bayyinaat

Published time: 19 ,April ,2018      11:35:23
Hii humfanya mwanadamu huyu kufanya au kujihusisha na mambo ambayo ana uwezo nayo na kujitokeza katika maeneo na mazingira ambayo anaweza kua na nafasi muhimu au kuwa na ujumbe fulani.
News ID: 294


Mtukufu Mtume (s.a.w.w) anasema: kila mwenye kujitambua basi amemtambua mwenyezi mungu. / al-hayat j 1/362.

Hii ina maana kwamba, ukweli wenyewe na nafsi ya mwanadamu ni johari ilio nyuma ya maada na kuitambua elimu kwa hoja au kuiona na kuigusa, ni jambo ambalo limethibitisha uhakika na ukweli huu ulioko nyuma ya maada na ishara kubwa kwa ajili ya kumuamini mwenyezi mungu mtukufu.

Hivyo basi kwa kulitambua hili na kulitathmini huleta uwezo na nguvu ambazo huweza kumsaidia mtu kuishi vizuri katika familia na jamii kiujumla salama na yenye kutumia akili.

Na hivyo kumfanya mwanadamu huyu kupiga hatua kwa mahesabu na umakini katika medani mbali mbali za maisha.

Hii humfanya mwanadamu huyu kufanya au kujihusisha na mambo ambayo ana uwezo nayo na kujitokeza katika maeneo na mazingira ambayo anaweza kua na nafasi muhimu au kuwa na ujumbe fulani.

Vile vile kujitambua kwa namna fulani kunaweza kuwa kwa namna ambayo, kutamfanya muhusika kuwatambua wanadamu wote katika jamii; kwani kwa namna fulani kadiri mtu anavyokuwa na maarifa kujihusu, basi hupata fursa ya kuwatambua watu wengine pamoja na nafsi maalumu walizonazo.

Sharti la kwanza kwa ajili ya kujenga nafsi, malezi na kuikamilisha ni kitambua nafsi yenyewe.

kwani kama mtu hajatambua thamani ya uwepo na uwepo wa nafsi yake pamoja na kipaji cha juu alichonacho, hawezi kufanya idili na hima kwa ajili ya kuilea na kuiimarisha nafsi husika, na hivyo hawezi kufanya juhudi za kustafidi na vipaji alivyo navyo.

Hii inatokana na kuwa, juhudi ya kila mtu kuhusiana na kila kitu, inafungamana na kiwango cha ufahamu alionao kuhusiana na kitu chenyewe pamoja na thamani ya kitu hicho. Ndio maana tunaona kuwa, kuna vipaji, uwezo na nguvu nyingi ambazo hazitumiwi ipasavyo, na faida yake haipatikani kama inavyotakiwa, kutokana na kuwa, vitu hivyo havija tambuliwa vyema, havijagunduliwa,

Bali vimebaki katika kona zisizojulikana na hivyo vimeangamia na kutokomea taratibu.

Allah atujalie tuwe wenye kutenda kwa kujua tulitendalo.

Na Sh Shaban Juma


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: