bayyinaat

Published time: 06 ,May ,2017      17:45:59
Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwingine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wanao jua.
News ID: 79

TALAKA TATU

_______

Ni kitu kilicho wazi kwa Waislamu kuwa mwanamke atakapoachwa na mumewe Talaka tatu haifai kwa mwanaume yule kumrejea tena isipokuwa baada ya kuolewa na mwanaume mwingine na akaachwa ndio anaweza kumuoa tena kwa mahari mpya ya kisheria . Na kinachokusudiwa katika neno Talaka tatu ni ile ambayo imetanguliwa na kuachana na kurudiana mara mbili na ikatolewa nyingine hiyo sasa ndio inaitwa talaka tatu.

Kama anavyosema Mwenyezi mungu katika Qur'an tukufu:

(الطَّلَاقُ مَرَّتَانِ ۖ فَإِمْسَاكٌ بِمَعْرُوفٍ أَوْ تَسْرِيحٌ بِإِحْسَانٍ

Talaka ni mara mbili. Kisha ni kukaa kwa wema au kuachana kwa vizuri

[Surat Al-Baqara 229]

(فَإِنْ طَلَّقَهَا فَلَا تَحِلُّ لَهُ مِنْ بَعْدُ حَتَّىٰ تَنْكِحَ زَوْجًا غَيْرَهُ ۗ فَإِنْ طَلَّقَهَا فَلَا جُنَاحَ عَلَيْهِمَا أَنْ يَتَرَاجَعَا إِنْ ظَنَّا أَنْ يُقِيمَا حُدُودَ اللَّهِ ۗ وَتِلْكَ حُدُودُ اللَّهِ يُبَيِّنُهَا لِقَوْمٍ يَعْلَمُونَ)

Na kama amempa talaka (ya tatu) basi si halali kwake baada ya hayo mpaka aolewe na mume mwingine. Na akiachwa basi hapana ubaya kwao kurejeana wakiona kuwa watashikamana na mipaka ya Mwenyezi Mungu. Na hii ni mipaka ya Mwenyezi Mungu anayoibainisha kwa watu wanao jua.

[Surat Al-Baqara 230]

Ama mtu akimuambia mke wake katika kikao kimoja nimekuacha mara tatu

( ﺃﻧﺖ ﻃﺎﻟﻖ ، ﻃﺎﻟﻖ ، ﻃﺎﻟﻖ ‏)

Hiyo inahesabiwa ni talaka moja na wala sio talaka tatu na hivyo ndivyo ilivyokuwa kipindi cha mtume (s.a.w.w) na kipindi cha ukhalifa wa Abubakar (r.a).

Lakini katika kipindi cha ukhalifa wa Omar bin Khattab (r.a) alifanya kuwa talaka tatu katika kikao kimoja yaani mwanaume akimuambia mke wake nimekuacha mara tatu ﺃﻧﺖ ﻃﺎﻟﻖ ، ﻃﺎﻟﻖ ، ﻃﺎﻟﻖ) ‏) inakuwa tayari keshamuacha talaka tatu kama ilivyo katika madhehebu za baadhi ya Waislamu.

Katika kitabu cha Sahih muslim imepokewa kutoka kwa Ibin Abass kwamba: katika kipindi cha Mtume (s.a.w.w) na kipindi cha Abubakar (r.a) na miaka miwili katika kipindi Umar(r.a) talaka tatu katika kikao kimoja ni moja . Lakini Umar akaifanya talaka tatu katika kikao kimoja ni tatu.

Taz: Sahih muslim kitabu talaq babul talqatu thalath Juz 3 Uk. 668

Na katika riwaya nyingine .Aliulizwa Ibin Abass :Je talaka tatu katika kikao kimoja hazijakuwa ni moja katika kipindi cha mtume na Abubakar akasema: Zilikuwa hivyo katika kipindi cha mtume talaka tatu ni moja. ilipokuwa kipindi cha Omar watu walizidisha kutoa talaka sana Omar akafanya talaka tatu katika kikao kimoja ni tatu.

Taz: Sahih muslim kitabu talaq babul talqatu thalath Juz 3 Uk. 670

Ni juu yetu kama Waislamu kuangalia je tuna haki ya kufuata suna ya nani katika dini ili tuweze kufanya jambo ambalo ni sahihi.

LABEL:
maoni Viewers
Name:
Email:
* Opinion: