bayyinaat

Published time: 19 ,April ,2018      12:09:16
Enyi watu hakika sisi tumewaumba kutokana na mwanaume na mwanamke na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane, hakika mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu zaidi, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua, mwenye habari."
News ID: 299

Enyi watu hakika sisi tumewaumba kutokana na mwanaume na mwanamke na tumewafanya mataifa na makabila ili mjuane, hakika mtukufu wenu zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu ni mchamungu wenu zaidi, hakika Mwenyezi Mungu ni mwenye kujua, mwenye habari."  Suratu hujrat aya 13.

Ujumbe wa Kiisilamu ni kwa watu wote. "Enyi watu," unawalingania kujuana na kupuuza mfarakano, na kuwakumbusha asili ya uwepo wa ushirikiano (tumewaumba mwanaume na mwanamke). Na kisha ni wito kwa Waisilamu wa leo kubeba ujumbe wa amani kwa ulimwengu mzima yaani pembe za dunia.

Anasema Imamu Ali (a.s.): Watu wako aina mbili: Ama ni ndugu yako katika dini au ni mwenzako katika maumbile." Na katibu mkuu wa zamani wa umoja wa mataifa alisema:" Ibara hii ni ni wajibu itundikwe katika kila taasisi, nayo ni ibara inayopaswa kuheshimiwa na binadamu wote ulimwenguni." KUJUANA INACHUKUA UHALISIA WAKE KATIKA PANDE MBILI:

1. Upande wa kibinadamu na kijamii

2.Upande wa kielimu na wa kimaendeleo.

Na hii inahitaji mkusanyiko wa sifa za kibinadamu na ratiba ya kielimu.

Na ikiwa dini yetu ina upana huu inapendeza kiasi hiki kwa nini tunaishi katika mfarakano, mizozo na hitilafu ndogo ndogo?

Hakika kutafakari katika aya za Quran Tukufu inatudhihirishia tofauti kubwa iliyopo baina ya ukweli wa Uisilamu na vitendo vya Waisilamu wenyewe.

Walhamdu lillahi rabbil-aalamiina.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: