bayyinaat

Published time: 11 ,March ,2018      21:12:48
"Na wapewe mafakiri walio zuilika katika njia za Mwenyezi Mungu, wasio weza kusafiri katika nchi kutafuta riziki. Asiye wajua hali zao huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambua kwa alama zao; hawang'ang'analii watu kwa kuwaomba. Na kheri yoyote mnayotoa, basi kwa yakini Mwenyezi Mungu anaijua”
News ID: 260

SHARTI LA NNE: Ni sadaka kuitoa kwa wenye kuhitajia kweli, kwa maana; kuwapa wale wenye mahitaji mazito, na watazamiwe kwa kupewa kipaumbele.

Mwenyezi Mungu mtukufu anasema:

«لِلْفُقَرَاءِ الَّذِينَ أُحْصِرُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ لَا يسْتَطِيعُونَ ضَرْبًا فِي الْأَرْضِ يحْسَبُهُمُ الْجَاهِلُ أَغْنِياءَ مِنَ التَّعَفُّفِ تَعْرِفُهُمْ بِسِيمَاهُمْ لَا يسْأَلُونَ النَّاسَ إِلْحَافًا وَمَا تُنْفِقُوا مِنْ خَيرٍ فَإِنَّ اللَّهَ بِهِ عَلِيمٌ».

"Na wapewe mafakiri walio zuilika katika njia za Mwenyezi Mungu, wasio weza kusafiri katika nchi kutafuta riziki. Asiye wajua hali zao huwadhania kuwa ni matajiri kwa sababu ya kujizuia kwao. Utawatambua kwa alama zao; hawang'ang'analii watu kwa kuwaomba. Na kheri yoyote mnayotoa, basi kwa yakini Mwenyezi Mungu anaijua”.[1]

SHARTI LA TANO: Ni kwamba sadaka bora ni ile itolewayo kwa siri na uficho.

Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

«إِنْ تُبْدُوا الصَّدَقَاتِ فَنِعِمَّا هِي وَإِنْ تُخْفُوهَا وَتُؤْتُوهَا الْفُقَرَاءَ فَهُوَ خَيرٌ لَكُمْ وَيكَفِّرُ عَنْكُمْ مِنْ سَيئَاتِكُمْ وَاللَّهُ بِمَا تَعْمَلُونَ خَبِيرٌ».

"Mkizidhihirisha sadaka ni vizuri; na mkizificha mkawapa mafakiri kwa siri basi hivyo ni kheri kwenu, na yatakuondoleeni baadhi ya maovu yenu. Na Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda”.[2]

Katika Aya hii tukufu imezungumzia pande zote mbili za sadaka, yaani sadaka ya uwazi na bayana na pia sadaka ya siri, imesema: Ikiwa mtadhihirisha sadaka zenu ni vizuri, kwa upande ambao kwamba wengine watapenda amali zenu na kazi zenu za misaada kwa wasio jiweza, lakini ikiwa mtazificha na mkawapa mafakiri wenye kuhitajia misaada ni bora, kwani amali hii itakuepushieni afa la ugonjwa mbaya ambao ni (Riyaa) kujionyesha, na mtu yule fakiri pia atasalimika kutokana na udhalili wa kupokea sadaka.

UTOAJI NA SADAKA YA SIRI KWA MUJIBU WA KAULI ZA MAASUMINA

1. Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) imenukuliwa kuwa amesema:

«يَا عَمَّارُ الصَّدَقَةُ فِي السِّرِّ وَ اللَّهِ أَفْضَلُ مِنَ الصَّدَقَةِ فِي الْعَلَانِيَة».

"Ewe Ammar! Ninaapa kwa Mwenyezi Mungu ya kwamba sadaka itolewayo kwa siri ni bora zaidi kuliko itolewayo kwa wazi/ bayana”.[3]

2. Kutoka kwa Imam Ali (a.s) imenukuliwa ya kwamba amesema:

«... صدقة السر فإنها تذهب الخطیئة وتطفئ غضب الرب».

"Sadaka ya siri kwa hakika huondoa madhambi na kuzima ghadhabu ya Mwenyezi Mungu mtukufu”.[4]

3. Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) imenukuliwa kuwa amesema:

«صدقة العلانیة تدفع سبعین نوعا من البلاء و صدقة السر تطفئ غضب الله».

"Sadaka ya dhahiri huzuia aina sabini ya balaa na sadaka ya siri huzima ghadhabu ya Mwenyezi Mungu”.[5]

4. Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) imenukuliwa kuwa amesema:

«الصدقة تطفئ الخطیئة کما تطفئ الماء النار وتدفع سبعین نوعا من البلاء».

"Hakika sadaka huzima madhambi kama ambavyo kwamba maji huzima moto na huzuia aina sabini za balaa”.

SWALI: Hapa imeelezwa ya kwamba kwanini zaka na sadaka za wajibu kuwa kuidhihirisha ni bora?

JAWABU: lazima ifahamike kuwa; Huenda ni kwa sababu ya vitu viwili:

1. Ni kwa ajili ya kwamba mtu asituhumiwe, yaani watu wasiseme ya kwamba mtu huyu si mtoaji wa sadaka na ni mwovu.

2. Au kwamba wengine waonapo watafuata mwenendo wake, kama vile ambavyo Sala za sunna ni bora zisaliwe kwa siri na mbali ya upeo wa macho ya watu wengine badala ya kuzifanya kwa kutaka kuonekana, lakini Sala za wajibu ni bora zikasaliwa msikitini na jamaa pia.



[1] Surat al Baqara/ 273. Rejea: Anwaar al Hidaayah, juz 1, uk 79-81.

[2] [2] Surat al Baqara/ 271.

[3] Rejea: Bihaar al anwaar, juz 52, uk 127, Riwaya ya 20.

[4] Rejea ile ile, juz 96, uk 177, riwaya 90.

[5] Rejea ile ile, uk 179, riwaya 20.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: