bayyinaat

Published time: 22 ,September ,2018      14:56:04
News ID: 344

بسم الله الرحمن الرحیم

Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema mwenye kurehemu


Mmoja wetu ana ndoto za kumpata mwenza wake wa maisha ambaye atashirikiana naye matatizo ya maisha yake, na kugawana naye majukumu na nyadhifa zake, na pindi mwanadamu anapokutana na ampendaye, na akaamua kwamba mtu huyo ndiye amfaaye, kwa kufanana sifa, na kuwa wanaendana, hapo ndipo mwanaume anatangulia kumchumbia binti ampendaye, na hapa ndipo majukumu huanzia ya kulinda mahusiano kati yake kwa kila mmoja kulinda hisia za mwingine, na kufahamiana wao kwa wao kwa kiasi kikubwa, kwani kufahamiana hujenga msingi wa maelewano katika yale yajayo, na kwamba uwazi ni jambo muhimu katika mahusiano kati ya wachumba wawili, na pindi maneno yawapo ya uwazi na bayana hakika hakitaharibika kitu, na pindi mahusiano yao yatakuwa yenye nguvu na kuiva basi ndio mwanzo ya kufaulu na kuendeleza maisha ya pamoja.

Wakati mwingine humtokea mchumba kusimamia misimamo yenye kujeruhi kwa mpendwa wake, na huenda yakajitokeza mengi katika akili ya kwamba ni jambo gani litazungumza na mchumba wangu na hivyo ndivyo yanayomkuta mchumba mwenyewe, na ukweli ni kwamba hutokea visingizio vingi katika maneno yao pindi yanapokuwa ni mchanganyiko, lakini ni jukumu la mchumba (wa kiume) kuzungumzia masuala ambayo ni muhimu sana na Mwenzi wake, kisha baada ya kufahamiana ndipo kuhamia suala la juu au chini kuhusiana na umuhimu wa mahusiano yao, bila shaka mazungumzo ni kipaji, na mchumba (mwanaume) mahiri ni mchumba mwenye uwezo wa kudhibiti kipaji za kuzungumza na mwenza wake kwa umahiri na ufanisi, sasa ni upi umuhimu wa kanuni katika mazungumzo ya mwanaume aliyechumbia kwa mwenza wa maisha mtarajiwa?

Yampasa Mtu ambaye (ni mchumba) na hasa yule ambaye yapo mafungamano baina yake na mshirika wa maisha kuzungumza naye kwa utulivu na kimahaba pamoja na mwenzi wake mtarajiwa, kwa ajili ya kulinda penzi la mwanamke kwa mazungumzo yake laini, kwani mwanamke humpenda ambembelezae kwa utulivu na mahaba, na yote hayo kawaida huwa ndani ya mipaka ya ustaarabu na heshima na wema, endapo atavuka mipaka siku zote huja natija hasi katika mahusiano yao.

Heshima ya mtu kwa mwenzi wake ina jukumu kubwa katika kufikia uelewa kati yao. Kwani mwanamke hampendi Mwanamume anayejikweza ambaye anaamiliana pamoja naye kana kwamba ndiye bora zaidi na mkubwa, kwa sababu muamala wa ubinadamu na mawada na huruma hujenga ndani ya nyoyo za watu miujiza ya ajabu.

Yampasa mwanamume kufuata nyenzo ambazo zamfurahisha mwenza wake kwa kuzisikia, ambazo zitamchangamsha mwenza wake kuhisi matarajio yake na ndoto zake, na vilevile ashirikiane naye pia katika kufikia ndoto zake na matarajio na yake ayafikiriayo kuhakikisha anafikia mustakabali wa maisha yake, na wafahamiane katika njia za maisha ya kifamilia, kwani kila mmoja wetu anazo matumaini na maono tafauti na mwingine, na malengo ya uchumba ni kuhakikisha muafaka kwa daraja kubwa, kwa ajili ya kujenga familia yenye maelewano mema na mazuri.

----------------------


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: