bayyinaat

Published time: 27 ,March ,2018      20:24:16
News ID: 280

2. Nguvu ya Ndoa na Kujamiiana

Pia ni neema nyingine ambayo Mwenyezi Mungu amewajaalia wanadamu, kwamba ili jamii ya wanadamu iendelee kuwepo ni lazima swala la ndoa lichukue nafasi yake. Tena pamoja na kwamba jambo hilo ni neema bado utakuta Uislamu unahimiza sana kutimizwa kwa jambo hilo, kama ambavyo imepokelewa kutoka kwa Mtume kwamba mwenye kuoa basi anakuwa ametimiza nusu ya dini yake.

Sasa balaa linaweza kutokea endapo tu neema hii na jambo hili likatumiwa kwa njia ambazo si sahihi, kwa maana lazima tutambue kwamba katika kutekeleza haya matamanio ambayo Mwenyezi Mungu ameyaweka kuna njia maalumu, sasa endapo njia hizo hazitafuatwa basi hakutakuwa na heri bali ni maandamano na mabalaa matupu.

Hadithi imepokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad (saww) anasema:

"أكثر ما تلج به أمتي النار الأجوفان: البطن والفرج"

".....Jambo ambalo litaingiza umma wangu sana motoni ni kati mbili, tumbo na tupu”

Kutokana na matumizi ambayo si sahihi ya vitu hivi viwili. Lakini wakati huo huo Imamu Ally (as) anakuja na njia ya kutuzuia kuingia katika balaa litokanalo na neema hii tuliyopewa, anasema:

فرحم اللَّه رجلاً نزع عن شهوته وقمع هوى نفسه"

"....Mwenyezi Mungu amrehemu mja ambaye amejiepusha na matamanio yake, na kupinga matakwa ya nafsi yake...”[1]

Kwamba mwenye kutaka kushindana na vishindo vya neema ya matamanio ya kimwili (hasa katika swala la kujamiiana), basi ni bora afuate njia sahihi kwanza, au aiminye nafsi yake kwa yale ambayo si sahihi na bado nafsi inamwamrisha, kwani kuiacha nafsi ikutawale mwisho wake si mzuri.



[1] Nahjul Balagha Hotuba 176


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: