bayyinaat

Published time: 17 ,November ,2018      18:11:19
Ili kutayarisha mazingira na uwanja mzuri wa kudhihiri Imam wa Zama, Waislamu wanapaswa kujitayarishawao wenyewe kabla ya jambo lolote jingine. Sharti la kujitayarisha huko ni ......
News ID: 366

Kutayarisha mazingira ya kudhihiri Imam Mahdi ATFS

Ili kutayarisha mazingira na uwanja mzuri wa kudhihiri Imam wa Zama, Waislamu wanapaswa kujitayarishawao wenyewe kabla ya jambo lolote jingine. Sharti la kujitayarisha huko ni kujijengakimaanawi na kiroho na kumjua ipasavyo mtukufu huyo na sifa zake. Kwani mtu anayemjua vyema Imam na kiongozi wake wa zama ataelewa pia kwamba, mtukufu huyo ni mtetezi halisi wa haki na uadilifu na mpinzani wa dhulma, ubaguzi na uonevu. Hivyo mtu anayesubiri kudhihiri mtukufu huyo anapaswa yeye mwenyewe awe mpigania haki na uadilifu na anayepambana na dhulma, ufuska na ubaguzi popote pale alipo.

Mwokozi katika Uislamu ni mkombozi wa walimwengu wote ambaye ataitunuku dunia nzima hali bora na uadilifu kamili wa kijamii. Imam Mahdi (as) ni shakhsia wa dunia nzima ambaye zama zake zinakomesha kabisa mifumo na sura zote za dhulma. Imam Mahdi, atakuja kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu SW anayesema katika aya za 105 na 106 za Suratul Anbiyaa kwamba:

وَلَقَدْ كَتَبْنَا فِي الزَّبُورِ مِن بَعْدِ الذِّكْرِ أَنَّ الأَرْضَ يَرِثُهَا عِبَادِيَ الصَّالِحُونَ

إِنَّ فِي هَذَا لَبَلاغًا لِّقَوْمٍ عَابِدِينَ

Na hakika tulikwishaandika katika Zaburi baada ya Kumbukumbu, ya kwamba nchi watairithi waja wangu waliowema.Hakika katika haya yapo mawaidhakwawatu wafanyao ibada.

Kwa mujibu wa aya hizi za Qur'ani, waja wema wa Mwenyezi Mungu ndio watakaorithi na kushika hatamu za kuongoza dunia nzima. Na kwa mujibu wa tafsiri na hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume Muhammad (saw), suala hilo litatimia wakati atakapodhihiri Imam Mahdi (as) na utawala wa dunia ukashikwa na waja wema wakiongozwa na mtukufu huyo na hatimaye kukomeshwa dhulma na uonevu. Wakati huo mbingu na ardhi vitatoa neema zake zote, utajiri utagawanywa kwa uadilifu na ustawi na maendeleo vitaonekana kote duniani. Kipindi hicho wanadamu watafika katika daraja ya juu kabisa ya kubalehe kiakiri. Hadithi za Mtume Muhammad (saw) zinazozungumzia suala la kudhihiri kwa mtukufu huyo zinaeleza kuwa, wakati huo kila kaumu, koo na kabila litasikia sauti na wito wake kwa lugha yake. Wito wa mtukufu huyo utakuwa wa dunia nzima na utakuwa na taathiraulimwenguni kote. Imam Mahdi (as) atatimiza mchakato wa kuwaunganisha wanadamu wote chini ya kivuli cha Tauhidi na maisha bora ulioanzishwa na Mitume wa Mwenyezi Mungu.

Katika mantiki ya Uislamu, ubaguzi, dhulma na uonevu ni miongoni mwa sababu kuu za kuporomoka tamaduni mbalimbali, na hapana shaka kuwa, mtu anayeweza kueneza uadilifu duniani ni yuleambaye yeye mwenyewe anaamini, anapigania na kutekeleza uadilifu. Hizi ndizo sifa wanazopaswa kujipamba nazo wafuasi wa mwokozi wa aheri zamani na Imam Mahdi aliyeahidiwa kudhihiri katika zama hizo na kuijaza dunia uadilifu na usawa.

Imam Mahdi katika vitabu vya Masuni

Kuna hadithi nyingi katika vitabu vya hadithi vya Waislamu wa madhehebu ya Suni kuhusiana na Imam Mahdi AF. Wanazuoni wakubwa wa Kiislamu kama Tirmidhi naAbu Daud katika sahihi zao na Imam Ahmad katika kitabu cha al Musnad wamenukuu hadithi ya Mtume (saw) inayosema kuwa:

Hata kama itakuwa imebakia siku moja tu katika umri wa dunia, basi Mwenyezi Mungu atamleta mtu kutoka katika kizazi changu ambaye ataijaza dunia kwa uadilifu na usawa baada ya kujazwa dhulma na uonevu.

Vilevile Muslim katika kitabu cha Sahihi Muslim, Abu Daud, Ibnu Majah na Tabarani ambao ni miongoni mwa maulama wakubwa wa hadithi wa Ahlusunna wamenukuu hadithi ya Mtume (saw) inayosema: Mahdi ni katika kizazi changu kutokana na watoto wa Fatima.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: