bayyinaat

Published time: 22 ,April ,2018      20:23:33
News ID: 305

Rais wa nchi ya Korea Kaskazini Bw Kim Jong Un, ameeleza kwamba si katika lengo lake kuja kuwa mfano wa Saddam Hussein au Muammar Gaddaf ambao walikuwa ni watawala wa nchi mbili za Iraq na Libya.

Akizungumza na kiongozi wa Korea Kusini Bw Moon Jae In, amesema kwamba jambo la kusimamia kile ambacho unaamini kwamba ndio sahihi si zuri kwa maslahi ya taifa, na ndio maana ameamua kuweka mazungumzo na Marekani kunako swala la kuachana na Nyuklia pamoja na majaribio ya silaha za kemikali hizo.

Mapema mwezi huu mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Bi Nikki Halley, alinukuliwa akisema kwamba Korea Kaskazini kupitia Raisi wake imekuwa ni mfano mzuri kufuatia kusoma kwao mazingira na kuamua kuchukua uamuzi sahihi.

"......Korea waliangalia makubaliano ya Iran na Mataifa sita, kisha kuangalia nini kimetokea baada ya makubaliano hayo, pia imekuwa wazi kwamba ni nyakati gani ambazo anaweza kupitia, jambo ambalo sisi hatupendi litokee tena” alinukuliwa Nikki Halley.

Rais Kim Jong Un anatarajiwa kukutana na Rais Donald Trump ikiwa ni katika harakati za kuzungumzia kunako kusimamisha majaribio ya makombora ya Nyuklia.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: