bayyinaat

Published time: 05 ,March ,2017      22:43:39
Bibi Fatima (as) alizaliwa siku ya Ijumaa Jamadil Akhir mwaka wa tano kabla ya Utume, wakati ule Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) alipofanikiwa kuwaepusha Makureishi na vita vikali viliyotaka kuzuka baina yao walipokuwa .........
News ID: 32

Kuzaliwa na kukuwa kwake

Jina lake ni Fatima (as) binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww), na mama yake ni Bibi Khadija binti Khuwaylid (Radhiya Llahu anha) mke wa mwanzo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) na mwanamke wa mwanzo kusilimu.

Juu ya kuwa riwaya nyingi zinasema kuwa huyu ndiye mdogo wa ndugu zake wote, lakini ziporiwaya zinazosema kuwa Ummu Kulthum (Radhiya Llahu anha) ndiye mdogo wao.

Fatima (as) ni mke wa Imamu Ally bin Abi Talib (as) Khalifa wa kwanza wa Waislamu, na mama wa Al Hassan na Al Hussein (as) mabwana wa vijana wa Peponi.

Bibi Fatima (as) alizaliwa siku ya Ijumaa Jamadil Akhir mwakawatano kabla ya Utume, wakati ule Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) alipofanikiwa kuwaepusha Makureishi na vita vikali viliyotaka kuzuka bainayaowalipokuwa wakiujenga upya msikiti wa Al Kaaba, na kila kabila likataka kupewa heshima ya kulirudisha jiwe jeusi mahali pake.

Makureshi waliridhikanauamuzi alioutoa Muhammad (Saww), uamuzi ulioweza kuwaepusha na vita vikubwa vilivyotaka kuzuka bainayao.

Ndani ya siku zile alizaliwa Bibi Fatima (as) na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) alimbeba binti yake huyo akiwa na furaha kubwa, na furaha ya Bi Khadija (Radhiya Llahu anha) ilikuwa kubwa zaidi alipomuona binti yake huyo akishabihiana sana na Mtume wa Mwenyezi Mungu ((Saww).

Imepokelewa kuwa Bibi Aisha alisema:

"Uso wa Fatima binti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ulikuwa umeshabihiana sana na uso wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) kupita mtu yoyote mwingine."

Na kutoka kwake pia alisema:

"Sikupata kukiona kiumbe cha Mwenyezi Mungu kilichoshabihianasanana Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) kupitaFatima."

Na imepokelewanaAddaylamiy kutoka kwa Abu Hurairah kuwa alimsikia Imamu Ally (as) akisema:

"Amepewa jinalaFatimakwa sababu Mwenyezi Mungu amemtenga mbali na moto."

Neno 'Fatm', ambaloniasili ya neno 'Fatima', maana yake ni kutenga.

Fatima (as) alilelewa ndani ya nyumba ya Utume, akapata mafundisho ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww), na kwa ajili hiyo alikuwa mwanamke aliyeikinai dunia, mwingi wa kuona haya na alikuwa na kila sifa na mwenendo na tabia njema alizonazo baba yake ((Saww).

Alipofikia umriwamiaka mitano, mabadiliko makubwa yalikuwa yakitokea wakati baba yake alipoanza kupata wahyi kutoka kwa Mola wake Subhanahu wa Taala, akashuhudia namna baba yake alivyokuwa akifanyiwa vitimbi na hila mbalimbali na Makureishi huku wakimhujumu na kujaribu kutaka kumdhuru.

Katika maovu makubwa aliyopata kuyaonanisiku ile Uqbah bin Abu Muiyt alipotupa taka juu ya kichwa cha baba yake aliyekuwa amesujudu mbele ya uwanja wa Al Kaaba. MtumewaMwenyezi Mungu (Saww) aliendelea kusujudu na hakuinua kichwa chake mpaka alipokuja BibiFatima(as) na kuondoa taka zile.

Na katika wakati mgumu alioishi ndani yakenizile siku za mwanzo za kulingania watu, wakati Waislamu walipopigwa pande na makafiri na kuzungukwa wakiwa katika bondela Bani Hashimmuda wa miaka mitatu bila kupelekewa chakula. Na Bibi Fatima (as) alikuwa akiwaona Waislamu wakiwa katika shidananjaa hata ikawabidi kula majani na ngozi, na wakati mwingine kilikuwa kikiwafikia chakula kwa njia ya kufichwa tena kwa siri.

Juu ya kuwa shida ile iliathirisanasiha ya Bibi Fatima (as) aliyekuwa na umbo dhaifu tokea utotoni mwake, lakini pia ilimuongeza imani, ushujaa pamoja na ukuaji wa akili na fikra.

Mara baada ya shida hiyo kumalizika, Bibi Fatima (as) alijikuta katika huzuni kubwa kutokana na kifo cha mama yake Bi Khadija (as) kilichotokea katika mwaka uliokuja kujulikana kwa jina la mwaka wa huzuni, na ndani ya mwaka huohuo alifariki pia Abu Talib ami yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww).

Bibi Fatima (as) aliweza kuyastahamilia yote hayo, akasubiri na kusimama imara pamoja na baba yake huku akimshughulikia na kumsaidia katika kuliziba pengola Bibi Khadija (Radhiya Llahu anha), na kwa ajili hiyo alikuwa akijulikana kwa jina la 'Mama wa baba yake'.

Hijra yake

Wakatiwakuhama kwenda Madina ulipowadia, Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) aliondoka na kumuacha nyumbani kwake Imamu Ally (as) kwa ajili ya kurudisha amana za watu, na aliwaacha pia binti zakeFatimana Ummu Kulthum.

Siku tatu baadaye,nabaada ya kukamilisha shughuli za kurudisha amana za watu, Aly (as) naye pia akahamia Madina, lakiniFatimana Ummu Kulthum walibaki Makkah mpaka pale Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) alipotuma ujumbe kwenda kuwachukua.

Kuolewa kwake

Baada ya MtumewaMwenyezi Mungu (Saww) kumuoa Bibi Aisha, wengi kati ya masahaba wakubwa wakataka kumuoa Bibi Fatima (as) akiwemo Abubakar na Abdul Rahman bin Auf, lakini Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) kwa upole aliwakatalia wote hao.

Ally bin Abu Talib (as) alikuwa miongoni mwa waliotaka kumuoa Bibi Fatima (as), lakini kwa vile alikuwa mwingi wa kuona haya alishindwa kumkabili Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) mpaka pale baadhi ya watu wa Madina walipompa moyo na kumkumbusha daraja yake mbele ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww), ndipo alipopiga moyo konde na kuamua kwenda katika majlis ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) na kumsemesha.

Aly (as) alishindwa kusema chochote alipowasili mbele ya MtumewaMwenyezi Mungu (Saww), lakini Mtume (Saww) alifahamu kuwa Ally (as) ana haja na kwamba anaona haya kutamka. Akamuuliza:

"Ana haja gani mwanawaAbu Talib?"

Imamu Ali (as) akajibukwahaya nyingi:

"Nilimkumbuka Fatima bintiwaMtume wa Mwenyezi Mungu."

Mtume (Saww) akamwambia:

"Unakaribishwa wakati wowote."

Maneno hayo yalikipooza na kukituliza kifua cha Imamu Ally bin Abu Talib (as) maana alielewa vizuri kusudi lake, na hazikupita siku nyingi akapiga moyo konde na kumwendea tena Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) aliyemkubalia ombi lake, na ndoa ikafungwa, na mahari aliyolipa yalikuwa ngao aliyopewa zawadi na Mtume wa Mwenyezi Mungu (Saww) aliyoipata ngawira katika vita vya Badr.

MtumewaMwenyezi Mungu (Saww) akawaombea dua, akasema:

"Mola wangu wabariki wao na vibariki vizazi vyao."

Itaendelea....

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: