bayyinaat

Published time: 21 ,September ,2018      16:03:00
Na katika maandishi yaliyomfikia Imam Sadiq (a.s), ameyajibu kwa kusema: “Hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha zinaa kwa sababu ya nakama ipatikayo ndani yake kwa machafuko mabaya zaidi kama...........
News ID: 334

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


KUHARIBIKA NASABA NA MALEZI YA MTOTO:

Na katika maandishi yaliyomfikia Imam Sadiq (a.s), ameyajibu kwa kusema: "Hakika Mwenyezi Mungu ameharamisha zinaa kwa sababu ya nakama ipatikayo ndani yake kwa machafuko mabaya zaidi kama vile kuua nafsi, na kupotea nasaba ya mwanadamu na kuacha malezi ya watoto na kubatilika hukumu za mirathi”.

KUTENDA ZINAA NA MWANAMKE MWENYE MUME:

Atakapozini na mwanamke mwenye mume adhabu yake itakuwa kali mno, kwani hududi za zinaa ni bakora mia moja, lakini hududi ya kutenda zinaa na mwanamke mwenye mume ni kifo kwa kupigwa mawe.

Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s): Watu aina tatu Mwenyezi Mungu hatozungumza nao siku ya kiama, na hatowatakasa na wanayo adhabu kali iumizayo, miongoni mwao ni mwanamke anayefanya zinaa kitandani kwa mumewe.

Na kutoka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) amesema: "Yeyote atendao uovu na mwanamke mwenye mume utabubujika katika tupu yake uji wa chuma cha moto wa jahanamu sawa na uwanja ambao mwendo wake ni miaka mia tano, wataudhika watu wa jahanamu kwa ubaya wa harufu na watakuwa katika watu wenye adhabu kali mno”.

TAHADHARI:

Hakika zinaa ni sababu ya maovu mengi na mapungufu ya nidhamu za jamii ya binadamu na maangamio yao, hivyo Mwenyezi Mungu amewajibisha kwa hekima yake isiyo na kifani mambo kadhaa, endapo Waislamu wataizingatia hakika hawatopata mtihani wa dhambi hii kubwa.

HIJABU NI KATIKA MISISITIZO YA QUR’ANI:

Hakika Mwenyezi Mungu amewaamrisha wanawake na katika mahali mbalimbali ndani ya kitabu chake kitukufu kulihifadhi kwa hijabu, na katika baadhi ya maamrisho hayo ni katika Aya ya 31 ya surat al- Nuur:

"وَلْيضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيوبِهِنَّ وَلَا يبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا لِبُعُولَتِهِنَّ أَوْ آبَائِهِنَّ أَوْ آبَاءِ بُعُولَتِهِنَّ".

"Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwa waume zao, au baba zao, au baba wa waume zao”.

Na anasema tena (s.w.t) katika surat al- ah’zaab Aya ya 59:

"يا أَيهَا النَّبِي قُلْ لِأَزْوَاجِكَ وَبَنَاتِكَ وَنِسَاءِ الْمُؤْمِنِينَ يدْنِينَ عَلَيهِنَّ مِنْ جَلَابِيبِهِنَّ ذَلِكَ أَدْنَى أَنْ يعْرَفْنَ فَلَا يؤْذَينَ وَكَانَ اللَّهُ غَفُورًا رَحِيمًا".

"Ewe Nabii! Waambie wake zako, na binti zako, na wake za Waumini wajiteremshie nguo zao. Hivyo ni karibu zaidi kuweza kutambulikana wasiudhiwe. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe, Mwenye kurehemu”.

Na anasema pia katika Aya nyingine ya sura hiyo hiyo, Aya ya 32:

"يا نِسَاءَ النَّبِي لَسْتُنَّ كَأَحَدٍ مِنَ النِّسَاءِ إِنِ اتَّقَيتُنَّ فَلَا تَخْضَعْنَ بِالْقَوْلِ فَيطْمَعَ الَّذِي فِي قَلْبِهِ مَرَضٌ وَقُلْنَ قَوْلًا مَعْرُوفًا".

"Enyi wake wa Nabii! Nyinyi si kama yeyote katika wanawake wengine. Kama mnamcha Mungu basi msiregeze sauti zenu, akaingia tamaa mwenye maradhi katika moyo wake. Na semeni maneno mema”.

Na anasema tena katika sehemu nyingine Aya ya 53:

"وَإِذَا سَأَلْتُمُوهُنَّ مَتَاعًا فَاسْأَلُوهُنَّ مِنْ وَرَاءِ حِجَابٍ ذَلِكُمْ أَطْهَرُ لِقُلُوبِكُمْ وَقُلُوبِهِنَّ".

"Na mnapo wauliza wakeze haja waulizeni nyuma ya mapazia. Hivyo ndio usafi zaidi kwa nyoyo zenu na nyoyo zao”.

Na kwa kujengea jambo hili ni wajibu kwa wanawake wa kiislamu kujistiri kwa mavazi mazuri wawapo mbele ya wanaume wasio halali kwao, na watokapo katika jamii ya kadamsani wadhihirike wakiwa katika mavazi yanayowastiri na macho ya wenye matamanio ya haraka, na huu ndio wadhifa wa mwanamke wa kiislamu na kwa njia hii atalinda shakhsiya yake na nafasi yake ndani ya jamii, na huepuka macho ya wenye misisimko ya matamanio ya wenye kutazama maumbile ya wanawake wanaovutia katika jamii, na hatimae kupelekea maambukizi hatari katika fikira za vijana ya kuelekea kwenye mahusiano yasiyokuwa ya kisheria. Kwa kujengeajambo hili ni wajibu wa mwanamke asionekane katika sehemu za mikusanyiko ya watu wanaotazama watembeaji kwa madaha.

Kwanini ifikie mwanamke kushusha heshima yake hadi daraja hii? Na kwanini ifikie kujianika bayana na kusababisha maovu na mmomonyoko wa kimaadili? Na baada ya wanawake wenyewe kujiweka uchi au nusu uchi katika mitaa na vichochoro mbele za wanaume, matarajio yake suala hilo huishia kwa kutazama tu? Je! Hakuwezi kutokea uovu mwingine? Je! Jambo hilo haliwezi kupelekea kutokea mahusiano yasiyo ya kisheria? Na hapawezi kutokea masaibu mengine mengi ambavyo hayawezi kuelezeka? Na wapi yatokeapo mapenzi yasiyo matakatifu ambayo hupelekea kubomoa maisha ua kifamilia na kusambaratisha wanandoa? Kwanini wanaume hujaribu kuwafuatilia wanawake wa watu? Je! Hayajawahi kutokea matatizo yanayojiri katika ya wanaume wanaofuatilia wake za watu na kupsababisha ugomvi na hadi mauaji? Je! Uesharati ni mchache katika taifa letu? Je! Mambo yote haya hayasababishwi na jamii ya wanawake kuacha kujistiri kwa stara ya kiislamu, na je! Hatujawahi kusikia mahusiano yasiyo kuwa ya kisheria ambayo yamesababisha kubomoka nyumba za mabinti na wake waliokwisha olewa? Je! Hujawahi kuona kesi mbalimbali kuhusu kuibiana wake? Na watoto wangapi wanaishi maisha bila Mama, na Baba?.

Hakika mazingira yote hayo yamepeleka watoto kuishi maisha ya huzuni katika mitaa. Na wote hufahamu kuwa natija yake ni mahusiano ya haramu na starehe za mpito. Na mengine yaliyo wapumbaza wanawake na mfano wa hayo…

Ndio kwa mtazamo wa haraka ni kwamba hilo ndio chimbuko la moto huu uchomao na uteketezao familia, na kwa sababu hii wanawake wengi wanaojieka mazingira ya utupu na wale wajiuzao wamesababisha matatizo mengi ya kijamii, na ili kuepusha na kukinga mazingira haya machafu kutokea Uislamu umeamrisha wanawake kujistiri kwa mavazi ya kiislamu ili kuepuka macho hatari ya wenye matamanio ya haraka, na kujiweka mbali na macho ya wanaume mfano wa hawa..

KUMTAZAMA AJINABI:

Na ameamrisha tena wanawake wa Kiislamu kutotazama mwanaume ajinabi, na ameamrisha wanaume kujieusha kutazama wanawake ajinabi. Anasema (s.w.t) katika surat al- Nuur:

"قُلْ لِلْمُؤْمِنِينَ يغُضُّوا مِنْ أَبْصَارِهِمْ وَيحْفَظُوا فُرُوجَهُمْ ذَلِكَ أَزْكَى لَهُمْ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا يصْنَعُونَ. وَقُلْ لِلْمُؤْمِنَاتِ يغْضُضْنَ مِنْ أَبْصَارِهِنَّ وَيحْفَظْنَ فُرُوجَهُنَّ وَلَا يبْدِينَ زِينَتَهُنَّ إِلَّا مَا ظَهَرَ مِنْهَا وَلْيضْرِبْنَ بِخُمُرِهِنَّ عَلَى جُيوبِهِنَّ وَلَا يبْدِينَ زِينَتَهُنَّ".

"Waambie Waumini wanaume wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao. Hili ni takaso bora kwao. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za wanayo yafanya. Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipo kuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao”.[1]

Itaendelea......



[1] Al- Nuur/ 30 – 31.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: