bayyinaat

Published time: 22 ,April ,2018      20:25:16
News ID: 306

Katika hali ambayo Rais wa Marekani Bw Donald Trump akiamini kwamba makubaliano yaliyojiri baina ya Iran na nchi sita zenye nguvu ni makubaliano mabaya kutokea katika uso wa ardhi, Rais wa Ufaransa Bw Emmanuel Macron ameibuka na kusema kwamba hakuna njia mbadala ya kukimbia makubaliano hayo zaidi ya kukubaliana nayo.

Katika makubaliano hayo nchi hizo ziliafikiana kwamba Iran iachane na matumizi ya Nyuklia ili iweze kuondolewa vikwazo vya biashara na Marekani, jambo ambalo Trump anasema mpka kufikia Mei 12 itajulikana kama bado analiendeleza au la.

Rais Macron ambaye anatarajia kukutana na Rais Trump katika kujadili kunako hali ya nchini Syria, amedokeza kwamba Marekani haitakiwi kutoa majeshi yake kwa sasa, kwani kufanya kwao hivyo kutawapa mwanya wasaidizi wa Bashar Al Asad hasa Iran katika kutawala nchi hiyo kijeshi.

Trump ambaye alitangaza kutaka kurejesha majeshi yake haraka iwezekanavyo baada ya kuamini kwamba kazi ya kusambaratisha vikundi vya kigaidi imekamilika.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: