bayyinaat

Published time: 21 ,April ,2018      23:23:55
Ndugu kwa njia moja au nyingine anayo nafasi kwa nduguye hivyo kiubinadamu haifai kumbeza, kumtelekeza, kwani yeye ni nduguyo tu
News ID: 303


Bila shaka sote twafahamu ndugu ninani na ana nafasi gani kwetu. Ndugu kama ndugu ana nafasi muhimu sana kwetu, na kwa kila mmoja kwa nafasi yake anapaswa kufahamu kuwa anayo masuulia kwa ndugu yake, bila kujali ndugu huyo ni mwenye imani sawa na aliyo nayo yeye au la.

Ndugu kwa njia moja au nyingine anayo nafasi kwa nduguye hivyo kiubinadamu haifai kumbeza, kumtelekeza, kwani yeye ni nduguyo tu.

Na jambo hili mitume, maimamu wametuasa sana juu ya udugu hivyo si jambo la kubezwa au kupuuzwa kiasi hicho.

Naye Imamu Ridhaa (a.s):

Anasema Tambua kwamba....Haki za ndugu ni wajibu na faradhi.....Fanya hima kwa kutumia nafsi na mali yako kwa ajili yao na kila katika lile ambalo linajuzu kufanya usawa, basi amiliana nao kwa usawa.

Kwa kauli hio ni vema kufahamu kua familia ina nafasi ya pekee kwa mujibu wa maneno ya Imamu,

Baada ya majukumu na masuulia, aliyonayo mtu kwa Mwenyezi Mungu, Mtume (s.a.w.w) na viongozi, jukumu kubwa na la juu zaidi ( baada ya hayo) ni jukumu lake kwa ndugu zake(ambao ni binadamu wenzake) na ndugu zake katika imani. Kutekeleza haki za ndugu ni chimbuko kuu la itikadi juu ya mwenyezi mungu. Asili ya udugu katika Uisilamu imekuja katika Qur-ani tukufu:

HAKIKA WAUMINI NI NDUGU, BASI PATANISHENI BAINA YA NDUGU ZENU.....

Katika hadithi za mtukufu mtume (s.a.w.w.) maimamu watoharifu (a.s) na kadhalika....jambo hili limetiliwa mkazo na kusisitizwa sana.

Imamu Sadiq (a.s) anabainisha jinsi uhusiano wa kidugu unavo paswa kuwa maneno ambayo yanaendana na maneno ya hekima ya Imamu Ridhaa (a.s).

Imamu Sadiq (a.s):

anasema.

Hapana naapa kwa mola! Katu muumini hawi muumini mpaka awe kama mwili wake: kama mshipa utapata dharuba, basi mishipa yake mingine nayo ihisi dharuba hio na maumivu (ish-takie kwa maumivu). Moja ya mshairi mashuhuri wa Kiirani akiistafidi na hadithi hizi ametunga shairi lake ambalo limetokea kuwa mashuhuri ulimwenguni:

Madhumuni ya maneno ya shairi hili ni kwamba: Wanadamu (baina yao) ni kama viungo vya mwili mmoja.

Maana yake ni kwamba mwili ukiungana, kisha kiungo kimoja kikapatwa na maumivu yale maumivu husambaa mwili mzima, hii ni wazi kua viungo hivyo vina mawasiliano ya pamoja na kwa ukaribu zaidi.

Hivyo hivyo waumini wanatakiwa wawe kama viungo vya mwili wa mwanadamu, ili muumini akipatwa na tatizo basi ionekane tatizo hilo ni la waumini wote popote walipo ndani ya Ulimwengu huu. Kwa mfano ikiwa huyu ataonewa basi wasimame na kumuhami kwani wote ni kitu kimoja.

au ikiwa maafa yamemkuta huyu basi wengine wahakikishe wanasimama kidete katika kulisimamia na kulimaliza, bila kujali ninani, kwani ile nembo kuu ambayo ni udugu inatosha kufanya kazi popote pale.

Lakini leo hii imekua kinyume kabisa na hali hio utasikia anae uwa husema Allahu Akbaru, na anaye uliwa naye husema hivyo hivyo yaani Allahu Akbaru.

Msiba mkubwa huo Allah atustiri na hali hio.

wabillahi taufiiqi:


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: