bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      11:11:08
Moja ya madhambi makubwa ambayo umekuja ushahidi wa wazi juu ya kuwa kwake ni ukubwa ni kula haramu kama ilivyokuja katika hadithi ya sheria ya Imam Ridhaa (a.s) katika kitabu U’yun al- akhbaar na aidha katika riwaya ya A’mash kutoka kwa Imam Sadiq (a.s), na Mwenyezi Mungu ameihesabu dhambi hii kuwa ni katika sifa za Wayahudi
News ID: 321

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Moja ya madhambi makubwa ambayo umekuja ushahidi wa wazi juu ya kuwa kwake ni ukubwa ni kula haramu kama ilivyokuja katika hadithi ya sheria ya Imam Ridhaa (a.s) katika kitabu U’yun al- akhbaar na aidha katika riwaya ya A’mash kutoka kwa Imam Sadiq (a.s), na Mwenyezi Mungu ameihesabu dhambi hii kuwa ni katika sifa za Wayahudi ndani ya Aya mbili katika Qur’ani tukufu:

"وَتَرَى كَثِيرًا مِنْهُمْ يسَارِعُونَ فِي الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يعْمَلُونَ. لَوْلَا ينْهَاهُمُ الرَّبَّانِيونَ وَالْأَحْبَارُ عَنْ قَوْلِهِمُ الْإِثْمَ وَأَكْلِهِمُ السُّحْتَ لَبِئْسَ مَا كَانُوا يصْنَعُونَ".

"Na utawaona wengi katika wao wanakimbilia kwenye dhambi, na uadui, na ulaji wao vya haramu. Ni maovu mno hayo wayatendayo!. Mbona hao wanazuoni na makuhani wao hawawakatazi maneno yao ya dhambi, na ulaji wao vya haramu? Ni maovu mno hayo wayafanyayo!”.[1]

Ulaji wa haramu unaohesabika kuwa ni katika madhambi makubwa ni kula mali ya haramu, na madhumuni ya kula mali ya haramu na matumizi ya moja kwa moja sawa iwe katika njia ya kula au kunywa, au kuvaa na maskani na kadhalika, au yamkini asitumie mali hizo lakini huzizuia kumfikia mlengwa, mambo yote hayo huhesabika kuwa ni moja ya ulaji wa haramu, kama ambavyo ilivyokuwa madhumuni kula mali za yatima na mali ya riba, ni haramu wa kila aina ya matumizi ya mali ya yatima na mali ya riba na si maalumu kwa njia ya kula au kunywa, pia ifahamike kuwa hakuna baraka katika ulaji wa mali ya haramu na hapana manufaa yoyote katika matumizi ndani yake, kwa ajili hii imeabiriwa ya kwamba ni uleule ulaji mbaya wa mali ya haramu ndani ya kitabu kitukufu, na mlaji wa mali ya haramu hujitangazia vita pamoja na Mwenyezi Mungu mtukufu na Mtume wake, kama vile mlaji wa riba, na baadhi ya wengine huhesabika katika hukumu ya ukafiri kama vile mlaji wa rushwa, kama ilivyopokelewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s):

Amesema (a.s): Kila kitu akipokeacho Imam ni haramu, na haramu imegawanyika katika mafungu mengi miongoni mwake na kile kipatikanacho katika matendo ya viongozi madhalimu, na miongoni mwake ni kiongozi jeuri aliyepindukia kwa uonevu, na mwovu zaidi aliyepindukia kwa uovu wake, na thamani ya pombe na mvinyo wenye kulevya, na riba baada ya kugundulika, na ama rushwa katika hukumu ni kumkufuru Mwenyezi Mungu mtukufu na Mtume wake (s.a.w.w).

Na imenukuliwa riwaya nyingine mfano wa madhumuni ya hii katika kitabu al- kafiy kutoka kwa Imam Baqir (a.s).

Na kutoka kwa Abuu Abdillah (a.s) amesema: Jambo la haramu ni mfano wa manunuzi au thamani au pesa ya mzoga, pesa ya nyama ya mbwa, na thamani ya pombe, na mahari ya mwonevu, na rushwa katika hukumu na malipo kwa kuhani.[2]

Yabainika katika madhumuni ya hadithi hizi ya kwamba kula mali ya haramu ni kosa, na uharamu na adhabu ya baadhi yake ni kali mno kuliko nyingine, na mbaya mno kuliko aina zote ni kula rushwa, kwani mlaji wa rushwa katika hukumu ni kafiri na amekwisha laaniwa na Nabii wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w).

VIGAWANYO VYA RUSHWA

Rushwa imegawanyika katika mafungu matatu: Rushwa katika nafasi ya hukumu, Rushwa kwa ajili ya kufikia jambo la haramu, na Rushwa kwa ajili ya kufikia jambo la halali.

Rushwa katika hukumu: ni mtu kutoa hongo kwa hakimu kwa ajili ya kutoa hukumu kwa masilahi ya mtoa rushwa, au amtetee ili kufikia haki yake, na hata akiwa ni mwenye kustahiki haki hiyo, na hakimu akamsimamia kwa kutetea masilahi yake mahakamani, na kama ambavyo kupokea rushwa na kuitumia kuwa ni haramu basi pia ni katika madhambi makubwa, kwani kutoa hongo pia ni haramu na Mwenyezi Mungu amekwisha mlaani mtoa rushwa na mpokeaji wake. Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Amemlaani Mwenyezi Mungu mtoaji rushwa na mpokeaji na wakili kati yao”.[3]

Amesema tena (s.a.w.w): Jiepusheni na rushwa kwani ni ukafiri halisi, na kamwe mtu wa rushwa hatoinusa harufu ya pepo.[4]

Kwa kuongea ni kwamba pamoja na kuwa rushwa inasaidia ufisadi na maovu, ndio endapo atatatizika na kukosa njia nyingine mbadala mbele yake basi hapana kizuizi kwa kufanya hivyo, hivyo inajuzu kwake kutoa rushwa ikiwa hana njia nyingine ili kufikia haki yake, na hata kama mpokeaji wake atahukumu kwa kula haramu, kama ambavyo wakili kati ya mtoa rushwa na mlaji wake huhukumiwa kwa hukumu ya kutenda haramu sawa iwe kiasi kidogo au kikubwa, hakika jambo hili ni haramu.

Na hapana tofauti pia katika iwe ni mali au keshi au milki au faida katika nyumba au duka na mfano wa mambo hayo au iwe ni kazi yoyote ile kama vile kumshonea hakimu nguo kwa anuani ya rushwa au hongo, au kumjengea nyumba, na wakati mwingine rushwa hushamili hata kauli za kumsifia hakimu kwa lengo la kukutetea, na hakuna shaka katika uharamu wa mambo hayo pamoja na vifungu vyake.

Itaendelea ....



[1] Surat al- maida, Aya 62 – 63.

[2] Al- wasaail, juz 12, uk 62, mlango wa 5, hadithi 5.

[3] Safinaat al- bihaar, juz 1, uk 523.

[4] Safinaat al- bihaar, juz 1, uk 523.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: