Kila
siku binadamu anatafuta mwongozo. Kutafuta huku humfanya binadamu huyu
aonane na binadamu wengine wengi, hivyo kwamba tunaweza
kukulinganisha huku kujaribu kwake zaidi au kidogo na kuhangaika kwa mtu mwenye
kiu katika jangwa lisilo na maji, ambaye anadanganywa na mazigazi, (sarabi) mia
moja na moja.
Tunahitaji
mtu asiyefanya dhambi na asiyekosea, mtu ambaye kwamba hata
tukichungua kiasi gani utu wake, hatuwezi kuona hata dalili ya hitilafu katika
mpango wake, ambao wingi wa tabia zake za maisha hufanya picha tukufu kwa ajili
ya macho yetu kutazama na roho zetu kujipatia mwongozo mwema.
Mtu
huyo ni lazima awe katika bali ambayo kila binadamu duniani kote
aweze kupata mfano wa kufuata. Tunapolinganisha na kuamua ni yupi
kati ya watu mashuhuri duniani, tunaona kwamba uwezo wa uongozi wao unafikia
kiwango fulani tu cha kazi zao na nguvu zao za uongozi. Tunaweza tukamtaja
Vikramaditya kama mfano wa mfalme mwadilifu lakini mfano wake ni kwa wafalme
tu; au tunaweza kumtaja Asoka kama bingwa wa amani walakini anashindwa kutupa
matumaini tunapojaribu kumfikiria kama kiongozi mashuhuri wa nchi; na wote hawa
wawili waliotajwa hapo juu wanashindwa kutupa mfano kwa raia. Au tunaweza
kumtaja Mtakatifu Petro kama roho chamungu lakini atawezaje
kutuongoza kama tukikabiliwa na machafuko ya kitaifa? Tunaweza pia
kuwataja wapiganaji na watekaji mashuhuri lakini majinayao hayatakuwa
na maana kwetu tukihitaji mfano wa mtu mwenye uvumilivu na uwezo wa kuvumilia
taabu na mateso.
Kwa
kifupi, tunaweza kupata watu walio nyota zitumulikazo kwa nuru ya
sifa za utu moja au zaidi, lakini historia itashindwa kutuonyesha jina
linaloweza kuwaongoza, watu wote waishio katika mazingira ya namna mbalimbali
isipokuwa Hadhrat Ali bin Abi Talib (Amani ya Mwenyezi Mungu na iwe juu yake)
tu.
Hapa
tunatoa kwa ufupi tu maisha ya ajabu ya mtu huyu wa ajabu mwenye
uwezo wa kufahamu mambo mengi ambaye walimwengu wanapasika kumjua na
kumpendelea.
Nasaba
yake:
Hadhrat
Ali (a.s.) alikuwa mwana wa Bwana Abu Talib mwana wa Abdul Muttalib wa ukoo wa
Hashim ambao ulikuwa wa kabila la Quraish mtu aliyekuwa na nguvu sana
na aliyeheshimiwa, aliyetokana na kizazi cha Nabii Ibrahimu (a.s.). Mama yake
Hadhrat Ali (a.s.) ni Bibi Fatimah binti yake Bwana Asad, mwanamke
aliyeheshimiwa na aliyekuwa wa ukoo wa Hashim. Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.) na Hadhrat
Ali (a.s.) ukoo mmoja.
|
|
ABDUL
MUTTALIB |
|
|
|
|
|
|
|
||
|
|
|
|
|
|
Abdullah |
|
Abu Talib |
|||
|
|
|
|
|
|
Mtukufu Mtume
Muhammad [s] |
|
Ali |
|||
Zaidi
ya hayo Bwana Abu Talib ndiye aliyemlea Mtukufu Mtume (s.a.w.) tangu baba yake
alipofariki dunia kabla hata ya kuzaliwa kwake Hadhrat Ali (a.s.).
Kuzaliwa
kwake:
Mtume
(s.a.w.) alikuwa na umri wa miaka thelathini alipozaliwa Hadhrat Ali
(a.s.) ndani ya Kaaba mnamo tarehe 13 mwezi wa Rajabu mwaka wa 30 Aamul-Fiil
(sawa na mwaka 600 Miladiya). Wazazi wake walifurahi sana kuona kuwa mwana wao
alikuwa anapendwa sana na mwana wa ndugu yao (yaani Mtukufu Mtume s.a.w.)
ambaye alikwishagundua kutokana na uso wa mtoto huyo (Ali a.s.) ushupavu na
nguvu vitu ambavyo vitamfanya kuwa msaidizi mkubwa utakapokuja mwito kutoka
Mwenyezi Mungu.
Kulelewa
kwake.
Kwa
sababu ya matuchumi ya Bwana Abu Talib, Hadhrat Ali (a.s.) alilelewa na Mtukufu
Mtume (s.a.w.) ambaye alimpenda na kumtunza vizuri sana kijana huyu
aliye binamu yake. Akamwongoza katika fikara zile zile zilizouongoza moyo
wake.
Waujumbe:
Ilikuwa
ni matokeo ya malezi (mema kutoka (wa Mtume s.a.w.) kwamba katika umri wa miaka
kumi Hadhrat Ali (a.s.) alisikia Mtukufu Mtume (s.a.w.) akitangaza kuwa
amechaguliwa kulichukua Neno Ia Mwenyezi Mungu na kuwataka watu wake waamini na
kumuunga mkono. Ilikuwa ni mvulana huyu mwenye umri wa miaka kumi, aliyekuwa na
ushupavu wa kusimama tayari kutii na kufuata (utume wa Mtume s.a.w.) na hivyo
basi akawa shahidi wake wa kwanza, msaidizi wake na mrithi wake. Sauti ya
Hadhrat Ali (a.s.) ilikuwa (ndio) ile sauti iliyopazwa ili kumpa
Mtukufu Mtume (s.a.w.) msaada wake familia yake, kabila lake, jamii yake, jiji
lake, na hata watu wote Uarabuni kote walipompinga vikali.
Nyakati
za shida:
Mara
tu baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) kutangazia Ujumbe wake upinzani ulianza
pande zote. Watu ambao mpaka jana yake, kabla ya kuutangaza
Ujumbe huo walimheshimu kwa sababu ya ukweli na uaminifu wake, sasa walianza
kumwita mnafiki, kichaa, mchawi na kwa nini wasimuite hivyo? Walianza kuweka
miiba katika njia yake, walimpiga mawe na hata kumtupia taka taka
kichwani kwake. Katika dhidi yote hii kijana mwenye umri wa miaka
kumi ndiye sahaba peke yake aliyelichukua Neno la Mwenyezi Mungu. Hadhrat
Ali (a.s.) katu hakukata tamaa na kila mara alikuwa karibu zaidi na Mtume
(s.a.w.). Hatimaye, wakati ulifika ambapo watu wa Maka waliamua
kumgomea Mtume (s.a.w.) na familia yake. Bwana Abu Talib alimchukua Mtume
(s.a.w.) na watu wake na kuwapeleka kwenye bonde (Iiitwalo (Shaab Abi
Talib) lililokuwa jirani na jiji la Maka na kuishi huko kwa muda wa
miaka mitatu wakiwa wametengwa kahisa na watu wengine. Waliishi katika hatari
ya kila mara ya kushambuliwa na maadui wao wakati wa usiku. Hivyo, ili kumkinga
Mtume (s.a.w.) na dhara lo lote lile liwezalo kutokea, Bwana Abu Talib alikuwa
akichukua hadhari ya kumhamisha Mtume (s.a.w) kutoka kitanda kimoja hadi
kingine kila usiku na kitandani pake Mtume (s.a.w.) alikuwa akimlaza mmoja
wa wanawe. Kutokana na hayo, Hadhrat Ali (a.s.) alijifunza jambo
ambalo alikuwa akilikariri kila mara katika maisha yake.
Hijrah
Baada
ya kifo cha ami yake mpenzi Bwana Abu Talib, Mtume (s.a.w.), ilimbidi kukutana na dhiki
na matatizo makubwa na maadui zake wakawa wakatili zaidi. Siku moja maadui wa Mtume
(s.a.w.) waliamuwa kuizunguka nyumba yake na kumuua akiwa usingizini. Mtume (s.a.w.)
alipopata hatari hizi alimwita Hadhrat Ali (a.s.) na akamwambia aIale kitandani
pake badala yake yeye Mtume (s.a.w.) aondoke kimya kimya kwenda Madina. Hadhrat
Ali (a.s.) alimuuliza Mtume (s.a.w.), "Je, Mpango huu utayaponyesha maisha
yako, ewe Mtume wa Mungu? Alipopata jibu la kumthibitishia kuwa Mtume (s.a.w.)
atasalimika, Hadhrat Ali (a.s.) alilala usingizi mzito (wa furaha kitandani pa
Mtume (s.a.w.).
Usika
wote ule Machifu wa Makuraishi waliokuwa na hamu ya kumwaga damu, walingojea
mpaka kuche na waingie ndani na kumuua Muhammad (s.a.w.) Lakini asubuhi
yake wale maadui waliona kuwa yule waliyekuwa wakimngojea alikwishaondoka na
badala yake walimkuta Hadhat Ali ambaye walimdhania kuwa ni yeye Mtume
(s.a.w.). Maadui hao walimwuliza Hadhrat Ali (a.s.) alikokwenda Mtume (s.a.w.).
Hadhrat Ali (a.s.) aliwauliza maadui hao swali badala ya kuwapa jibu la swali
lao akiwauliza kama walimuweka kuwa mchunga wa Muhammad. Hivyo maadui
hao walirudi makwao huku wakiwa wamejaa hasira na wasi wasi. Mtume
(s.a.w.) alifaulu kwenda mwendo mrefu bila ya matatizo yo yote. Hadhrat
Ali (a.s.) alibaki mjini Maka kwa muda wa siku tatu zaidi na aliutumia muda huo
kuwarudishia wenyewe vitu vilivyowekwa amana kwa Mtume (s.a.w.). Baada ya hapo
Hadhrat Ali (a.s.) aliondoka kwenda Madina kwa miguu akiongoza msafara wa
ngamia waliowabeba wanawake wa nyumba yake. Alipofika Madina miguu yake ilikuwa
inatoka damu na nyayo zake zilikuwa zikitoka malengelenge. Hii
inaonyesha imani Mtume (s.a.w.) aliyokuwa nayo juu ya Hadhrat Ali (a.s.) na
nguvu na ujasiri vita ambavyo Hadhrat Ali (a.s.) alivithibitishia imani yake
hiyo.
Ndoa
yake:
Mtume
(s.a.w.) alipofika Madina, kitu cha kwanza kumuoza binti yake Bibi Fatimah (a.s.)
kwa Hadhrat Ali (a.s.). Mtume (s.a.w.) alimpenda sana binti
yake na kila mahali alipomjia, Mtume (s.a.w.) alisimama ili kuonyesha heshima
yake kwake. Kwa hiyo, kila mmoja alitazamia kumuoa Bibi Fatimah (a.s.) na
wengine waliwahi hata kupeleka posa zao kutaka kumuoa binti wake Mtume
(s.a.w.). Lakini Mtume (s.a.w.) alimwambia kwamba binti yake hawezi
kuolewa bila ya ruhusa ya Mwenyezi Mungu. Ilikuwa katika mwaka wa kwanza
wa Hijira Hadhrat Ali (a.s.) alipochaguliwa kutunukiwa heshima hii ya kumuoa
binti yake Mtume (s.a.w.) na harusi ilifanyika katika njia rahisi sana.
Binti yake Mtume (s.a.w.) hakufungashiwa hata vyombo vya nyumbani na baba
yake, bali vile vyombo vya nyumbani alivyovipata vilinunuliwa kutokana tu na
fedha aliyoitoa Hadhrat Ali (a.s.) kwa ajili ya "Mahari". Vyombo
hivyo ni pamoja na vyungu vya udongo wa mfinyanzi vichache, mito michache
ya majani ya mtende, kitanda cha ngozi, gurudumu Ia kusokotea nyuzi za sufi,
kijaa na kiriba. Na Hadhrat Ali (a.s.) aliuza deraja yake ili kupata fedha ya
kulipia mahari. Kwa hiyo, ulikuwa mfano kwa Waislamu wote ili kutumia
akili katika matumizi yao na kuepuka kutumia pesa zao holela wakati
wa sherehe za harusi.
Itaendelea...