bayyinaat

Published time: 02 ,April ,2018      12:16:11
News ID: 281


 Nguvu ya Hasira

Ni jambo la kawaida kushuhudia mikinzano na mifarakano katika maisha ya kila siku, japokuwa lengo la Ubinadamu ni kuhakikisha kwamba hii migongano inakoma na inaisha kabisa, hivyo hapa tunazungumza kutokana na hali insi ilivyo na si inavyotakiwa kuwa.

Sasa ikiwa jambo la migongano na mikwaruzano ni jambo la kawaida katika maisha yetu, kuna umuhimu wa kila mmoja wetu kujikinga na kuhakikisha kwamba anakabiliana na migongano hiyo. Na kwa kuwa Mwenyezi Mungu ni mjuzi wa kila jambo ambalo linamtokea huyu mwanadamu, hakumwacha hivi hivi bila ya kumpatia jambo ambalo litakuwa ni lenye kumjuza kunako yenye kumkera yeye kama mwanadamu ili ajue ni namna gani ataweza kukabiliana nayo, na hapo ndipo alipopatiwa nguvu ya hasira.

Kwa hiyo hasira kama hasira ni moja ya neema za Mwenyezi Mungu kwa wanadamu bali hata wanyama katika kuhakikisha kwamba wanatambua yenye kuwakera na kujikinga nayo.

Sasa tatizo litakuja katika sehemu moja kunako neema hii, ni pale ambapo hasira zitatumika katika mambo ambayo si yake, hapa hasira zinageuka na kuwa wendawazimu.

Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ally (as) akisema:

"الحدّة ضر من الجنون لأن صاحبها يندم، فإن لم يندم فجنونه مستحكم"

"..Hasira ni sehemu ya wendawazimu, kwani mwenye kuwa nazo hujuta, a endapo hatojuta basi wendawazimu wake ni wenye kuthibiti...”

Hivyo kwa minajili hii ni kwamba nguvu ya hasira inaweza kutumika kwa ajili ya kuelekea katika ukamilifu wetu endapo tu tutaitumia ama ilivyokusudiwa, na endapo itakuwa kinyume na hivyo basi itapelekea katika maangamio.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: