Falsafa Ya Kuumbwa Shetani
Shetani ni kiumbe
ambae analaaniwa misikitini na makanisani, na sehemu mbalimbali za ibada, na
hajabahatika katika yake kupata watu wanaomuabudu kama ilivyo ng`ombe, moto,
masanamu na mengineo. Na mara nyingi watu hujiuliza kwamba kuna haja gani Mungu
kumuumba kuimbe huyu anayelaaniwa na kila mtu? Hali hiyo ndio imepelekea mimi
kuchagua mada hii ili kuitolea ufafanuzi.
SHETANI
Kwa nini Mungu
kamuumba Shetani?
Je kama Mungu asinge muumba
Shetani hauoni kwamba ungekuwa wacha Mungu sana?
Je Mungu kamuumba
shetani kwa kuwa anamuhitaji awepo au kwa kuwa anamuhitaji awepo au kwa
kuwa wanadamu wanamuhitajia?
JAWABU
Maswali kama haya
yanatokana na watu kuitakidi kwamba kuwepo shetani ni jambo baya, na Mwenyezi
Mungu hafanyi isipokuwa kheri na kuwepo shetani ni kinyume na itikadi yetu
kuhusu Mungu.
Majibu ya mwaswali
hayo ni mengi, na huu ni muhtasari:
1-Ndugu zangu, kuwepo
shetani katika ulimwengu huu ni jambo zuri, na ni kheri lakini uzuri au kheri
inamrejea yeye mwenyewe (shetani). Na halikadhalika kila kilichopo (kama
Malaika, majini binadamu, mimea, wanyama) bilashaka kuwepo kila kimoja katika
hivyo vilivyotajwa ni kheri kwake na kwa faida yake, kuliko kutokuwepo moja kwa
moja.
Ama ubaya au uchafu
utakaotokana na kuwepo kitu kile, utabakia kuwa ubaya vilevile, lakini bado
asili inayotuhukumu, itaendelea kuwa ni ile tulioiashiria hapo kabla. Na mfano
wa haraka kuthibitisha hilo ni kama ifuatavyo;
*Ni wanadamu wangapi
wanaumbwa na baadaye kuwepo kwao kunahatarisha maisha ya wenzao, lakini
haimaanishi kwamba asili ya kuwepo kwao ni ili waje kuwa na mazingira kama
hayo. Na halikadhalika shetani kuwepo kwake ingawa ni hatari kwetu, lakini ni
kheri kwake, na kwa sababu kama hiyo, ndio maana tunamkuta shetani alitumia
fursa ya kuwepo kwake kujikamilisha, kwa kumuabudu sana Mwenyezi Mungu , na alinufaika upande huo na huenda
ibada aliyofanya hakuna yeyote katika wanadamu alimfikia isipokuwa wachache
mno, kwa mfano, riwaya zinasema kwamba ,(Ibilisi) alisali rakaa mbili kwa muda
wa miaka elfu moja ndipo alimaliza rakaa hizo. Mpaka Mwenyezi Mungu
akampandisha cheo, akamfanya kuwa Malaika wa kweli, na kama hatutaamini hivyo
basi Mungu alipowaamrisha Malaika wamsujudie Adam, kisha Ibilisi akakataa
kusujudu, basi Mungu hana haki ya kumlaumu kwa amri iliotolewa iliwahusu
Malaika na yeye si Malaika ni jini, kwa hiyo hatuna haki ya kumuita muasi,
lakini kwa kuwa Mungu kutokana na ibada yake alimfanya kuwa Malaika wa kweli,
ndio maana Ibilisi mwenyewe hakusema hoja
kama hiyo.
Tunarejea katika
maudhui yetu, sasa mpaka hapo tunaona kwamba kama Ibilisi asingekuwepo angewezaje kumuabudu Mungu kiasi
hicho? Ukamilifu alioufikia mpaka Mungu kumfanya kuwa Malaika angefikaje kama
angelikuwa hayupo? Mpaka hapo imethibiti kwamba Mungu haja umba kitu kibaya ,
na wala haja umba kwa lengo baya, kwa hiyo swali kwa nini alimuumba shetani?
Jawabu kwa kuwa kuwepo ni kheri kwake kuliko kutokuwepo, kama tulivyobainisha.
Kwa nini Shetani
aendelee kuwepo mpaka siku ya mwisho?
Jawabu:
*Kama atatokea mtu
asali swala za usiku kwa lengo Mungu amfungulie milango ya riziki, siku ya
Kiyama atamuuliza Mungu, ziko wapi thawabu za swala za usiku nilizo Sali
duniani? Mungu atamjibu nilikufungulia milango ya riziki kama ulivyoniomba, na
hizo ndio thawabu zako( yaani huna haki ya kunidai thawabu akhera maadamu lengo
lako ulikusudia malipo ya duniani), na halikadhalika yeyote atakayefanya mema
kisha akalenga kitu kingine tofauti na ridhaa ya Mungu au pepo, basi malipo
yake ni kile anachokikusudia.
Na shetani pia
alimuabudu sana Mwenyezi Mungu na siku hadi siku akawa akipanda daraja za ibada
( na ni wazi kwamba ibada zote hizo hakuzifanya bure pasi na malengo au madai
yoyote kutoka kwa Mungu), kwa hiyo na yeye pia ana haki ya malipo kama vile
yule aliyesali swala za usiku na malipo yake ikawa ni kufunguliwa milango ya
riziki na kuendelea.
Kwa hivyo na shetani
pia alimuomba Mungu, na Mungu akampa kama alivyowapa wengine.
Sasa madai au maombi
ya shetani kutoka kwa Mungu ni nini?
Shetani alimuomba
Mungu mambo mawili;
1)Alimuomba Mungu
ampe umri mrefu, akisema;
Ewe Mola wangu!
Nakuomba unipe kabakia (au kuwepo) mpaka siku ya ufufuo (Kiyama). Mungu
akamjibu, hakika wewe utakuwa ni miongoni kwa watakaobakia mpaka siku hiyo
iliyopagwa.
2)Kisha shetani
alimuomba Mungu ruhusa ya kuichezea au kuimiliki mioyo ya binadamu na nafsi zao
kama alivyosema;
(Mola wangu!)
nitawarubuni wote kwa ujumla isipokuwa waja wako waliotakaswa. (Rejea surat
Al_Hijiri, aya 30-36).
Kwa hiyo Mungu alimpa
Ibilisi alioyataka kama malipo ya amali zake alizozifanya, na ni wazi kwamba
alikuwa nastahiki kulipwa (kama tulivyosema hapo kabla) na Mungu alimpa kwa
kiasi kile alichomuomba, na hayo uliyoyasikia ndio maombi yake. Kwa hiyo, hiyo
ndio falsafa ya kuumwa shetani na kuendelea kuwepo mpaka siku ya Kiyama, na huu
ni muhtasari mno.
Sh Swaleh Maulid