bayyinaat

Published time: 19 ,December ,2018      19:29:07
Inaelezwa kwamba Al Mar-ashiy alikuwa akifanya sana ibada na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa lengo kwamba siku moja aonyeshwe kaburi la Binti wa Mtume Bi Fatma Zahra (as), kiasi kwamba
News ID: 381

"....Karimatu Ahli Bait...”:

Hii ni lakabu nyingine ambayo ni mashuhuri sana kwa Bi Fatma Maasuma, ikiwa na maana ya Mkarimu wa watu wa nyumba ya Mtume (saww). Kuna kisa ambacho kimepokelewa kutoka kwa Sayyid Mahmud Almarashiy ambacho ndani yake kumetajwa lakabu hii kwa mdomo wa Imamu wa zama (atfs).

Inaelezwa kwamba Al Mar-ashiy alikuwa akifanya sana ibada na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa lengo kwamba siku moja aonyeshwe kaburi la Binti wa Mtume Bi Fatma Zahra (as), kiasi kwamba alikuwa amejiwekea utaratibu wa kwenda Masjidul Sahla (Mjini Kufa) kwa muda wa usiku 40, na kwa bahati nzuri siku ya mwisho akapata nafasi ya kukutana na Imamu Mahdi (atfs) ambaye alimwamia kwamba ashikamane na Karimatu Ahlibait.

Al Mar-ashiy akadhania kwamba aliyekusudiwa hapa ni Bi Fatma Zahra (as), hivyo akamjibu Imamu kwa kumwambia kuwa hata yeye yupo katika harakati za kujua mahala alipo ili aweze kwenda kumzuru. Imamu akamwambia "...Makusudio yangu ni kaburi la Bi Fatma Maasuma aliyezikwa Mjini Qom,.....”. na kuanzia hapo Sayyid Al Mar-ashiy akaazimia kufunga safari ya kutoka Najaf mpaka Qom kwa ajili ya kumzuru Bi Fatma Maasuma.

Hizi ni baadhi ya fadhila ambazo zinapatikana kwa mwanamke kama huyu ambaye aliaga dunia hali ya kuwa akiwa ni mdogo, kama ambavyo pia hakuwa hata ameolewa, moja ya mambo ambayo yanahesabika ni shubuha kuhusu mwanamke huyu, na kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu tutajaribu kuelezea sababu ya kutoolewa kwa mwanamke huyu katika nafasi nyingine.

Wasalamu alaykum.

Sh Abdul Razaq Bilal (AbuuAsghar).


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: