bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      10:50:11
Moja ya vigawanyo vya madhambi makubwa ni kudharau wazazi wawili na hakika Mtume na Imam Ali na Imam Sadiq na Imam Ridhaa na Imam Jawadi wote wamebainisha kwa uwazi ukubwa wa dhambi katika riwaya zilizonukuliwa kutoka kwa katika idadi ya madhambi ya makubwa.............
News ID: 319

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Moja ya vigawanyo vya madhambi makubwa ni kudharau wazazi wawili na hakika Mtume na Imam Ali na Imam Sadiq na Imam Ridhaa na Imam Jawadi wote wamebainisha kwa uwazi ukubwa wa dhambi katika riwaya zilizonukuliwa kutoka kwa katika idadi ya madhambi ya makubwa, bali imekuja kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) aliposema: Moja ya madhambi makubwa ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na kudharau wazazi wawili. Na hiyo ni katika madhambi yalipokelewa ndani ya Qur’ani na hadithi sahihi kuwa adhabu yake ni kali mno siku ya kiama.

Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu ndani ya Qur’ani akisimulia kisa kwa ulimi wa Issa bin Maryam (a.s):

"وَبَرًّا بِوَالِدَتِي وَلَمْ يجْعَلْنِي جَبَّارًا شَقِيا".

"Na nimtendee wema mama yangu. Wala hakunifanya niwe jeuri, mwovu”.[1] Na sababu ya kuwa kwanini hakumtaja Baba yake ni kwa kuwa Nabii Issa hakuwa na baba. Kwa minajili hii Mwenyezi Mungu akaleta kabla hiyo kwa kumtaja Baba na Mama pamoja katika ambayo anaikumbusha kisa cha Yahya (a.s):

" وَبَرًّا بِوَالِدَيهِ وَلَمْ يكُنْ جَبَّارًا عَصِيا".

"Na akawa mwema kwa wazazi wake, wala hakuwa jabari mua'si”.[2] Na hakika ameelezea kwa ufasaha ndani ya Aya mbili hizi tukufu kuwatendea wema wazazi wawili kwa sifa aina tatu:

Jeuri, mwovu na muasi, na moja ya sifa hizo Mwenyezi Mungu ameahidi adhabu iumizayo na kali, aliposema kuhusu tabia ya ujeuri:

" وَخَابَ كُلُّ جَبَّارٍ عَنِيدٍ. مِنْ وَرَائِهِ جَهَنَّمُ وَيسْقَى مِنْ مَاءٍ صَدِيدٍ. يتَجَرَّعُهُ وَلَا يكَادُ يسِيغُهُ وَيأْتِيهِ الْمَوْتُ مِنْ كُلِّ مَكَانٍ وَمَا هُوَ بِمَيتٍ وَمِنْ وَرَائِهِ عَذَابٌ غَلِيظٌ".

"na akashindwa kila jabari mkaidi. Ambaye nyuma yake ipo Jahanamu, na atanyweshwa maji ya usaha. Awe anayagugumia, wala hawezi kuyameza. Na mauti yawe yanamjia kutoka kila upande, naye wala hafi. Na zaidi ya hayo ipo adhabu nyengine kali vilevile”.[3]

Na anasema (s.w.t) katika wasifu wa uovu:

" فَأَمَّا الَّذِينَ شَقُوا فَفِي النَّارِ لَهُمْ فِيهَا زَفِيرٌ وَشَهِيقٌ. خَالِدِينَ فِيهَا مَا دَامَتِ السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ إِلَّا مَا شَاءَ رَبُّكَ إِنَّ رَبَّكَ فَعَّالٌ لِمَا يرِيدُ".

"Ama wale wa mashakani hao watakuwamo Motoni wakiyayatika na kukoroma. Watadumu humo muda wa kudumu mbingu na ardhi, isipo kuwa apendavyo Mola wako Mlezi. Hakika Mola wako Mlezi hutenda apendavyo”.[4] Na anasema tena kuhusu muasi:

" وَمَنْ يعْصِ اللَّهَ وَرَسُولَهُ وَيتَعَدَّ حُدُودَهُ يدْخِلْهُ نَارًا خَالِدًا فِيهَا وَلَهُ عَذَابٌ مُهِينٌ".

"Na anaye muasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na akaipindukia mipaka yake, (Mwenyezi Mungu) atamtia Motoni adumu humo, na atapata adhabu ya kudhalilisha”.[5]

KUDHARAU WAZAZI WAWILI KWA MUJIBU WA HADITHI:

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): Jiepusheni na kudharau wazazi kwani harufu ya pepo inapatikana katika njia yenye umbali wa miaka elfu moja na kamwe haipati harufu hiyo kwa mwenye kudharau wazazi wake na mkata udugu.[6]

Aidha kutoka kwake (s.a.w.w): Yeyote mwenye kuwakasirisha wazazi wawili hakika amemuudhi Mwenyezi Mungu na mwenye kuwaghadhibisha hakika amemughadhibisha yeye.[7]

Vilevile kutoka kwa Mtume (s.a.w.w): Na atende amali yoyote mwenye kuasi wazazi wake wawili kamwe hatoingia peponi.[8]

Itaendelea.......



[1] Surat Maryam, Aya 32.

[2] Surat Maryam, Aya 14.

[3] Surat al- Ibrahim, Aya 15 – 17.

[4] Surat Hud, Aya 106 – 107.

[5] Surat al- Nisaai, Aya 14.

[6] Al- Kafiy, juz 2, uk 349, mlango; al- U’quuq, hadithi 6.

[7] Al- mustadrak, juz 15, uk 193, mlango wa 75, hadithi 18.

[8] Al- mustadrak, juz 15, uk 196, mlango wa 75, hadithi 35.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: