bayyinaat

Published time: 21 ,November ,2018      19:05:01
News ID: 373


Mwakilishi wa Minnesota katika Kongresi ya Marekani, Ilhan Omar amesema ataanzisha jitihada za kuhakikisha kuwa sheria ya kupigwa marufuku uvaaji wa mitandio kichwani ikiwemo Hijabu inayovaliwa na wanawake Waislamu katika Bunge la Wawakilishi wa Marekani, inaangaliwa upya.

Ilhan Omar amesema ataunga mkono hoja ya chama cha Democrat ya kutaka kufutwa marufuku hiyo, huku akisisitiza kuwa huu ndio mwanzo wa kushinikiza kuangaliwa upya sheria kandamizi za nchi hiyo.

Amesema, "Hakuna anayenivalisha kwa nguvu Hijabu kichwani, huo ni uamuzi wangu uliolindwa kisheria."

Sheria hiyo ya miaka 181 inawapiga marufuku wawakilishi wa Marekani kufunika vichwa vyao au kuvaa Hijabu wanapoingia katika jengo la Kongresi au wanapolihutubia bunge hilo.

Baraza la Uhusiano wa Kiislamu nchini Marekani (CAIR) limesema linaunga mkono kufutwa marufuku hiyo, likisisitiza kuwa sheria hiyo imepitwa na wakati na inakiuka katiba na uhuru wa kuabudu.

Ilhan Omar ambaye amewahi kuwa mkimbizi katika kambi ya Dadaab nchini Kenya alishinda kiti hicho na kumbwaga mpinzani wakeJennifer Zielinski, baada ya kusisitiza katika kampeni zake kuwa iwapo ataibuka mshindi, atashinikiza mageuzi katika mfumo wa sheria, huduma za afya, na kulindwa haki za wahamiaji nchini Marekani.


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: