bayyinaat

Published time: 21 ,September ,2018      14:23:33
Katika mafunzo ya Maimamu watukufu kupata kuwa wao walikuwa ni mfano bora kwa familia zao! Kwa mienendo ya maisha katika familia zao. Kama anavyosimulia Salman Farsiy katika riwaya mbalimbali.......
News ID: 332

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Mkusanyiko uonekanao katika jamii na muamala kati ya familia (zilizoshamili katika jamii) huhesabika kuwa ni jambo muhimu mno. Familia yenye mafanikio katika jamii si ile inayoepukana tu na upande wa matatizo na hitilafu, la hasha. Bali kujua familia yenye mafanikio katika jamii; ni ile familia ambayo haitetereki wala kusambaratika inapotokea hitilafu ya aina yoyote ile kati yao, pia huwa mstari wa mbele kutafuta suluhu zinapotulia shaghala baghala za mikingamo, na hujirekebisha na tabia zisizofaa. Kwa kuongezea hilo ni kwamba, familia yenye mafanikio makubwa katika jamii kwa mujibu wa dini tukufu ya Kiislam, ni ile iliyokuwa na itikadi thabiti, pia uadilifu.

Katika mafunzo ya Maimamu watukufu kupata kuwa wao walikuwa ni mfano bora kwa familia zao! Kwa mienendo ya maisha katika familia zao. Kama anavyosimulia Salman Farsiy katika riwaya mbalimbali.

Vilevile tunakuta Maimamu hao walikuwa wakiheshimu familia zao na shakhsiya za Wake zao pia, katika sekta za kiuchumi, walikuwa wakizipa kipao mbele nadharia wake zao.

Tanbihi:

Ndugu msomaji wangu mpendwa; Ili tujaaliwe kuwa ni wenye familia kamilifu na yenye upendo kwa Qur’ani tukufu, ni lazima tuzingatie mwanzoni mwa fasili ya kwanza ya maisha yetu iwe ni fasili yenye utangulizi mzuri (Kuanzia wakati ule wa kuchagua mchumba bora, aliyepambika kwa sifa zilizotajwa ndani ya Kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu). Kwani kila jambo litokealo katika fasili ya kwanza ya maisha ya Mwanadamu ni lazima lilete taathira katika fasili ijayo, sawa liwe jambo zuri au baya. Hivyo ni lazima tujitahidi tuanze kurekebisha katika fasili ya kwanza ya maisha yetu, ili kuzipa nguvu fasili zijazo kwa uwezo wake Allah (s.w.t).

----------------------

Imekusanywa na:

Ndg: Juma. R. Kazingati.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: