bayyinaat

Published time: 19 ,September ,2018      11:40:28
Tunasema katika kulipembua jawabu ya kwamba, hakika maana ya Mwenyezi Mungu kumpandikizia mtawala dhalimu huyu ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hamzui yule ambaye anayetaka kuwadhulumu ........
News ID: 324

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


KUTOKEA NAKAMA YA DHALIMU KWA WANAWE HAIPINGANI NA UADILIFU:

Na itakapodaiwa kwamba ni ipi dhambi ya watoto wa dhalimu au watoto wa watoto wa dhalimu hadi kufikiwa na natija ya matendo ya baba yao au babu yao? Na kupatwa kwa dhulma aliyotenda dhalimu… hakika jambo hili hupingana na uadilifu wa Mwenyezi Mungu.

Tunasema katika kulipembua jawabu ya kwamba, hakika maana ya Mwenyezi Mungu kumpandikizia mtawala dhalimu huyu ni kwa sababu Mwenyezi Mungu hamzui yule ambaye anayetaka kuwadhulumu watoto wa dhalimu, kwa sababu Mwenyezi Mungu kuzuia dhulma kwa watoto ni sawa na kutoa utukufu na hisani kwa mzazi wao, na kwa kuwa mzazi amedhulumu mali ya yatima, hivyo hastahiki kupata utukufu na hiani hii.

Anasema Imam Sadiq (a.s): "Hulindwa watoto kwa wema wa baba zao, kama ambavyo Mwenyezi Mungu alivyolinda vijana wawili kwa wema wa wazazi wao wawili. Kama alivyosema (s.w.t) katika kitabu chake kitukufu

"وَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَينِ يتِيمَينِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنْزٌ لَهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَنْ يبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيسْتَخْرِجَا كَنْزَهُمَا رَحْمَةً مِنْ رَبِّكَوَأَمَّا الْجِدَارُ فَكَانَ لِغُلَامَينِ يتِيمَينِ فِي الْمَدِينَةِ وَكَانَ تَحْتَهُ كَنْزٌ لَهُمَا وَكَانَ أَبُوهُمَا صَالِحًا فَأَرَادَ رَبُّكَ أَنْ يبْلُغَا أَشُدَّهُمَا وَيسْتَخْرِجَا كَنْزَهُمَا رَحْمَةً مِنْ رَبِّكَ"

Na ama ukuta, huo ulikuwa ni wa vijana wawili mayatima kule mjini. Na chini yake ilikuwako hazina yao; na baba yao alikuwa ni mtu mwema. Basi Mola wako Mlezi alitaka wafikie utu uzima na wajitolee khazina yao wenyewe, kuwa ni rehema itokayo kwa Mola wako Mlezi”.

Hivyo basi, wema wa mzazi ni sababu ya Mwenyezi Mungu kuwalinda watoto, kama ambavyo ni sababu ya kuzuia wema huu kwa kuwa kwake dhalimu.

KIFO CHA MDAI NA WATOTO WADOGO:

Afapo mdai na akawa ni mwenye watoto wadogo, basi mdaiwa endapo hatotenda amali ambayo italingana na hisa ya watoto hao, hakika huhesabika kuwa ni mlaji wa mali za yatima, kwa sababu mali huhamia kwa warithi pindi afapo mzazi.

KUTENDEA HISANI YATIMA:

Kama ambavyo kumdhulumu yatima ni jambo lenye adhabu kali duniani na akhera, pia na kumtendea hisani yatima ni jambo lenye malipo mema duniani n akhera, hasa kumlinda na kumlea yatima huyo, na zimepokelewa riwaya tele kuhusu ukubwa na jambo hili ambapo tutaashiria baadhi yake:

Imepokelewa kutoka kwa Imam Sadiq (a.s) kuwa amesema: "Yeyote atakaye mlea yatima Mwenyezi Mungu amemuwajibishia pepo kama ambavyo alivyomuwajibishia moto wa jahannam mlaji wa mali yake”.

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): "Mimi na mlezi wa mayatima tutakuwa kama viwili hivi kwenye pepo atakapokutana na Mwenyezi Mungu, kisha (s.a.w.w) akaashiria vidole viwili (kidole cha shahada na kidole cha kati)”.

Na amesema tena (s.a.w.w): "Atakapolia yatima hutikisika enzi ya Mwenyezi Mungu kwa kilio chake kisha atasema Mwenyezi Mungu: Enyi malaika zangu, huyu si yatima ambaye baba yake amezikwa ardhini, watasema Malaika; Wewe ni mjuzi zaidi, atasema Mwenyezi Mungu: Enyi malaika wangu hakika ninashuhudia ya kwamba yeyote atakaye mnyamazisha yatima huyu na akamridhisha nitamridhia siku ya kiyama”.

Na katika athari ya kumgusa yatima kichwani kwake kwa mkono kwa kumhurumia, huepusha maradhi na kuzuia ugumu wa moyo kama ilivyoelezwa katika riwaya mbalimbali, na hadithi tele kuhusu maudhui hii, na tutosheke hapa kwa kiasi hiki.

.........................


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: