Maisha ya Ibn sina (Avicnena)
Makala iliopita tulieleza kwa ufupi Historia
ya Tiba katika Uislamu, na kuashiria baadhi ya madaktari waliopatika katika
ulimwengu wa Kiislamu, ambapo miungoni mwao alikuwa ni daktari mahiri, mashuhuri
Ibun Siina (Aviccena).
Ama katika makala hii nitazungumzia maisha
yake kwa ufipi na kugusia baadhi ya nukta muhimu za Elimu ya Tiba katika Qur'an
na mtazamo wake kunako masuala ya Tiba na taaluma mbalimbali za kisayansi,
hivyo basi nakuomba ndugu msomaji kuwa pamoja nami katika kuangalia misingi ya Kiislamu kunako
Elimu za Tajiruba na sayansi.
Ibun Sina (Avicena) alizaliwa mwaka
370 A.H Sehemu ya Balakh ambayo ilikuwa ndani ya taifa la Iran ya zamani,
ambapo hivi sasa ni ndani ya nchi ya Afghanistani, baba yake alikuwa ni katika mwana
siasa na ni miungoni mwa wanazuoni maarufu wa zama zake, Ibun Sina (Avicena) alilelewa
katika mazingira ya kiimani sambamba na mashiko halisi ya dini ya kiisilamu,
ambapo katika miaka kumi ya awali alijifunza Qur’an na elimu za kilugha, pia
alijifunza Elimu za kiakili na hesabu
kwa bwana Mahmudi Masaha na kusoma Elimu
ya Mantiki kwa bwana Natly, pia
kujifunza alimu za Sheria na Kifikihi kwa sheikh Ismail Zahid katika sehemu
hiyo.
Imeelezwa kuwa Avicenna alisoma
kitabu cha Arustrit mara arubaini, pia alikuwa anachunga sana masuala ya Imani,
Dini na Sheria zake, naye alikuwa mtu wa ibada sana na mwenye jitihada katika
kutafsiri Qur’an na kuihifadhi na
kujifunza Elimu ya Hadithi. Alianza kujifunza Utabibu na Udaktari akiwa na umri
wa miaka 16 naye alikuwa akisema: katika muda mchache nilipokuwa ni kujifunza
Elimu ya Tiba nilipata umahiri na uwezo mkubwa wa Elimu hiyo, na nikapata
umaarufu mkubwa na kufahamika sana katika kutibu wagonjwa.
Avicenna aliendelea na harakati zake
hizo mpaka mnamo mwaka 428 A.H akafariki na kuitika wito wa mola wake. Ama Kuhusiana
na mahala alipo fia kuna tafauti baina ya wana Historia kama ifuatavyo: baadhi
yao wanasema alifia Hamadani na wengine husema amefia Isfahani, vyovyote vile
iwavyo Ibun sina amezikwa Hamadani na kaburi lake linapatikana hapo.
Kuathiriwa kwake na mafunzo ya Kiislamu
Kama nilivyo sema hapo mwanzo kuwa
Avicenna alijitahidi kutafsiri Quran na kujifunza Elimu ya Hadithi, hivyo basi vitu
hivi vilikuwa vina mchango mkubwa katika Elimu yake na hapa nitaashiria nukta muhimu zifuatazo:
1-Lengo la kuteremshwa Qur’an ni kumlea na kumuongoza Mwanadamu
katika masuala ya kiroho na kumfikisha Mwanadamu huyu katika saada, ukamilifu
na uzima wa milele, na hapa jambo la kuzingatiwa ni kwamba ijapokua Qur’an imeelezea kwa mapana zaidi saada ya
mwanadamu lakini pia haikuacha kuashiria
masuala ya kisayansi na elimu za Tajiruba, na kuashiria kwake masuala
hayo hakumaanishi kwamba Qur’an imegeuka
kuwa ni kitabu cha sayansi. kwani Elimu ya Sayansi na Tajiruba zinaweza kufikiwa
na akili ya Mwanadamu pekee kwa minajili hiyo hakuna maana kusema kuwa Qur`an
ni kitabu cha Elimu za Tajiruba. ama kuashiria kwa Qur’an kunako masuala hayo ni kama ifuatavyo:
1.
Kumshajiisha Mwanadamu katika kumjua Mola Muumba wake
2.
Kumfanya Mwanadamu awe mchunguzi katika masuala ya Elimu ya Tajiruba
3.
Kuwashajiisha Waisilamu na wanadamu katika kutafuta Elimu katika
Nyanja tafauti .kwa minajili hiyo Qur’an
si kitabu cha Tiba mpaka Wanadamu watarajie Elimu ya Tiba kutoka kwenye Qur’an
la hasha sivyo hivyo kwani Elimu hizi zinaweza fikiwa kwa akili aliopewa
mwanadamu.
Ama kugusia kwake Quran katika
baadhi ya masuala ya kitiba na elimu zingine za Tajiruba kama vile: utungaji wa
ujauzito, alama za mikono, uponyaji wa asali, Afya ya mwili na usalama wake, na… yote hayo
ni kwaajili ya kumfanya Mwanadamu atafakari
katika alama za kuwepo Mola wake muumba na kuamsha hisia za mwanadamu
huyu kunako utafiti katika masuala ya sayansi na Tajiruba.
2-Hakuna dini au kundi lolote la kiimani
lilioipa kipaumbele elimu na kusisitiza kunako elimu kama ilivyo sisitiza dini
ya Kiislamu, kiasi kwamba daraja ya msomi na mwanazuoni mwenye imani ni tafauti
na muumini asiyekuwa na elimu, na Mwenyezi mungu anasema katika Qur’an surat mujadalah aya 11 akisema :
یرفع الله الذین آمنوا والذین اوتواالعلم درجات
"Mwenyezi mungu
atawanyanyua walioamini na wenye elimu miongoni mwenu, daraja la juu”.
na neno (elimu) katika Qur’an limekaririwa
mara 80 pia neno (wenye utambuzi) na (wenye akili) limekaririwa zaidi ya mara
10 na aya zinginezo nyingi zikiwataka wanadamu wawe wenye kutafakari na
kuzingatia na…
Haya yote yanaashiria kuwa Uislamu umezingatia zaidi na kuhimiza suala la Elimu na kutumia
akili. pia upande wa hadithi za mtukufu Mtume (s.a.w) nazo zimehimiza suala la
kutafuta Elimu na kutafakari kama alivyo sema mtukufu Mtume (s.a.w.w):فکرة ساعة خیر من عبادة سنة
Saa moja katika hali ya kutafakari
ni bora kuliko ibada ya mwaka mmoja .
Pia anasema mtukufu Mtume (s.a.w.w):
kuhudhuria katika kikao cha mwanazuoni ni bora zaidi kuliko kusindikiza
majeneza Elfu moja ya waumini, kuwatembelea wagonjwa elfu moja waumini ,… kufunga siku elfu
moja... kwani mwafahamu kwamba Mungu huabudiwa kwa Elimu.
Hivyo basi Uisilamu umesisitiza vitu
viwili katika jamii ya kibinadamu navyo ni: mwanazuoni, Hakimu, na Tabibu.
Kama alivyosema Imam Swadiq (a.s) kila
mji na mkoa wahitaji vitu vitatu :mwanazuoni ,hakimu wa sheria na tabibu au
daktari.
Semi hizi na wito huu wa Uislamu
ndio uliomfanya Ibun sina abobee katika Nyanja tofauti kwani yeye alikuwa mtaalamu
wa elimu tafauti, falsafa, Erfani, Hesabu, Utabibu, na… naye ndie pekee aliyeikosoa tiba ya Jalinusi katika kitabu
alichokiandika Ibun Siina kiitwacho( Qaanun)
***
Hivyo aviccena alizaliwa mwaka 370
A.H katika sehemu ya Balakh na kulelewa katika mazingira bora ya Kiisilamu
hatimaye kujifunza Elimu za dini na baadaye kujifunza Elimu za Sayansi na Tajiruba
na kupata umaarufu mkubwa duniani hapo zamani hadi sasa. na amefariki mwaka 428
A.H (Mungu amuweke mahala pema peponi).