bayyinaat

Published time: 02 ,April ,2018      14:12:44
Ni Sura maarufu, yenye fadhila nyingi sana kwa mwenye kuisoma, inatosha tu kuelewa kwamba Sura hii inachukua nafasi ya Theluthi ya Quran kutokana na daraja na cheo chake kama ilivyopokelewa kutoka kwa Mtume Muhammad (saww) aliposema:
News ID: 283

Jambo la kuzingatia katika aya hii ni kwamba makafiri walitarajia kutoka kwa Mtume jibu ambalo litaendana na matakwa yao, kwamba Mtume aje asema huyu hapa ndiye Mungu ninayewalingania kwake, kwa maana nyingine awajibu kwa kutumia kiashiria cha karibu kihisia, lakini Mwenyezi Mungu katika kumpa jibu Mtume wake akatumia kiashiria cha mbali kihisia, akatumia neno "Yeye”, ambalo ni kiashiria cha nafsi ya tatu ambayo haipo sehemu ambayo mazungumzo yanafanyika.

Hii maana yake ni kwamba, Mwenyezi Mungu hayupo karibu na nyinyi kihisia mpaka muweze kumuashiria kwa neno huyu hapa, kama ambavyo hamuwezi kumgusa wala kumuona kwa macho kama ambavyo mnaona miungu yenu. Lakini pamoja na hayo ni kwamba yupo karibu na kila mmoja wetu kwa maana ambayo si maana ya kuweza kumuhisi au kumuona.

Pia tunajifunza kutoka katika aya hii kwamba, neno "Yeye” lililotumika hapo ni neno zito mno kimaana, kwani ni neno lenye kuiwakilisha dhati ya Mwenyezi Mungu mtukufu, na ndio maana katika mafundisho yanayotoka kwa Ahlu Bayt (as) tunaambiwa kwamba neno hilo ni katika yale majina matukufu ya Mwenyezi Mungu ambayo endapo ataombwa kupitia majina hayo basi maombi huwa ni yenye kukubaliwa moja kwa moja. Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ally as kwamba amesema:

"رأيت الخضر عليه السلام في المنام قبل بدر بليلة، فقلت له: علمني شيئاً أُنصر به على الأعداء. فقال: قل: يا هو، يا من لا هو إلاّ هو. فلمّا أصبحت قصصتها على رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم فقال لي: يا علي عُلمت الاسم الأعظم

".....Usiku mmoja kabla ya vita vya Badr niliona ndotoni nikimwomba Khidhir anifundishe jambo ambalo kwalo nitawashinda maadui, akaniambia " Sema Ya Huwa, Ya mana la Huwa illa Huwa”, na nilipoamka asubuhi nikamwelezea Mtume jambo hili naye akaniambia "...Ewe Ally, hakika umefundishwa jina tukufu”.

Pia historia inasema kwamba hata siku ya vita vya Siffin, Imamu Ally alikuwa akikariri sana jina hili mpaka Ammar bin Yasir akamuuliza kunako jambo hilo, Imamu akasema "...Ewe Ammar, hakika hili ni jina Tukufu la Mwenyezi Mungu, na ni msingi wa Tawhid”.

Bado tukiwa katika hiyo hiyo aya ya kwanza ya Sura hii tukufu, tunakutana na Jina lingine la Mwenyezi Mungu, jina ambalo hakuna mwenye kushirikiana naye katika hilo, tofauti na majina yake mengine ambayo kwa namna moja au nyingine inawezekana Mungu kushirikiana na hata viumbe wake. Mfano ni yale majina ambayo yamekuwa yakiwakilisha sifa zake, kama vile "Aalim” kwa maana ya Mjuzi, sifa hii hata kiumbe anaweza kuwa nayo japokuwa haitakuwa kwa maana sawa na inayopatikana kwa Mwenyezi Mungu, lakini jina "Allah”, huwezi kulipata kwa asiyekuwa yeye Mwenyezi Mungu hata kwa maana ya chini kabisa. Ukiachilia mbali na hilo, katika Quran tukufu jina "Allah” tunaambiwa limerudiwa karibu mara Elfu moja, zaidi ya kila jina la mwenyezi Mungu, hii yote ni dalili ya utukufu na daraja ya jina hili.

Na mwisho kabisa katika aya hiyohiyo ya kwanza, Mwenyezi Mungu amemalizia kwa kujisifu kwa sifa ya "Ahad”, sifa ambayo kwa lugha yetu ya haraka tunaweza kusema ni "Mmoja”, lakini kimaana ndipo ambapo tunaweza kuelewa utofauti uliopo baina ya neno Mmoja na ile Ahad iliyokusudiwa na Mwenyezi Mungu.

Katika lugha ya Kiarabu kuna maneno mawili ambayo yanakaribiana kimatamshi, lakini yapo mbali kimaana, maneno yenyewe ni "Ahad” na "Wahid”, ambapo la kwanza lina maana ya Upweke wa kitu fulani, huku la pili likiwa na maana ya Moja. Sasa ni Umoja upi ambao Mwenyezi Mungu ameukusudia katika aya tukufu?.

Katika kujibu swali hili, nitahitajia kidogo kusherehesha maana ya hayo maneno mawili hapo juu, yaani neno Ahad na Wahid, kisha ndio tuone ni lipi ambalo linaendana na Mwenyezi Mungu.

Kuna wakati mtu unataka kuashiria kunako jambo ambalo lipo peke yake katika namna ambayo hakuna hata kitu kimoja kilichohusika katika kuwezesha jambo lile, na kuna wakati unataka kuashiria kunako jambo ambalo lipo peke yake kwa maana ya kwamba hakuna kitu chenye kufanana na kitu kile.

Na kuna wakati unataka kuelezea jambo ambalo lipo peke yake kwa maana ya umoja wake kiidadi, ukiwa na maana kwamba si viwili wala vitatu wala kuendelea.

Mwisho kabisa kuna wakati unataka kuelezea kitu ambacho kipo peke yake katika mfumo wa ugawanyaji wa vitu, yaani kuna kundi la vitu vingi vinavyoshirikiana sifa, kisha unakuja na kusema kwamba hiki kipo peke yake katika jambo fulani.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: