bayyinaat

Published time: 19 ,April ,2018      12:03:01
Hali ambayo umma wa Kiisilamu unaishi leo, miongoni mwa ugomvi na mapigano yaumwagaji damu, yanatilia mkazo na umuhimu wa kueneza utamaduni wa umoja, usamehevu na kukubali rai ya mwingine, kwani utamaduni ndio ambao unatengeneza tabia na mwenendo wake.
News ID: 298

"Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu na wala msifarakane na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu juu yenu ambapo mlikuwa maadui, naye akaziunganisha nyoyo zenu, hivyo kwa neema yake mkawa ndugu."

Kati ya mafanikio makubwa ya mtukufu nabii Muhammad (s.a.w.w) ni kuisafisha jamii hio yenye kupigana na kuinusuru kutokana na vurugu za kikabila kikoo hata za kiupotevu wa imani, na kuipeleka kwenye uelewano na udugu ujamaa nakuondoa khitilafu zao za hapo kabla, nayo ni kati ya neema kubwa sana za mwenyezi mungu Mtukufu kwa waja wake katika jamii yoyote ile.

Pamoja na kutofautiana fikra na kutofautiana daraja au kutofautiana uchumi nasaba au imani baina ya Waisilamu bado Mwenyezi Mungu Mtukufu anaelekeza mazungumzo kwa wote, nao ni wajibu ambao Waisilamu wa leo wanapaswa kuutambua, kwani tofauti ya kifikra haizuii kuishikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu mtukufu.

Hali ambayo umma wa Kiisilamu unaishi leo, miongoni mwa ugomvi na mapigano yaumwagaji damu, yanatilia mkazo na umuhimu wa kueneza utamaduni wa umoja, usamehevu na kukubali rai ya mwingine, kwani utamaduni ndio ambao unatengeneza tabia na mwenendo wake.

Kuwepo kwa khitilafu katika ufafanuzi wa kiitikadi na kifiqihi haizuii kutengeneza jamii moja inayotuunganisha pamoja kwani sote ni wana wa Adam na mama yetu Hawa, hivyo twaweza kutengeneza jamii moja inayo tawaliwa na uelewano na upendo.

NINI VIKWAZO VYA UMOJA NA UVUMILIVU KATIKA JAMII ?

1. Elimu duni.

2. ushauri mbovu unao tolewa na wanazuoni.

3. Vishawishi katika kujipatia kipato cha haraka.

4. Kupandikizwa chuki kwa ajili ya kujitafutia wafuasi nk.

NAMNA GANI TUTAWEZA KULETA HALI YA UMVUMILIVU NA KUISAMBAZA?

1. Kuelimisha jamii elimu sahihi ya mtukufu mtume (s w w) na Alul-bayti zake.

2. Kuilea jamii kwa kuipa tabia njema.

3. Kutoa mbinu mbali mbali katika kukabiliana na chuki za kupandikizwa.

4. Kukuza kipato katika jamii ili kuwakinga kutokana na hali ngumu ya kimaisha, kufanya hivyo itaiepusha jamii na kuingia katika kushawishiwa na vijipesa. Nk.

WABILLAAH TAUFIIQI.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: