bayyinaat

Published time: 19 ,April ,2018      11:47:10
Akili ya kweli ni nuru katika uwepo wa mwanadamu. Katika mafundisho ya Uisilamu, akili inahesabiwa kwamba, ni Mtume wa ndani wa mtu.
News ID: 296


قال امام الرضا "ع"

صديق كل امرء عقله، وعدوه جهله. اصول الكاف - ج/25

Anasema Imamu:

Rafiki wa kila mtu ni akili yake, na adui wa kila mtu ni ujinga wake.

Akili ya kweli ni nuru katika uwepo wa mwanadamu. Katika mafundisho ya Uisilamu, akili inahesabiwa kwamba, ni Mtume wa ndani wa mtu.

Lakini pia imamu Asaadiqi (a.s) amesema: Mitume ni hujja wa mwenyezi mungu kwa waja wake na hoja ya ndani baina ya waja wa Allah ni akili.

Hapo tunaikuta akili ina mchango mkubwa katika kumuongoza mwanadamu.

Tukitupia jicho hekima hii ya Imamu Ridhaa (a.s) tunaona kuwa, johari bora kabisa ya uwepo wa mwanadamu ni akili na hekima.

Pamoja na zahama kubwa ya uwepo wa mwanadamu, lakini mwenyezi mungu mtukufu anaiabidisha na kuielezea adhama (utukufu) wa akili waliopewa wanadamu na anaitambua akili kwamba, ni johari bora kabisa waliopatiwa wanadamu.

Kustafidi na kitu hiki kisicho na mithili ni kwamba, mwanadamu anapaswa kutumia akili katika kila jambo, hatua anayo chukua au kazi anayoifanya au harakati anayotaka kuifanya kwa ajili yake binafsi au kwa jamii.

Hii ni kusema kuwa, kabla ya kuchukua hatua yoyote ile inayo husiana na kazi katika uga wowote ule, mwanadamu anapaswa kutumia akili yaani aifanye akili kuwa mzani na kipimo chake. Yaani aifanye kazi hio au kuchukua hatua yoyote ile kwa tathmini ya akili, na kwa utambuzi wa akili.

Kwa hakika akili ndio inayo mtofautisha mwanadamu na mnyama; kwani mnyama yeyote huongozwa zaidi na matamanio yake badala ya akili.

Kujaaliwa akili na kuiongoza na kuitumia vema ndiko ambako humzuia na kumuokoa mwanadamu,

Akili ndio ambayo humwambia mwanadamu aitumie na kustafidi na kila tamanio na ghariza kwa njia sahihi.

Kwa msingi huo, inaeleweka kwamba katika uwepo wa mwanadamu adui na rafiki anafahamika wazi. Matamanio ya nafsi na matamanio ya kinyama yasiyo na mahesabu wala kipimo ni sababu ya kuporomoka (kuangamia) mwanadamu kimaadili na kiakh-laqi (tabia)


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: