bayyinaat

Published time: 21 ,April ,2018      23:14:03
Na hivyo ndivyo dini yetu yatufundisha na kutuasa, kwani hakuna maisha, ima katika kumjua mungu au katika kuishi na watu pasina kutekeleza muamala na watu wenzio
News ID: 302


امام رضا (ع) قال رسول الله (ص) راس العقل بعد الايمان بالله، التود الى الناس، و صنع الخير الى كل بر و فاجر (ايون اخبار ال-رضا ج/35.

Imamu Ridhaa (a.s) amenukuu kutoka kwa mtukufu mtume (s.w.w.w) yakwamba amesema:

Kilele cha akili( busara) baada ya kumuamini Mwenyezi Mungu nikufanya urafiki na watu na kumtendea wema kila mtu, awe mwema au mwovu.

Na hivyo ndivyo dini yetu yatufundisha na kutuasa, kwani hakuna maisha, ima katika kumjua mungu au katika kuishi na watu pasina kutekeleza muamala na watu wenzio. Ingawa wapo wenye kujitenga lakini mwisho wa siku lazima atawahitajia watu au atamuhitajia Mwenyezi mungu katika haja zake.

Muamala wa kiutu kwa binadamu na raia wote ni katika mafundisho ya imamu Ridhaa (a.s). Watu wema au waovu, wawe watu wazuri na wenye kutambua majukumu yao na kufungamana nayo au wawe ni watu ambao si wenye kujifunga na mambo na sio watu wema na wazuri, mtu anapaswa kuamiliana nao kwa muamala wa kiutu na kibinadamu.

Kwa maana kwamba muamala wa mtu kwa mtu mwema na mwovu unapaswa kua muamala wa kiutu na wa kibinadamu na muamala wa aina moja.

Katika mahusiano kama hayo mwanadamu anapaswa kuthibitisha ubinadamu wake na aamiliane na watu wote kwa msingi wa ubinadamu na utu; kwamaana kwamba, kigezo cha muamala na watu wengine na mtindo wa tabia za kijamii kinapaswa kuwa kusita kuamiliana kwa wema na watu wengine eti kwa sababu tu watu hao ni waovu na wamepotoka. Ni bora kuamiliana na watu kwa muamala wa kiutu na kibinadamu kwani asaa kupitia muamala huo mzuri watu hao wakazinduka kutoka katika mghafala na hivyo kuwafanya wabadilike na kuwa watu wema.

Kwani hilo linaweza kuwasaidia na kuwafanya wagundue makosa yao na hilo linaweza kuwa funzo la msingi wa utu na hivyo kuwa chanzo cha kuenea utu na ubinadamu.

Naye imamu Hussein (a.s) kazi ya kiutu na kibinadamu imeshabihiswa na umande wakati wa msimu wa machipuo, ambao huenea katika ardhi yote na kutoacha sehemu ambayo halijafikiwa na tone lake.

Imamu Hussein (a.s):

قال عند رجل:

ان المعروف اذا اسند الى غير اهله ضاع. فقال(ع): ليس كذلك ولكن تكون الصنيعة مثل وابل المطر تصيب ابر والفاجر (تحاف العقول 175 )

Kila mara kazi ya kibinadamu wanapopewa watu wasio husika (wasiostahili) basi kazi hio huharibika. Imamu Hussein (a.s) baada ya kusikia kauli hio akamwambia bwana yule: Hivyo sivyo, bali kazi ya kiutu na nzuri ni kama matone makubwa ya mvua (na umande wa machipuo) ambayo humdondokea mtu mbaya na mwema.

Hali halisi ya maneno haya yachomayo nyoyo, ni maneno ya kuzingatiwa na kufanyiwa kazi kwani hivi ndivyo tunavyoshuhudia mambo yakienda mrama katika jamii zetu.

Wengi huingia katika majukumu pasina kujua nini walifanyalo, hatimaye hujikuta wakitoa maamuzi au fatuwa kwa msukumo wa nyoyo zao. Allah atujaalie tuwe wenye kuamiliana kwa kufuata utu.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: