bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      11:16:43
Vigezo vya rushwa: Mali ambayo itolewayo kwa anuani ya zawadi au hadia au kipatanishi kwa lengo la rushwa, au kwa anuani za mali za wajibu kama vile khumsi na zaka kwa kusudio la rushwa jambo hili ni haramu hakika......
News ID: 322

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


ZAWADI, KHUSI NA SADAKA KWA ANUANI YA RUSHWA

Vigezo vya rushwa: Mali ambayo itolewayo kwa anuani ya zawadi au hadia au kipatanishi kwa lengo la rushwa, au kwa anuani za mali za wajibu kama vile khumsi na zaka kwa kusudio la rushwa jambo hili ni haramu hakika, na haizingatiwi kile alichokitoa kuwa ni khumsi au zaka bali yampasa kurudia kutoa tena kwani dhima yake itabakia kuwa ni wajibu kwake kutoa tena, kwani sharti ya kusihi ulipaji wa khumsi na zaka ni kukusudia kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu ambapo kwa kukusudia rushwa wajibu wake haujathibiti.

Anasema (s.a.w.w) katika hadithi tukufu anayozungumzia alama za kukaribia kiama kwamba; Itafikia zama itahalalishwa ndani yake rushwa kwa anuani ya zawadi.[1]

Aina ya pili ya rushwa, ni Mtu kumlipa hakimu dhalimu au maarufu kitu, au msimamizi wa mambo fulani ili amfanyie wizi na kumnyanganya mtu mwingine haki au kumpandikizia kosa mtu mwingi, hakika hapana shaka ya kwamba katika aina hii rushwa ni haramu pia, kama vile kifungu cha kwanza, na kula mali kwa batili kama asemavyo Mwenyezi Mungu katika Qur’ani tukufu:

" وَلَا تَأْكُلُوا أَمْوَالَكُمْ بَينَكُمْ بِالْبَاطِلِ وَتُدْلُوا بِهَا إِلَى الْحُكَّامِ لِتَأْكُلُوا فَرِيقًا مِنْ أَمْوَالِ النَّاسِ بِالْإِثْمِ وَأَنْتُمْ تَعْلَمُونَ".

"Wala msiliane mali zenu kwa baat'ili na kuzipeleka kwa mahakimu ili mpate kula sehemu ya mali ya watu kwa dhambi, na hali mnajua”.[2]

Mwenyezi Mungu anakataza Waislamu ndani ya Aya hii mambo aina mbili:

1. Kuacha kula mali isiyokuwa na njia ya ya kisheria kama vile wizi na usaliti au hiana.

2. Kuacha kulipa mahakimu na viongozi mali ili kuwanunua kwa lengo la kudhulumu mali ya watu kwa nguvu.

RUSHWA YA HALALI

Kifungu cha tatu cha Rushwa: Ni Mtu kumpa mwingine mali yake ili aweze kufikia haki yake au kuzuia balaa la dhulma linalomkabili, au kufikia lengo la halali, hii ni katika vifungu vya rushwa ya halali, ambapo imepokelewa katika hadithi sahihi kutoka kwa Muhammad bin Muslim kuwa amesema: Nilimuuliza Abuu Jaafar (a.s) kuhusu Mtu anayetoa rushwa ili kubadilishiwa nyumba yake na akaishi, akasema (a.s): Hapana tatizo.[3] Na si madhumu katika hadithi hii kuwa ni miliki binafsi, bali madhumuni yake ni nyumba za shurika au waqfu za umma kama vile msikitini au shuleni, na mfano wa hivyo.

Na muhtasari wa mazungumzo yote ni kwamba kutoa rushwa kwa ajili ya kuzuia dhulma na kufikia haki ni jambo linajuzu na sahihi, lakini rushwa kwa kuzuia haki ya wengine iliyokuwa katika dhima ni jambo la haramu.

ATHARI YA KULA HARAMU

Kula haramu huzuia baraka ya mali na imepokelewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) kuwa amesema:

"Yeyote atakayechuma mali pasina uhalali atashushiwa mamlaka ya jengo bovu, mchanga ua udongo na maji”.[4] (Mpaka afilisike) yaani mamlaka yatakayomfanya kuishi katika nyumba ya huzuni na kumaliza umri wake na mali yake katika mali na udongo ambao hautamfaa si hapa duniani wala akhera, na kana kwamba kipande cha ardhi hii kimekuwa ni askari jinamizi wa kumtahini na kupeperusha mali yake.

Na kula haramu huzuia kupokelea ibada za mja kama ilivyoelezwa katika vitabu mbalimbali na hadithi sahihi.

Kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): Litakapoingia tonge au chakula cha haramu ndani ya tumbo la mja watamlaani malaika wa mbingu na nchi.[5]

Na amesema pia (s.a.w.w): Hakika kufanya ibada pamoja na kula mali ya haramu ni mfano wa kujenga nyumba juu ya mchanga.[6]

DUA YA MLAJI HARAMU HAIPOKELEWI

Anasema (s.a.w.w): Yeyote alaye chakula cha haramu haitokubaliwa Sala yake kwa masiku arobaini, na hazitajibiwa dua zake kwa maasubuhi arobaini, na kila nyama iotao kwa kula haramu basi moto ni aulaa kuicho,a. na kwa hakika tonge moja la haramu huotesha nyama katika mwili wa mlaji haramu.[7]

Amesema tena (s.a.w.w): Yeyote apendaye kujibiwa dua zake basi aombe chakla na machumo ya halali.[8]

Na kutoka kwake (s.a.w.w): amesema kumwambia aliyemwambia ninapenda kupokelewa maombi yangu, alimjibu (s.a.w.w) kwa kusema: Safisha chakula chako, na kisiingie cha haramu katika tumbo lako.[9]

Na amesema (s.w.t) kumwambia Issa bin Maryam (a.s): "Sema kuwaambia madhali ya banii israil kwamba, musiniombe na ilihali haramu iko chini ya miguu yenu…”.[10]

MWIZI HUNYIMWA RIZIKI YA HALALI

Imepokelewa kuwa Amirul muuminin (a.s) siku moja aliingia msikini na akamwambia mtu: Nishikie kipando wangu huyu, mtu yule alishikilia lijamu yake, aliondoka na kuacha kipando pale, Alitoka Imam amirul muuminiin na ilihali ameshikilia dirhamu mbili mkononi mwake ili amlipe mtu aliyeshikilia lijamu ya kipando wake, alimkuta farasi wake amesimama bila kamba, alipanda na kuondoka, kisha akampa kijana wake dirhamu mbili akanunue lijamu nyingine, alimkuta kijana wa lijamu sokoni amekwisha uza kwa dirahmu mbili, Imam akasema: "Hakika mja hupoteza riziki yake ya halali kwa kukosa subira, na haitozidi zaidi kile alichokadiriwa”.[11]

----------------------



[1] Madhumuni ya riwaya.

[2] Surat al- Baqara, Aya 188.

[3] Al- wasaail, juz 12, uk 72, mlango 9, hadithi 4.

[4] Bihaar al- anwaar, juz 33. Safinaat al- bihaar, juz 1, uk 298.

[5] Safinaat al- bihaar, juz 1, uk 298.

[6] Safinaat al- bihaar, juz 1, uk 299.

[7] Safinaat al- bihaar, juz 1, uk 24.

[8] U’ddat al- Dai’, uk 139, fii man kaa yustajaab Dua’uhum.

[9] U’ddat al- Dai’, uk 139.

[10] U’ddat al- Dai’, uk 140.

[11] La aalaai al- akhbaar, uk 151.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: