bayyinaat

Published time: 06 ,April ,2017      19:26:10
Mwanamke katika zama za ujinga alikuwa akionekana ni kama chombo cha starehe na bidhaa ambayo kila mtu alikuwa ana uwezo wa kumiliki bidhaa hiyo wakati wowote ule aliokuwa anahitaji. Wanaume walikuwa wakioa wanawake bila ya idadi maalumu na kuacha bila ya talaka. Mwanamke alikuwa haruhusiwi kumiliki kitu chochote na wala hana haki ya ..............
News ID: 75

UMUHIMU WA MWANAMKE KATIKA UISLAMU

Kwanza kabisa ningependa kumzungumzia mwanamke kabla ya kuja Uislamu na baada ya kuja Uislamu. Mwanamke katika kipindi cha kijahili alikuwa akidharauliwa na kuonekana kama ni mtu asiyekuwa na thamani wala hana haki ya aina ya aina yeyote ile mpaka Uislamu ulipoingia. Baada ya kuja Uislamu mwanamke alikuwa akitizamwa kwa mtazamo mwingine kabisa, kwani mwanamke aliweza kupata haki zake zote za msingi, na kupata heshima na pia aliweza kuokolewa kutokana na unyanyasaji, ukandamizaji ambao alikuwa akiupata katika kipindi cha zama za ujinga. Uislamu uliweza kumfanya mwanamke sawa na mwanaume katika nyanja mbalimbali za kidini na katika malipo mema na mateso.

Hali ya mwanamke kabla ya kuja Dini ya Uislamu

Mwanamke katika zama za ujinga alikuwa akionekana ni kama chombo cha starehe na bidhaa ambayo kila mtu alikuwa ana uwezo wa kumiliki bidhaa hiyo wakati wowote ule aliokuwa anahitaji. Wanaume walikuwa wakioa wanawake bila ya idadi maalumu na kuacha bila ya talaka. Mwanamke alikuwa haruhusiwi kumiliki kitu chochote na wala hana haki ya kurithi chochote na pia anaweza kuolewa na wanaume zaidi ya mmoja. Mwanamke hakuwa na cheo katika zama za kijinga bali alikuwa akionekana ni mtu ambaye analeta aibu katika jamii. Ikafikia hadi wanaume wakipata watoto wa kike walikuwa wakiwazika wakiwa hai ili kuepuka kupata aibu katika familia zao.

Mwenyezi mungu anatuambia katika Quran yake tukufu katika Sura ya NAH-L aya ya 58na 59 kwamba:

وَإِذَا بُشِّرَ أَحَدُهُمْ بِالْأُنْثَىٰ ظَلَّ وَجْهُهُ مُسْوَدًّا وَهُوَ كَظِيمٌ(58)

يَتَوَارَىٰ مِنَ الْقَوْمِ مِنْ سُوءِ مَا بُشِّرَ بِهِ ۚ أَيُمْسِكُهُ عَلَىٰ هُونٍ أَمْ يَدُسُّهُ فِي التُّرَابِ ۗ أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ (59)

"Na mmoja wao anapopewa habari ya (kuzaliwa mtoto wa kike) uso wake huwa mweusi, naye kajaa chuki, akawa anajificha asionekane na watu kwa sababu ya habari mbaya aliyoambiwa. Je, akae naye juu ya fedheha hiyo au amfukie udongoni? Tazama uovu wa wanavyohukumu”.

Hii ndio hali halisi aliyokuwa nayo mwanamke kabla ya kuja dini ya Uislamu. Na hali hii ilikuwa sawa katika mataifa yote sawa na mataifa ya Kiarabu na yasiyokuwa ya Kiarabu.

Hali ya mwanamke katika Uislamu

Baada ya mwanamke kukaa katika dhulma kwa muda mrefu bila kupata haki zake wala ukombozi wowote ule. Mwenyezi mungu subhaanahu wataala alimuagiza mtume Muhammad (saww) na dhulma na udhalili aliokuwa akiupata kutoka katika jamii aliyokuwa akiishi. Dini ya Uislamu inampa mwanamke haki zake zote za kimsingi na za kijamii. Haki hizo ni kama:

1)MWANAMKE NA MWANAMUME NI SAWA KATIKA KUTEKELEZA MAJUKUMU YA DINI

Katika sura ya NAHL aya ya 97 kwamba :

مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِنْ ذَكَرٍ أَوْ أُنْثَىٰ وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً ۖ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُمْ بِأَحْسَنِ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ

"mwenye kufanya mema mwanamume au mwanamke hali ya kuwa ni muumini basi tutamhuisha maisha mema, na bila shaka tutawapa malipo yao kwa sababu ya matendo bora waliyokuwa wakitenda”.

2)MWANAMKE ANAHAKI YA KURITHI

Katika sura ya NISAA aya ya 7 kwamba:

لِلرِّجَالِ نَصِيبٌ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ وَلِلنِّسَاءِ نَصِيبٌ مِمَّا تَرَكَ الْوَالِدَانِ وَالْأَقْرَبُونَ مِمَّا قَلَّ مِنْهُ أَوْ كَثُرَ ۚ نَصِيبًا مَفْرُوضًا

"Wanaume wana fungu katika yale waliyoyaacha wazazi ndugu na jamaa waliowakaribia, na wanawake wana fungu katika yale waliyoyaacha wazazi na jamaa waliowakaribia, ikiwa kidogo au kingi , (hili ni) fungu lililofaradhiwa”.

3)MWANAMKE ANA HAKI YA KUCHAGUA MUME WA KUMUOA

Uislamu unampa haki mwanamke kumchagua mwanamume anayempenda na anayemuona kuwa ni sahihi kwake na wanaweza kuoana na kuanzisha familia bila ya kulazimishwa na mtu yeyote. Tofauti na zama za kijinga ambazo mwanamke alikuwa akichukuliwa kama chombo cha starehe na cha kuondoa matamanio na chenye thamani ya chini kabisa.

4)MWANAMKE ANA HAKI YA KUJIKOMBOA KUTOKA KWA MUME MDHALIMU

Sheria ya Kiislamu imempa haki mwanamke ya kutoa talaka kwa mumewe ambaye hampi haki zake za kimsingi ambazo kwa sheria ya dini yeye kama mume anastahiki kuzitimiza kwa mke wake.

Haya ni baadhi ya mambo muhimu ambayo mwanamke amepewa katika Dini ya Kiislamu. Na hii ndio hali halisi ya mwanamke katika Uislamu. Uislamu umempa mwanamke hadhi na utukufu wake katika jamii, na ikatambua mchango mkubwa katika kuandaa kizazi cha kesho na kulea viongozi wa kuisimamia Dini ya Kiislamu. Amesema Mtume (saww) "Mcheni mwenyezi mungu katika kuwasimamia wanawake kwa sababu wao ni wasaidizi wenu”. Mtume amekiweka wazi cheo cha mwanamke nacho ni wasaidizi wa wanaume na sio watumwa au mtumishi au mtu asiye na haki kama wanavyodai watu wengine kuwa Uislamu umemfanya mwanamke kuwa ni mtumwa na hana haki yeyote.

Wasalaam

Imeandikwa na Dada Maryam .M. Mbepey

maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: