bayyinaat

Published time: 19 ,December ,2018      19:32:08
Je, unaweza tambua tofauti ya maneno hayo hapo juu kwa mtazamo wa kwanza?, au ni sahihi unayatumia maneno haya kwa mwenza wako?.
News ID: 382

Hakuna mwenye shaka juu ya mahusiano mazito yaliyopo baina ya Mwenyezi Mungu (swt) na walimwengu, kwa maana ya kwamba laiti kama Mungu atasema hata kwa wakati mchache tu awaache walimwengu kama walivyo basi hatutaweza kudumu hata kwa sekunde kadhaa.

Na moja ya dalili za kuashiria kwamba Mwenyezi Mungu anajali walimwengu ni huruma na mapenzi yake juu yao mpaka kufikia hatua ya kuwatumia Mitume pamoja na Vitabu Vitukufu kwa lengo tu la kuwaongoa na kuwaweka katika njia sahihi.

Moja ya Vitabu ambavyo vimekuja ulimwenguni kwa lengo la kuwaongoa watu ni kitabu ambacho alikuja nacho Mtukufu Mtume Muhammad (saww), kitabu ambacho kilikuwa muujiza kuanzia wakati ule kinashuka mpaka leo hii tunavyozungumza.

Quran Tukufu, ndio kitabu ninachokimaanisha katika uwanja huu, kitabu ambacho muujiza wake unaweza kuzungumzika katika sehemu mbalimbali, lakini mimi katika nafasi hii finyu nitazungumzia muujiza na umakini wa Quran katika utumiaji wa maneno yake. Ndio, huwezi kuwa mtaalamu wa kuongea na kushangaza watu kwa umakini wako ikiwa kwamba neno fulani unaliweka katika maana nyingine na kusema kwamba ulikuwa unamaanisha maana uitakayo wewe, bali kama unataka maana fulani basi ni lazima utumie neno husika katika maana ile.

Na katika kuanza mada yangu nitapenda kuyatambulisha kwenu maneno matatu ambayo tukiyaangalia kwa mtazamo wa kwanza basi hatutaweza kugundua tofauti iliyopo baina yake, lakini baada ya kuona namna ambavyo Quran imeyatumia vipi basi tutazinduka na kujua uhalisia wake.

"..Mwanamke..” "..Mke..” "...Mwenza..”

Je, unaweza tambua tofauti ya maneno hayo hapo juu kwa mtazamo wa kwanza?, au ni sahihi unayatumia maneno haya kwa mwenza wako?. Nauliza maswali haya nikiwa nalenga hasa ambao wanaishi maisha ya pamoja au wanandoa kwa maana rahisi, maana wao ndio ambao wanakuwa na matumizi mbalimbali ya maneno haya katika maisha yao, kuna wakati mtu anasema kuwa huyu ni mwanamke wangu, wakati mwingine anasema huyu ni mke wangu, na wakati mwingine husema kuwa huyu ni mwenza wangu. Je umehisi tofauti iliyopo baina ya maneno hayo?.

Quran kupitia aya zake inaweza kuwa mwalimu mzuri wa kujibu maswali haya, kwa kutuwekea misingi ya kujua, Mwanamke ni nani ,Mke ni nani na mwenza ni nani?.

Mwanamke: Ni yule ambaye anakuwa na mahusiano ya kimwili na mwanaume, lakini baina yao hakuna mahusiano ya kimawazo na mwendano wa mapenzi. Hapa sasa anaitwa mwanamke, na mwanamme ndio husema huyu ni mwanamke wake.

Quran inasemaje?

ضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا لِلَّذِينَ كَفَرُوا امْرَأَتَ نُوحٍ وَامْرَأَتَ لُوطٍ ۖ كَانَتَا تَحْتَ عَبْدَيْنِ مِنْ عِبَادِنَا صَالِحَيْنِ فَخَانَتَاهُمَا فَلَمْ يُغْنِيَا عَنْهُمَا مِنَ اللَّهِ شَيْئًا وَقِيلَ ادْخُلَا النَّارَ مَعَ الدَّاخِلِينَ

Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio kufuru: mke wa Nuhu na mke wa Lut'i. Walikuwa chini ya waja wetu wema wawili miongoni mwa waja wetu. Lakini wakawakhuni waume zao, nao wasiwafae kitu. Na wakaambiwa: Ingieni Motoni pamoja na wanao ingia![1]

وَضَرَبَ اللَّهُ مَثَلًا لِلَّذِينَ آمَنُوا امْرَأَتَ فِرْعَوْنَ إِذْ قَالَتْ رَبِّ ابْنِ لِي عِنْدَكَ بَيْتًا فِي الْجَنَّةِ وَنَجِّنِي مِنْ فِرْعَوْنَ وَعَمَلِهِ وَنَجِّنِي مِنَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ

"….Na Mwenyezi Mungu amewapigia mfano walio amini - mkewe Firauni, alipo sema: Mola wangu Mlezi! Nijengee kwako nyumba Peponi, na uniokoe na Firauni na vitendo vyake, na uniokoe na watu madhalimu”.

Mwenyezi Mungu ametumia neno "Mwanamke” kwa wake wa Mitume wake, na hii ni kutokana na kutokuwepo kwa mfanano wa kimapenzi na hata kimawazo, kwani Mitume ni watu wema lakini wao hawakuwa hivyo, bali walikuwa njia tofauti na njia ambayo waume zo wapo, na mwisho wake wameingia motoni. Kama ambavyo pia neno mwanamke limetumika kwa mke wa Firaun kutokana kuwa tofauti na Firauni kimtazamo.

Inaendelea.....

[1] Surat Tahrim aya 10


maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: