bayyinaat

Published time: 19 ,December ,2018      19:10:46
Katika makala hii nataka kuelezea vipindi vitatu muhimu ambavyo alipitia Imamu Askary katika njia yake ya kutekeleza majukumu ya Mwenyezi Mungu, lakini kabla ya kuingia katika vipindi hivyo
News ID: 376

Tarehe 8 mwezi wa Rabiul Thani (Mfungo saba) ni siku ambayo ulimwengu wa Kiislamu unakumbuka kuzaliwa kwa moja ya viongozi walioachwa na Mtukufu Mtume Muhammad (saww) kwa walimwengu, Imamu Hassan Bin Ally maarufu kwa jina la Askary.

Imamu ambaye kutokana na njama za maadui hakuweza kuishi zaidi ya miaka 28, lakini kutokana na rehema za Mwenyezi Mungu katika kipindi hicho kifupi aliweza kuandaa mazingira muhimu ambayo kwayo tunaweza kusema kuwa ulikuwa ni msingi sahihi kwa ajili ya mkombozi wa Ulimwengu, Al Imamu Muhammad Bin Hassan Al Mahdi (atfs). Kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutaelezea japo kwa kifupi kunako njia ambazo alipita katika kufanikisha kwamba mkombozi huyo hafikiwi na mikono ya maadui.

Katika makala hii nataka kuelezea vipindi vitatu muhimu ambavyo alipitia Imamu Askary katika njia yake ya kutekeleza majukumu ya Mwenyezi Mungu, lakini kabla ya kuingia katika vipindi hivyo ni lazima kuonyesha kwanza, je, huyu ambaye tunasema anatekeleza majukumu ya Mwenyezi Mungu ni kweli anastahiki kazi hiyo?, kwa maana ya kwamba je, Imamu Hassan Askariy ni katika wale ambao Mtume alituusia kama Waislamu au la?.

Maulama wameandika na kuzungumzia mara nyingi mno kunako uhalali wa watu hawa katika swala zima la kuteuliwa na Mwenyezi Mungu, kama ambavyo kuna Riwaya nyingi mno zenye mpaka kuwataja majina yao wa kwanza mpaka wa mwisho wao. Mimi hapa nitatosheleza na maneno ya moja ya Maimamu, nikiwa na maana kwamba moja ya njia za kuthibitisha uimamu wa imamu ni pamoja na maneno ya Imamu aliyetangulia. Ila kama utataka kujua zaidi vipi umethibiti uimamu wa huyu ambaye nachukua maneno yake basi unaweza kurejea katika vitabu vilivyoelezea kwa kipana dalili za Uimamu wa Maimamu 12.

Imepokelewa kutoka kwa Imamu Ridha (as), imamu wa nane katika maimamu 12, anasema:

إن الإمام بعدي ابني عليّ أمره أمري وقوله قولي، طاعته طاعتي، والإمامة بعده في ابنه الحسن

"..Hakika Imamu baada yangu ni mwanangu, atakayoamrisha ndiyo ambayo nayaamrisha, na atakayosema ndio ambayo nayasema, pia kumtii yeye ni kama kunitii mimi. Na kisha Uimamu baada yake utakuwa kwa mtoto wake Hassan.....”[1]

Hii ni moja tu ya dalili kati ya dalili nyingi katika kuashiria usahihi wa Imamu Askariy kunako cheo cha Uimamu na kusimamia majukumu ya Mwenyezi Mungu katika ardhi hii. Na sasa tunaweza kuangalia zama au vipindi vitatu muhimu katika maisha yake.

1. Zama za kuamiliana na watawala

Ni jambo ambalo lipo wazi kwa kila mwenye kurejea historia, kwani atakuta kwamba katika kila zama za Imamu basi kulikuwa na mtawala au watawala ambao kwa namna moja au nyingine walikuwa na lengo la kuhakikisha kwamba Maimamu wanakuwa chini yao, na mwisho wa siku swala zima la Uimamu linakufa kama ambavyo mafundisho ya Mwenyezi Mungu pia yanapotea.

Vivyo hivyo ukirejea zama za Imamu Askariy utakuta kwamba mfano wa viongozi hao walikuwepo, tena hasa baada ya watawala hao kutambua kwamba kupitia Imamu Askari yatapatikana yule ambaye wanamsoma katika vitabu vya imani zote kwamba atakuja kuondosha dhulma na tawala zote zisizo za kisheria katika uso wa ardhi, hivyo kufanya zama za Imamu Hassan kuwa ngumu kupita kiasi.

Itaendelea…..[1] Ikmalu Din Juz 2 Mlango wa 2


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: