bayyinaat

Published time: 22 ,September ,2018      14:52:34
News ID: 341

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye ku rehemu


Uongo ni haramu, nao ni katika madhambi makubwa ambayo kwamba Mwenyezi Mkungu ameahidi adhabu kali juu yake, akibainisha hilo ndani ya kitabu chake kitukufu na kwamba amewajibisha moto juu yake. Na hakika uongo ni maradhi mabaya mno, kwa sababu husimamia suala la kumpumbaza mwanadamu kuwepo kwa mizania ya uongo. Uchache wake ni kumuokoa kutokana na mashinikizo na kubebeshwa majukumu. Na bila shaka utamsababishia matatizo makubwa mno, na ukweli ni kwamba uongo kiujumla ni uharibifu na matatizo pia:

RIWAYA TUKUFU

Imepokelewa kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w)- alipoulizwa: Je! Muumini huwa mwoga? Akajibu: Ndio. Akaulizwa Je! Muumini anakuwa bahili? Akajibu: Ndio. Akaulizwa tena: Je! Muumini anapaswa kuwa muongo? Akajibu: Hapana. [1]

ADA YA UONGO

Muongo hukosea asemapo uongo, kwani huwa akidhani kuwa kutosema ukweli kutamuepushia baadhi ya majukumu yanayomkuta, na ilihali ukweli ni kwamba matendo yake haya husababishwa na kasoro pamoja na mapungufu ya ufahamu wake na maarifa yake, kwani hufedheheka hata baada ya muda, na athari zake huwa mbaya mno. Imepokelewa kutoka kwa Imam Ali (a.s): "الصدق منجاة وكرامة" "Ukweli ni uokovu na utukufu pia”.[2]

MIONGONI MWA WASIFA MBAYA NA ATHARI ZA UONGO

Uongo hukinzana pamoja na imani: anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

﴿إِنَّمَا يَفْتَرِي الْكَذِبَ الَّذِينَ لاَ يُؤْمِنُونَ بِآيَاتِ اللّهِ وَأُوْلئِكَ هُمُ الْكَاذِبُونَ.

"Wanao zua uwongo ni wale tu wasio ziamini Ishara za Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waongo”.[3]

Uongo ni katika alama za unafiki: Kutoka kwa Mtume (s.a.w.w):

"ثلاث خصال من علامات المنافق: إذا حدّث كذِب، وإذا ائتمن خان، وإذا وعد أخلف".

"Mambo matatu ni alama za Mnafiki: azungumzapo husema uongo, na akiaminiwapo hufanya hiana, na anapoahidi hukhalifu ahadi”.[4]

Uongo ni chimbuko la madhambi yote: Kutoka kwa Imam Askari (a.s):

"جُعِلت الخبائث كلها في بيت وجُعِل مفتاحها الكذب".

"Yamewekwa machafu yote katika nyumba moja na ufunguo wake ni uongo”.[5]

Tahadhari za dini kwa kuongozana na muongo: Kutoka kwa Amirl muuminin (a.s):

"ينبغي للرجل المسلم أن يجتنب مؤاخاة الكذّاب، فإنّه يكذب حتى يجيء بالصدق فلا يُصدَّق".

"Yampasa Mtu Mwislamu kujiepusha kusuhubiana na muongo, kwani husema uongo kiasi ambacho akileta ukweli hasadikiki”.[6]

Ukosefu wa kusali sala za usiku: Kutoka kwa Imam Sadiq (a.s):

"إن الرجل ليكذب فيُحرم بها صلاة الليل، فإذا حرم صلاة الليل حُرِم بها الرزق".

"Hakika Mtu asemapo uongo hukosa ladha ya Sala ya usiku, na akosapo Sala ya usiku hukosa Riziki”.[7]

NASAHA YA NABII (S.A.W.W)

Inasimuliwa ya kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w) alimnasihi mtu mmoja, kwa kumwambia: Jistiri kwa kuepuka mambo manne: Zinaa, kunywa pombe, wizi na uongo, vyote utakavyo nimekuachia. Akamjibu (s.a.w.w): "Acha uongo”. Alipoondoka ilimjia shauku ya kujua kuhusu zinaa, na akauliza kuhusu zinaa, kisha wizi, na kisha kunywa pombe, kisha akazidi kusisitiza juu ya hayo. Akasema nimeshikilia njia hizi zote, na nitaacha yote hayo.[8]

UONGO KATIKA MZAHA NA UONGO MDOGO

Katika vigawanyo vya uongo wa haramu ni ule uwapo kwa utani na kwa lengo kuchangamsha jamii na kucheka pamoja ya msikilizaji kutofahamu hilo, kutoka kwa Imam Amirul muuminin (a.s):

"لا يجد عبد طعم الإيمان حتّى يتّرك الكذب جدّه وهزله".

"Mja hatopata ladha ya Imani hadi atakapoacha uongo ima kwa mzaha au kwa kukusudia”.[9] Aidha yampasa kujiepusha na uongo ulio kwa kiwango kidogo, kutoka kwa Imam Sajjad (a.s):

"اتّقوا الكذب، الصغير منه والكبير، في كلّ جدّ وهزل".

"Ogopeni uongo, ima uwe mdogo au mkubwa, katika hali ya utani na ithibati”.[10]

KUTOKA MOYONI!

Ndugu yangu mpendwa, hakika hapana jambo zuri kuliko ukweli, na hapana starehe kubwa ya nafsi na roho kuliko ukweli, kwani muongo anaishi chini ya kidhibiti cha uongo wake maadamu bado haujajulikana. Na daima huishi kwa fedheha na udhalili pindi atambulikapo. Na ama mtu mkweli huenda baadhi ya nyakati akaathirika kidogo lakini anakuwa ni uthibitisho wa Aya hii tukufu:

{قَالَ اللّهُ هَذَا يَوْمُ يَنفَعُ الصَّادِقِينَ صِدْقُهُمْ لَهُمْ جَنَّاتٌ تَجْرِي مِن تَحْتِهَا الأَنْهَارُ خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا رَّضِيَ اللّهُ عَنْهُمْ وَرَضُواْ عَنْهُ ذَلِكَ الْفَوْزُ الْعَظِيمُ}.

"Mwenyezi Mungu atasema: Hii ndiyo Siku ambayo wasemao kweli utawafaa ukweli wao. Wao watapata Bustani zipitazo mito kati yake. Humo watadumu milele. Mwenyezi Mungu amewawia radhi, nao wawe radhi naye. Huku ndiko kufuzu kukubwa”.[11]

----------------------[1] Kashf al- Ghummah, juz 3, uk 8.

[2] ‘Uyuun al- Hikam wa al- mawaaidh, uk 42.

[3] Surat an- Nahl, 105.

[4] Wasaail al- Shia, juz 15, uk 340.

[5] Bihaar al- anwaar, juz 69, uk 263.

[6] Rejea ile ile, uk 288.

[7] Al- dhunuub al- kabirah, Dastaghib, juz 1, uk 287.

[8] Miizan al- Hikma, juz 3, uk 2674.

[9] Al- dhunuub al- kabirah, Dastaghib, juz 1, uk 292.

[10] Rejea ile ile, uk 292.

[11] Surat al- Maida, 119.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: