bayyinaat

Published time: 22 ,September ,2018      14:51:17
News ID: 340

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Sote tunajua kwamba maonyo mfano wa lawama ni jambo zito nafsini, hasa lawama hii itakuwa imepitiliza mipaka anayoitumia mtu kila wakati kulaumu wengine kwa namna ambayo kwamba itakuwa ni jambo la linajitokeza kila mara, na mwanadamu ambaye kwa kawaida yake ni kulaumu watu wengine, atajikuta amekosa marafiki wengi na watu wa karibu siku hadi siku, ni jambo la muhimu kwa mke kutambua ni namna gani atakavyomkanya mumewe ili isipelekee lawama hizo kuharibu hisia za mume za kuwa pamoja na mkewe, na asije kukosa malengo na makusudio yake, hakika mke kiujumla hakanyi kwa ajili ya kumuadhibu mumewe, bali hulaumu kwa sababu ndani yake ni kutaka marekebisho na kutojirudia makosa kwa mara nyingine tena, lakini pia ziko njia mbalimbali na mazingira mbalimbali na mbinu mbalimbali ambazo hazilinganishwi na maonyo haya, tutazipembua katika nukta zifuatazo:

Kwanza: Ni juu yake kugeuza kiini cha lawama mbele yake, na kuikagua pande zote, aonapo maudhui yake ni kero basi hastahiki kuibua ghadhabu yake na bora zaidi ni kupuuzia na kutofungua ukurasa wa lawama mbele ya mume wake, na asithubutu hata chembe ya kunena kama wasemavyo wahenga.

Pili: Mke apaswa kuchagua muda na mahali pafaapo kwa kumshauri mumewe, hivyo asiwe ni mwenye kutoa lawama kwa suala fulani, ambalo itarudi kwenye kumbukumbu chungu arudiapo nyumbani baada ya kufukuzwa kazi kwa mfano, na kisha asimlalamikie ilihali yu usingizini au kumwamsha usingizi na kumshtakia malalamiko pia, na vilevile asimtenze nguvu kwa kumlaumu mbele ya kadamnasi au mbele ya watoto wake, na asimlalamikie wakiwa mahali pa utulivu na pahitajikapo utulivu na ukimya.

Tatu: Yampasa Mke kuchagua njia sahihi ya ushauri kwa mume wake, na kuwa makini kuhusu mambo yafuatayo:

Kuzungumza kwa sauti ya utulivu na upole, na asiwe mwenye kubeba sauti ya hasira, na kupiga kelele, chuki, dhihaka, na kutoheshimu na kushusha shani yake.

Pia yampasa kumshitakia kwa ulaini na kumuachia nafasi ya kuzungumza na kujieleza, hata kama kile anachosema kinaukera moyo kwa ukweli au maelewano mabaya kutoka kwake, na akubaliane na uongo wake kwa uhalali wa busara, hivyo ajiepushe kumwambia "Wewe ni muongo” na badala yake aseme "unachosema sio kweli”.

----------------------


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: