bayyinaat

Published time: 21 ,April ,2018      21:51:23
Wakati watu watakapo fanya mambo walio katazwa na kila mtu akafanya kila alitakalo, bila ya mtu kuwa na usimamizi (katika hali kama hii)
News ID: 301

Ni vyema hapa tuanze na maneno ya Imamu Ridhaa (a.s). Anasema:

Wakati watu watakapo fanya mambo walio katazwa na kila mtu akafanya kila alitakalo, bila ya mtu kuwa na usimamizi (katika hali kama hii)

watu wote watakumbwa na maovu na ufisadi. katika kazi binafsi na vikundi, mtu anapaswa kukubali misingi na vigezo na akubali haki, na ili yeye asiingie katika maovu na kuangamia na katika hali kama hii, jamii haitaingia katika hali ya shaghalabaghala na wala haitokumbwa na kusambaratika.

Katika kiwango cha maisha ya mtu binafsi kunakazi nyingi, miamala, matakwa, mielekeo, vipato, kugharamika na utumiaji vitu na kadhalika......kama hakutakuwepo na mipaka, mtu hupoteza uzima wake (wa kiafya labda aangalie vizuri) kutokana na kufanya mambo kwa kuchupa mipaka na hatimaye jambo hilo humpelekea katika kuangamia.

Katika kiwango cha jamii na mahusiano na watu wengine, jambo la dharura na asili ni kutambua mipaka (sheria). Kwani wanadamu katika jamii hukabiliana na makatazo mengi (sheria) ambayo ni lazima kuyaheshimu na wanapaswa kuyapokea na kuyakubali makatazo hayo kwa uwepo wao wote.

Kuanzia wa kwanza hadi wa juu kabisa ni haki za watu wengine ambapo haki hizo zinapaswa kupewa kipaumbele mbele ya haki na matakwa pamoja na mielekeo binafsi na hivyo jambo hilo kumzuia mtu kufanya kila kazi au kufuata kila njia aitakayo (pasi na mpaka). Hii itamzuia muhusika kukanyaga na kupora haki za wengine. Kwa msingi huo basi, uhuru wote unawekewa mipaka katika uhuru na haki za jamii. Hii ina maana kwamba, mtu haruhusiwi kufanya jambo litakalo pelekea kukeuka uhuru wa wengine katika jamii au kukanyaga haki za watu wengine katika jamii anayoishi.

Hapa ndipo unapopatikana udharura wa nafsi ya tawala na serikali ambayo huzuia uvamizi na ukiukwaji wa haki za watu wengine, serikali au utawala hudhibiti kufanya mambo na miamala kwa matakwa ya watu. Utawala hapa huwa na jukumu la kuingilia kati na kulinda haki za Watu katika jamii.

Hivyo basi kupitia maneno haya ya hekima ya Imamu Ridhaa (a.s), mwanadamu anapaswa katika harakati zake za kiuchumi, kisiasa, kitamaduni na hata katika miamala yake binafsi anapaswa kuheshimu sheria na kanuni, ajitenge mbali na kiburi, kufanya mambo kama anavyotaka yeye na kujiepusha na kutaka makuu.

Ili kwa njia hio jamii iweze kufikia katika ustawi na hivyo haki na uhuru wa kimantiki uweze kupatikana. Kwa kuwa maisha yetu yanategemea kustawi kwa kulinda na kufuata sheria basi ni lazima tuishi kwa kuchunga mipaka ili jamii isalimike kutokana na sheria hizo. Wabillah taufiqi


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: