّدَقَةِ أَنْ يَتَعَلَّمَ الرَّجُلُ الْعِلْمَ وَ يُعَلِّمَهُ النَّاس‏».

"Ni katia amali za sadaka mtu kujifunza elimu sahihi na kuwafundisha watu elimu hiyo”.[2]

3) Amesema tena (s.a.w.w):

«كُلُّ مَعْرُوفٍ صَدَقَةٌ وَ الدَّالُّ عَلَى الْخَيْرِ كَفَاعِلِهِ وَ اللَّهُ يُحِبُّ إِغَاثَةَ اللَّهْفَان‏».

"Hakika kila jambo jema ni sadaka, na mwongozaji juu ya jambo la heri ni mithili ya mtenda mema, na Mwenyezi Mungu anampenda asikiaye sauti ya wanyonge na waliodhulumiwa”.[3]

4) Amesema (s.a.w.w):

«كُلُّكُمْ يُكَلِّمُ رَبَّهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ لَيْسَ بَيْنَهُ وَ بَيْنَهُ تَرْجُمَانٌ فَيَنْظُرُ أَمَامَهُ فَلَا يَجِدُ إِلَّا مَا قَدَّمَ وَ يَنْظُرُ عَنْ يَمِينِهِ فَلَا يَجِدُ إِلَّا مَا قَدَّمَ ثُمَّ يَنْظُرُ عَنْ يَسَارِهِ فَإِذَا هُوَ بِالنَّارِ فَاتَّقُوا النَّارَ وَ لَوْ بِشِقِّ تَمْرَةٍ فَإِنْ لَمْ يَجِدْ أَحَدُكُمْ فَبِكَلِمَةٍ طَيِّبَة».

"Nyote, siku ya kiama pasi na wasila wala mkalimani mtazungumza pamoja na Mwenyezi Mungu, basi ataangalia mbele yake mmoja wenu na hatopata kitu chochote ila kile alichokitanguliza, na ataangalia kulia kwake na hatopata kitu ila kile alichokitanguliza, kisha atatazama kushoto kwake atauona moto, hivyo basi uogopeni moto hata kwa kipande cha tende, na asipokipata mmoja wenu basi aseme hata neno moja lililokuwa zuri.”.[4]

5) Amesema tena (s.a.w.w) kuwaambia Masahaba wake:

«أَ لَا أُخْبِرُكُمْ بِشَيْ‏ءٍ إِنْ أَنْتُمْ فَعَلْتُمُوهُ تَبَاعَدَ الشَّيْطَانُ مِنْكُمْ كَمَا تَبَاعَدَ الْمَشْرِقُ مِنَ الْمَغْرِبِ قَالُوا بَلَى قَالَ الصَّوْمُ يُسَوِّدُ وَجْهَهُ وَ الصَّدَقَةُ تَكْسِرُ ظَهْرَه‏».

"Je! Nikuhabarisheni kitu ambacho ikiwa mtakifanya Shetani atajiweka mbali nanyi kama ulivyokuwa umbali wa mashariki kwa magharibi?

Wakasema: ndio;

Akasema: Saumu huufanya uso wa sheitani kuwa mweusi, na sadaka huvunja uti wa mgongo wake”.[5]

UTOAJI WA KIMALI NA UMUHIMU WAKE.

Kwa hakika katika riwaya nyingi za Kiislamu zimekuja maana nyingi ambazo kwamba zinaonyesha kuacha suala la kutoa (Zaka) ni sawa na kukufuru kwa anuani ya mifano ya riwaya hizo:

1. Katika hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Imamu Sadiq (a.s) tunasoma kutoka katika sentensi ya nasaha za Mtume kwa Imam Ali (a.s) ambayo ni kama ifuatayo:

«یا علی! کفر بالله من هذه الأمة عشرة... وعد منهم مانع الذکاة، ثم قال یا علی! من منع قیراطا من زکاة ماله فلیس بمؤمن ولا مسلم ولا کرامة، یا علی تارک الزکاة یسئل الله الرجعة إلی الدنیا، وذلک قوله تعالی: «حَتَّى إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ».

"Ewe Ali! Makundi kumi katika umma huu wamemkufuru kukubwa Mwenyezi Mungu… na moja kutoka katika kumi hawa ni mwenye kuzuia zaka.. kisha akasema: Ewe Ali! Yeyote atakaye zuia haya thumni ya zaka ya mali yake basi si muumini, na si Mwislamu na hana thamani yoyote mbele ya Mwenyezi Mungu.

Ewe Ali: Mwenye kuacha kutoa zaka wakati wa kufa kwake ataomba kurejeshwa duniani ili atende aliyoacha, na hii imekwisha kuja katika kauli ya Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake kitukufu aliposema: "Mpaka yanapomfikia mmoja wao mauti, husema: Mola wangu Mlezi! Nirudishe””.[6]



[1] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 72, uk 50.

[2] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 2, uk 24.

[3] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 93, uk 119.

[4] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 93, uk 131.

[5] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 93, uk 114.

[6] Tafsir al amthal. Juz 20, uk 219.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: