bayyinaat

Published time: 04 ,May ,2018      18:10:13
News ID: 309

Zikiwa zimesalia siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa Wabunge nchini Iraq, maulama mbalimbali wameashiria kunako umuhimu wa uchaguzi huo pamoja na kutoa nasaha mbalimbali kwa wananchi.

Miongoni mwa maulama hao ni Kiongozi Mkuu wa Wanazuoni wa Kishia nchini humo Ayatollah Ally Sistani, ambaye katika hotuba yake iliyowasilishwa na moja ya manaibu wake, ameelezea kwamba Wananchi wa Iraq wanatakiwa kuwa makini katika kutoruhusu mafisadi kushika hatamu ya nchi kwa mara nyingine, hasa baada ya kuona namna gani walivyofeli hapo awali.

"....Tumeona katika chaguzi zilizopita, ambapo wengi wao walichaguliwa kushika nyadhifa za juu Serikalini, lakini walitumia vibaya nyadhifa hizo katika Ufisadi na matumizi mabaya ya mali za uma...” Ilisema sehemu ya Ripoti hiyo.

Aidha katika ripoti hiyo pia aliashiria kunako umuhimu wa nchi ya Iraq kuhakikisha kwamba hakuna nchi nyingine yeyote ambayo itatia mkono wake katika uchaguzi huo, bila ya kutaja ni nchi zipi ambazo anazikusudia.

Wananchi wa Iraq wanatarajia kushiriki katika uchaguzi mkuu wa Wabunge nchini humo mnamo May 12 mwaka huu, huku kukiwa na hamasa kubwa sana ukizingatia ndio uchaguzi ambao utamtoa Waziri Mkuu atakayekuwa na dhamana ya kuijenga Iraq mpaya baada ya kuwa katika kipindi cha vita.

Mji wa Baghdad peke yake unakadiriwa kuhitaji kiasi cha Dola za Kimarekani Bilioni 100, ili kuweza kurejesha tena majumba, maofisi pamoja na miundo mbinu iliyoharibiwa vibaya.

Rushwa pamoja na ufisadi nchini humo vinatajwa kuwa ni kizuizi kikubwa sana katika kuijenga Iraq mpya, na ndio maana wananchi wanashauriwa wasifanye makosa katika Uchaguzi huu.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: