bayyinaat

Published time: 21 ,September ,2018      16:06:30
News ID: 336

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


ATHARI YA JAMII YENYE DHAMBI YA ZINAA

Hapana shaka ya kwamba yale yaliotufikia kutoka katika Qur’ani tukufu pamoja na kauli za Maasummin ni kwamba; Madhambi ya mtu binafsi pia huishamili jamii ya wanadamu. Kwa mujibu wa kauli ya Shahid Mutahhari; katika kubainisha athari ya madhambi ya mtu binafsi yanayoishamili jamii amesema:

Suala la madhambi kumvaa mtu katika jamii huambukiza maradhi hayo watu wengine. Kwani mkusanyiko wa watu katika jamii huhesabika kuwa ni nafsi moja, yenye roho moja, yenye umri mmoja. Ambapo Allamah Tabatabaai anatubainishia matilaba hii yenye kustaajabisha ya kwamba; Kwa mujibu wa Qur’ani tukufu imebainisha kuwa mkusanyiko wa jamii ni kana kwamba ni; nafsi moja, bila kubagua mtu mmoja au kundi fulani katika jamii. Pindi Mwenyezi Mungu anaposema kwamba:

"وَلِکُلِ ّ أُمَّةٍ أَجَلٌ فَإِذَا جَآءَ أَجَلُهُمْ لَا یَسْتَأْخِرُونَ سَاعَةً وَلَا یَسْتَقْدِمُونَ".

"Na kila umma una muda wake. Utakapo fika muda wao basi hawatakawia hata saa moja, wala hawatatangulia”.

Baadhi ya watu hujiuliza ya kwamba; kwanini kaumu fulani inapotenda dhambi, na pindi adhabu ya Mwenyezi Mungu mtukufu inaposhuka huwakusanya Waja wema wachache wanaoishi katika jamii hiyo?

Hakika jawabu la swali hilo ni kwamba; Waulizaji hao hawatambui ya kwamba watu wa jamii huhesabika kuwa ni kiungo kimoja, hivyo pindi inapotolewa hukumu basi hukusanya viungo vyote vya jamii hiyo. Kwa sababu pindi kiungo kimoja kinapopatwa na ugonjwa la saratani, basi mizizi yake hushambulia viungo vyote vya mwili, hivyo viungo vingine havitaweza kusema kwamba kwanini tuangamie kwa ugonjwa huo na ili hali kiungo kimoja ndicho kilichoathirika. Hivyo basi; tambueni kuwa nyinyi ni kiungo kimoja, kwani kila kiungo kimoja katika mwili kinapopata ponyo bora basi ponyo hiyo hushamili viungo vyote na vile vile kinapopatwa na madhara ndivyo vingine vinapoathirika na kuadhibika. Isipokuwa Akhera ndio ulimwengu ambao watu huwa kila mmoja pekee. Ikiwa na maana kwamba, katika Dunia hii wanajamii wote huhesabika kuwa ni kitu kimoja hushirikiana katika furaha na karaha, shida na raha.

Kwa mujibu wa kanuni za kielimu imeafiki ya kwamba ikiwa kundi fulani katika jamii, litakuwa ni kundi fisadi ambapo kwa sababu ya maovu yao ikashuka balaa ya Mwenyezi Mungu basi balaa hiyo huikusanya jamii na watu wake, aliyekuwa salama na asiyekuwa salama pia humpata. Vile vile katika Dunia hii, Ardhi yenye rutuba na kavu huungua inaposhuka adhabu ya Mwenyezi Mungu, Minajili hiyo Dunia hii ni nyumba ya adhabu kwa wanaostahiki adhabu, na Akhera ni ulimwengu wa malipo kwa wanaostahiki Thawabu.

Minajili hii, kauli za wale ambao huyahusisha madhambi kwa mtu binafsi na kukabiliana na suala la kuamrisha mema na kukemea mabaya kwa ukali basi atakuwa ametoka nje ya mpaka wa kimantiki, kwa sababu akili pamoja mantiki salama huhukumu ya kwamba kuathirika kwa mtu binafsi, ametaka au bila kutaka, pia huathiri jamii nzima.

Hizi ni baadhi ya athari ya jamii yenye madhambi kwa kukiuka maamrisho ya Mwenyezi Mungu:

UKAME NA UKOSEFU WA MVUA

Kwa mujibu wa Riwaya tofauti zilizopokelewa kutoka kwa Maimamu watakatifu ni kwamba: Miongoni mwa matendo yanayopelekea kutonyesha mvua, ni kutotoa Zakaa, kama alivyosema Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) ya kwamba:

"خَمْسٌ إِنْ أَدْرَکْتُمُوهُنَّ فَتَعَوَّذُوا بِاللَّهِ مِنْهُنَّ لَمْ تَظْهَرِ الْفَاحِشَةُ فِی قَوْمٍ قَطُّ حَتَّی یُعْلِنُوهَا إِلَّا ظَهَرَ فِیهِمُ الطَّاعُونُ وَ الْأَوْجَاعُ الَّتِی لَمْ تَکُنْ فِی أَسْلَافِهِمُ الَّذِینَ مَضَوْا وَ لَمْ یَنْقُصُوا الْمِکْیَالَ وَ الْمِیزَانَ إِلَّا أُخِذُوا بِالسِّنِینَ وَ شِدَّةِ الْمَئُونَةِ وَ جَوْرِ السُّلْطَانِ وَ لَمْ یَمْنَعُوا الزَّکَاةَ إِلَّا مُنِعُوا الْقَطْرَ مِنَ السَّمَاءِ وَ لَوْ لَا الْبَهَائِمُ لَمْ یُمْطَرُوا وَ لَمْ یَنْقُضُوا عَهْدَ اللَّهِ وَ عَهْدَ رَسُولِهِ إِلَّا سَلَّطَ اللَّهُ عَلَیْهِمْ عَدُوَّهُمْ وَ أَخَذُوا بَعْضَ مَا فِی أَیْدِیهِمْ وَ لَمْ یَحْکُمُوا بِغَیْرِ مَا أَنْزَلَ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ إِلَّا جَعَلَ اللَّهُ عَزَّ وَ جَلَّ بَأْسَهُمْ بَیْنَهُمْ".

"Mambo matano iwapo mtayadiriki basi tafuteni kimbilio kwa Mwenyezi Mungu ambayo miongoni mwayo ni kwamba; Haitadhihiri dhambi ya zinaa katika jamii; isipokuwa hufuatiwa na magonjwa mazito yenye maumivu makali ambayo hayakutokea katika wale waliotangulia kabla yenu ambao wamepita. Hawakupunguza vipimo vya mizani isipokuwa wamepatwa na shida ya mapato pamoja na ukame na dhulma ya Watawala wa zama zao. Hawakukataza kutoa Zaka isipokuwa wamezuiliwa tone hata moja la mvua kutoka Mbinguni, laiti isingekuwa wanyama basi wasingeletewa mvua hata mara moja. Na hawakupinga ahadi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake isipokuwa wametawaliwa na Adui wakali, (Adui hao) wakapokonya waliyokuwa wakimiliki. Na hawakuhukumu kwa mujibu wa maamrisho ya Allah mtukufu isipokuwa Mwenyezi Mungu ameweka hofu kati yao”.

Amesema Imamu Baqir (a.s):

"اَما اِنَّهُ لَیْسَ مِنْ سَنَةٍ اَقَلَّ مَطَراً مِنْ سَنَةٍ وَلَکِنَّ اللَّهَ یَضَعُهُ حَیْثُ یَشاءُ اِنَّ اللَّهَ جَلَّ جَلالَهُ اِذا عَمِلَ قَوْمٌ بِالْمَعاصِی صَرَفَ عَنْهُ ما کانَ قَدَّرَ لَهُمْ مِنَ الْمَطَرِ فِی تِلْکَ السَّنَةِ اِلَی غَیْرِهِمْ وَاِلی الْفَیافِی وَالْبِحارِ وَالْجِبالِ وَاِنَّ اللَّهَ لَیُعَذِّبُ الْجُعَلَ فِی حُجْرِها بِحَبْسِ الْمَطَرِ عَنِ الْاَرضِ الَّتِی هِیَ بِمَحَلَّتِها لِخَطایا مَنْ بِحَضْرَتِها وَقَدْ جَعَلَ اللَّهُ لَها السَّبِیلَ اِلی مَسْلَکٍ سِوَی مَحَلَّةِ اَهْلِ الْمَعاصِی قالَ ثُمَّ قالَ اَبُو جعفر(ع) فَاعْتَبِرُوا یا اُولِی الْاَبْصار".

"Hakika hapana mwaka uliopungukiwa na mvua isipokuwa Mwenyezi Mungu huelekeza mvua hiyo atakapo. Na pia huwaondolea watu mvua aliyowakadiria katika mwaka huo na kuelekezea mahala pengine kwa sababu ya kutenda kwao maasi, mfano jangwani, baharini na milimani, vile vile Mwenyezi Mungu hufukia matundu ya mende ardhini kwa kuangukiwa na mvua kwa sababu ya kuhudhuria mahali patendekapo maasi ya watu wa hapo, hadi watakapoelekea katika kivuli cha wasiotenda maovu (Ndio utakuwa wokovu wao), Kisha akasema Imamu Abu Jaafar(a.s) kuwa: Zingatieni enyi wenye macho na wazingativu”.

Itaendelea.......


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: