bayyinaat

Published time: 05 ,March ,2017      23:45:39
Misingi ya tiba na udaktari ilianza pamoja na kuwepo mwanadamu katika sayari ya dunia, na kutoka karne kwenda nyengine elimu hii ilikuwa ikiimarika zaidi, na ulipofika Uislamu, kwa kuwa unasisitiza kutafuta elimu na kutafakari pia uashiriaji wake katika aya na hadithi za tiba na udaktari, kuliwafanya Waislamu nguvu katika kufanya.........
News ID: 36

Historia ya tiba katika Uislamu

Misingi  ya tiba na udaktari ilianza pamoja na kuwepo mwanadamu katika sayari ya dunia, na kutoka karne kwenda nyengine elimu hii ilikuwa ikiimarika zaidi, na ulipofika Uislamu, kwa kuwa unasisitiza kutafuta elimu na kutafakari pia uashiriaji  wake  katika aya na hadithi za tiba na udaktari, kuliwafanya Waislamu nguvu katika kufanya uchunguzi katika suala la tiba, usalama na afya ya mwanadamu

Baada ya kumshukuru Mola muumba, na kumtakia rehema na amani mtukufu Mtume (s.a.w.w) na ahali zake watakatifu.

Nachukua nafasi hii kuelezea kwa ufupi historia ya tiba kisha kuangalia mtazamo wa dini ya Kiislamu kunako tiba na afya ya mwanadamu. Swali muhimu linalopaswa kujiuliza ni kwamba elimu ya tiba na usalama wa mwanadamu ilianza zama na kipindi gani? Pia mtazamo wa Uislamu kuhusu tiba na suala la afya ni upi?

Ndugu msomaji naomba tushirikiane pamoja ili kupata tija itakayotunufaisha sisi na jamii kwa ujumla katika suala hili, Kuna khitilafu baina ya wataalamu na wana historia kunako kuanza kwa elimu hii (tiba)! Ambapo baadhi yao wakadai kwamba mwanzilishaji wa elimu hii ni Nabii Idrisa (a.s), huku wengine wakidai kuwa mwanzilishi wake ni: Harmas Lul, pia wengine wakainasibisha elimu hiyo na tamaduni za Babel, Yemen, Misri, Fars, India, Ugiriki  n.k.

Wengine wakasema kuwa elimu ya kidaktari imeanzishwa  na kutambulika kama sanaa, na  baada ya karne nyingi kupita ikapata mfumo na sura mpya na kuwa  elimu kamili.

Ndugu msomaji vyovyote iwavyo elimu ya tiba ilikuwa sambamba na kuwepo  mwanadamu katika sayari hii (ya dunia) kwa sababu magonjwa yanaambatana na maisha ya mwanadamu, hivyo kulikuwa kuna aina mbalimbali za tiba zilizokuwa zikitumika katika kujiponya.

Ila ni kwamba tiba ya zama hizo ni tofauti na sasa ukilinganisha na maendeleo ya zama zile na sasa. Hata hivyo kuna tofauti kati ya tiba ya zama hizo na zama hizi, ukilinganisha maendeleo yaliokuwepo zama hizo na sasa kwa sababu zama za Jalinus(201), Biqrati(277) na Plato (428) elimu ya tiba ndipo ilipangiliwa kiufanisi na kitaalamu nawala si kwa maana ya uanzilishi wa elimu hii, pia baada ya kudhihiri Uislamu udaktari ulipanuka zaidi, na hii ni kwa sababu kuwa Uislamu  unasisitiza utafutaji wa elimu katika nyanja tofauti, pia katika nyanja maalumu kama vile tiba na...

Mtume  mtukufu [s.a.w.w] anasema ; elimu ziko ya aina mbili; Elimu ya dini na ya miili.

 

 

 

Maendeleo ya tiba yaliboreka kama ifuatavyo:

  a) Kutoka zama za Mtume mtukufu mpaka mwaka[133 A.H] sawa na[750 A.D]

Zama hizi za zinaambatanisha kuanzia zama za uongozi wa Mtume mpaka zama za makhalifa wanne.

Katika zama hizi kwa sababu ya upya wa serikali ya Kiislamu, Waislamu walishindwa hawakuipa kipaumbele kwa sababu hiyo hakukupatikana daktari aliye bobea katika elimu ya tiba, isipokuwa kulikuwa na watu kadhaa walikifahamika kuwa madaktari wa zama zile mfano wa

1- Shimrdel

2- Dhamad bin Thaalabah

3- Ibun Abi Ramdhah Tamimi

b) Kutoka mwaka (133A.H) mpaka mwaka (287A.H) sawa na (900A.D)

Zama hizi zilifanyika kazi mbili nazo ni kama zifuatazo;

1) zama za tarijama:

Zama hizi Waislamu walianza kutarijumi vitabu vya Kigiriki, Kirumi na Kihindi ambapo aliyekuwa amesimamia kazi hii ni Mheshimiwa Abu Zaidi Husaini bin Is-haka na mwanawe.

2) Zama za utunzi na uandishi wa vitabu vya tiba ambapo Mheshimiwa Abu Hasan Ally bin Sahari bin Tabariy ambae aliandika kitabu kwa jina Firdawsil Hikmah, akiwa ni mwandishi wa kwanza katika elimu ya tiba kwa Waislamu.

c) kuanzia mwaka (287-700 A.H) 

ni zama ambazo Waislamu walipiga hatua na kuendelea katika taaluma ya tiba kiasi kwamba wasomi wa kimagharibi walivikia kusema kuwa: muda huu ni muda wa thamani na dhahabu kwa Waislamu kimaendeleo.

Dokta mmoja miongoni mwa madaktari wa kimagharibi katika zama ambazo wamagharibi walikuwa katika kipindi kibaya, kipindi  ambacho Waislamu katika miji tofauti ya kitamaduni ulimwenguni wakisonga mbele kimaendeleo ambapo Bagdad, Damaskas, Cairo na miji mengine ambayo ilikuwa na vyuo vya kidaktari na tiba pia kujenga mahospitali katika miji hiyo hali ambayo ikionyesha maendeleo ya hali ya juu katika elimu ya tiba na udaktari.

Anaendelea kusema kuwa Baghdad zilijengwa hospitali zaidi ya 60 na Cairo 33 hali ya kuwa ndani ya Ulaya hospitali ya kwanza ilijengwa mwaka 1793 (A.D) katika mkoa  wa Yuraki Uingereza.

Madaktari mashuhuri wa zama hizo

Katika zama hizo walipatikana madaktari tofauti miongoni mwao ni:

Ibn Sina, Razi, Ahwazi, Jurjaniy, n.k

d) Zama ambazo Waislamu walishuka kitaaluma kwa sababu zifuatazo:

1. Kukithiri kwa vita: Vita ziliokuwa zimetokea baina ya Waislamu na uma nyingine zilipelekea kushuka kielimu hususan katika elimu ya tiba na elimu ya kimea, kwani maadui wa Uislamu katika vita hizo walikuwa wakichoma moto Maktaba za Waislamu, baada ya kuchukua kila chapa ya vitabu viliokuwa humo, kitu ambacho kilikuwa ndio msingi wa kuporwa teknolojia mbalimbali walizokuwa nazo Waislamu na kwenda jamii zingine.

2. Kukithiri kwa khitilafu za kimadhehebu baina  ya Waislamu

3 –Kukimbia kwa wanazuoni na kwenda nchi nyengine: hali hii ilitokea kwa baadhi ya wataalamu kulazimika kuhama katika maeneo waliokuwa kwenda nchi za kigeni, kwa maana baada ya Waislamu kuporwa misingi ya kielimu waliokuwa nayo, pamoja na hayo maadui wa Uislamu hakuwa wenye kuwaacha huru Waislamu hao, bali waliwajengea mazingira ambayo walifanya baadhi ya Waislamu wachague kuhamia nchi zingine za kigeni kama unavyoona hivi sasa kunako wataalamu wa nchi za ulimwengu wa tatu wanavyo baki katika mataifa makubwa duniani, kwa madai mbalimbali ikiwemo urahisi wa upatikanaji wa kazi nk

4 –Kuchomwa moto maktaba za Kiislamu, kama nilivyo bainisha katika kipengere namba mbili moja.

Sababu hizi zilipelekea Waislamu kuporomoka kielimu na kuathiri maendeleo yao, kwa kiasi ambacho hivi sasa kinaonekana katika uma wa Kiislamu.

Hivyo basi baada ya kuporomoka Waislamu ndipo nchi za kimagharibi zikaanza kupamba moto na kuanzisha vitengo vya elimu ya tiba katika karne ya 16 nchini Uingereza mkoa wa Yurak.

Hii ni ishara inayoonyesha kuchelewa kimaendeleo katika nchi za kimagharibi ukilinganisha na Waislamu katika kipindi hicho.

Misingi  ya tiba na udaktari ilianza pamoja na kuwepo mwanadamu katika sayari ya dunia, na kutoka karne kwenda nyengine elimu hii ilikuwa ikiimarika zaidi, na ulipofika uislamu, kwa kuwa unasisitiza kutafuta elimu na kutafakari pia uashiriaji  wake  katika aya na hadithi za tiba na udaktari, kuliwafanya Waislamu nguvu katika kufanya uchunguzi katika suala la tiba, usalama na afya ya mwanadamu.

Waislamu waliingia katika elimu hii hata kufanikiwa kutoa madaktari maarufu duniani, mfano wa Ibn Sina (Avicena), baada ya hapo maadui wa Uislamu walipora elimu hii na nyinginezo kama elimu ya kemia hisabati na kujitangaza kuwa wao ndio wenyewe, hali yakuwa si hivyo, kwa minajili hiyo tunaweza kusema kuwa elimu ya tiba haina mwanzilishi maalumu kwani katika kila jamii kulikuwa na aina ya tiba ambayo ilikuwa inatumika sehemu hiyo, kwani ni jambo lisilo wezekana kuwa na taswira ya jamii bila ya tiba inayoendana na jamii hiyo.

  

 

 

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: