bayyinaat

Published time: 21 ,April ,2018      21:46:48
Kila mara mahusiano ya watu yanapoambatana na utambuzi na weledi huu na kuweko hali ya kudirikiana, basi, mahusiano ya kijamii huwa yenye uelewa na ufahamu na hivyo
News ID: 300

Mahusiano ya watu katika jamii ndogo yaani familia, na jamii kubwa yaani miji na nchi yanapaswa kuwa kwa mujibu wa ufahamu na utambuzi, thamani, utukufu wa wanadamu, kutambua haki zao na kuelewa taklifu (majukumu) mkabala wao.

Kila mara mahusiano ya watu yanapoambatana na utambuzi na weledi huu na kuweko hali ya kudirikiana, basi, mahusiano ya kijamii huwa yenye uelewa na ufahamu na hivyo mafungamano ya kijamii huwa imara na yasiyoweza kutetereka na kusambaratika.

Jamii ambayo ina sifa hizi zote za mtu binafsi huondokea na huwa kitu kimoja na huwa kama kizingiti cha imara cha chuma mkabala na tukio lolote.

Umoja wa watu wenye uelewa, harakati zilizo ratibiwa ,zenye kuleta ukamilifu wa kijamii na watu, yote hayo yanafungamana na ufahamu na uelewa. Elimu, uelewa, ufahamu na muono wa mbali huwafanya watu kuwa katika sura kamili na ya daima na hali hiyo huwafikisha watu katika malengo makuu.

Katika jamii ndogo ya familia vile vile, kama kuta kuwepo na ufahamu wenye misingi na wenye pande mbili na kila mmoja kati ya wanandoa, akawa ni mwenye kutambua vyema thamani za kibinadamu na haki za mwenzake, familia huwa ni yenye kudumu na huwa mbali na hali ya kusambaratika.

Bila shaka mahusiano ni jambo muhimu saana katika jamii:


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: